Alhamisi, 03 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

"Uvumilivu" wa Watawala wa Ghuba Unajumuisha Vipengee na Sheria zote Isipokuwa Uislamu na Waislamu!

Chini ya kichwa cha urongo cha "Uvumilivu", watawala wa Imarati walizindua hekalu jipya la moja ya dini za kikafiri katika eneo la Jebel Ali. Hapo awali walitotora hisia za Waislamu walipofungua makanisa kadhaa kwa ajili ya Wakristo, na pia sinagogi la Mayahudi. Yalikuwa yameundwa na wizara iitwayo Wizara ya Uvumilivu mnamo 2016 ili kupigia upatu ufunguzi wa mahekalu ya ziada ya makafiri chini ya kichwa cha “Uvumilivu.”

Soma zaidi...

Chini ya Makucha ya Mfumo Muovu wa Kibepari Maisha Yanaendelea kuwa Magumu na Dhiki Zaidi

Gharama za maisha nchini zinaendelea kuwa juu zaidi kwa kupanda maradufu bei za vyakula na bidhaa nyengine hali inayowafanya raia wa kawaida wakaukiwe mifukoni na kuwaacha kutapatapa wasijue nini cha kufanya! Wakenya wanaitaka na kuiomba serikali iliyoko mamlakani kwa sasa itatue tatizo hili ambalo ndani ya mfumo wa kibepari limekuwa ni dimbwi la kudumu.

Soma zaidi...

Kukamatwa kwa Wabebaji Da’wah kutoka kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir na Mamlaka za Houthi ni Jinai ambayo kwayo watahesabiwa mbele ya Al-Aziz Al-Jabbar

Mnamo Alhamisi, Oktoba 23, 2022, mamlaka za Houthi nchini Morocco zilimkamata Ustadh Muhammad Musaad Al-Warafi (miaka 57), mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kutoka Msikiti wa Al-Hikma katika Jimbo la Ibb, baada ya kutoa hotuba ambayo kwayo ilifafanua Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara yake njema pale aliposema

Soma zaidi...

Makundi ya Kiislamu Yanawezaje Kuunga Mkono Katiba ya Kisekula?!

Katika taarifa ya pamoja kutoka kwa Chama cha People’s Congress na Ansar al-Sunnah Muhammadiyah – Kituo Makuu, pande hizo mbili ziliunga mkono suluhu ya kisiasa kwa msingi wa kikatiba; iliyoanzishwa na kundi lililoandaliwa katika Baraza la Chama cha Mawakili, na walitoa wito kwa vikosi vyote vya kitaifa kuunga mkono suluhu hii.

Soma zaidi...

Enyi Waislamu, Sarakasi ya Uchaguzi sasa ni ya Kipuuzi mithili ya Demokrasia Yenyewe! Uchaguzi utakuwa wa Haki na wa Maana chini ya Mfumo wa Khilafah

Sarakasi ya kisiasa kwa jina la demokrasia kwa mara nyengine tena imeregea Bangladesh kabla ya uchaguzi ujao wa kitaifa mnamo 2023. Joto la kisiasa linazidi kuongezeka mitaani huku chama kikuu cha upinzani, Bangladesh Nationalist Party (BNP), kikiruhusiwa ghafla na Serikali ya Hasina kuhamasisha umati kwa ajili ya kampeni dhidi ya serikali.

Soma zaidi...

Watoto wa Palestina Wanalilia Majeshi ya Waislamu

Tangu mwanzoni mwa 2022, zaidi ya watoto 45 wa Kipalestina wameuawa shahidi, na uvamizi wa Kiyahudi umeongezeka katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem, katika wiki chache zilizopita, ambao umesababisha vifo vya watoto zaidi, wa mwisho wao akiwa ni mtoto Mahmoud Al-Samoudi, mwenye umri wa miaka 12, ambaye alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.

Soma zaidi...

Mapigano Mapya ya Kimakundi kati ya Vipengee vya Mfumo na Makundi Yanayohusishwa ni Jinai dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham na Kupuuza Hatima yake

Maeneo ya Ngao ya Furat na Operesheni Tawi la Mzaituni, kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Aleppo, yameshuhudia mapigano makali kwa siku kadhaa kati ya vipengee vya mfumo wa makundi yanayohusishwa na utawala wa Uturuki, kutokana na kuhusika kwa wapiganaji wa Kitengo cha Hamza katika mauaji ya mwanaharakati wa vyombo vya habari Muhammad Abu Ghannoum na mkewe, ambaye alitumiwa kama kisingizio cha kutatua hesabu na kupanua ushawishi na udhibiti.

Soma zaidi...

Barua ya Mwaliko kutoka kwa Manispaa ya Amsterdam: Sera Dhahiri ya Uoanishaji!

Manispaa ya Amsterdam imealika bodi kadhaa za misikiti kutia saini taarifa ya kuunga mkono ambapo misikiti inalaani ghasia na ubaguzi dhidi ya jamii ya LGBTQ+. Barua hii ya Amsterdam kutoka kwa Meya Femke Halsema kwenda kwa ‘bodi zote za misikiti jijini’, ilikuja kujulikana baada ya Lody van de Kamp, rabbi (mwanachuoni wa Kiyahudi), kueleza hadharani ukosoaji wake dhidi ya kitendo hiki cha kibaguzi katika safu yake.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu