Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  9 Sha'aban 1444 Na: 04 / 1444 H
M.  Jumatano, 01 Machi 2023

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Denmark Yataka Kuutia Hatiani Wito wa Ukombozi wa Palestina

(Imetafsiriwa)

Mnamo Mei 2021, Hizb ut Tahrir / Denmark ilifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Misri jijini Copenhagen dhidi ya jinai zinazoendelea za uvamizi wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina. Nilitoa hotuba katika amali hiyo nikiwataka Waislamu wote kuyataka majeshi ya Waislamu katika nchi zinazoizunguka Palestina kuingilia kati kijeshi ili kuikomboa Palestina yote na kukomesha uvamizi wa Wazayuni.

Hii sasa imesababisha upande wa mashtaka ya umma kunifungulia mimi, Elias Lamrabet, mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir Denmark, mashtaka, ukitoa wito wa hukumu ya kifungo cha jela kwa kukiuka §136 Na. 1, kifungu kidogo cha Kanuni ya Adhabu, na §81, Na. 6; uchochezi wa kitendo cha jinai “kwa misingi ya asili ya kikabila, imani, ulemavu, mwelekeo wa kijinsia au kadhalika”.

Jinsi upande wa mashtaka utakavyojifanya kuwa uvamizi wa kijeshi unajumuisha “asili ya kikabila, imani, ulemavu, mwelekeo wa kijinsia au mengineyo” bado tungali kupata majibu yasiyokinaisha.

Kesi hii inasisitiza uungaji mkono usio na masharti wa serikali ya Denmark kwa uvamizi wa kikatili wa Kizayuni wa Palestina, na haiwezi kuchukuliwa kuwa kitu chengine chochote isipokuwa jaribio rasmi la kuharamisha wito wa ukombozi wa Palestina. Ni jaribio la wazi la kuwatisha Waislamu katika kuwanyamazisha, katika wakati ambapo kila aina ya matamshi ya chuki na matusi kwa Uislamu na Waislamu yanahalalishwa kwa maregeleo ya “uhuru wa kuzungumza”, ambao kwa muda mrefu umeonyeshwa kuwa ni chombo tu cha kisiasa.

Wakati Wazayuni wakiendelea na umwagaji damu na ukandamizaji wao wa kikatili huko Palestina, serikali ya Denmark inawataka Waislamu waogope hata kuzungumzia kuhusu ukombozi!

Hili, hata hivyo, ni jaribio lisilo na matumaini. “Israel” ni uvamizi wa kijeshi, na uvamizi wa kijeshi humalizwa kwa ukombozi wa kijeshi. Mithili ya Makruseda waliotangulia, uvamizi wa Kizayuni utafikia mwisho wake kwa kukusanywa kwa jeshi katika ulimwengu wa Kiislamu.

Hizb ut Tahrir inaendelea bila kusita, popote tulipo, kutoa wito wa suluhisho pekee la kweli la Palestina, ambalo Uislamu unaamuru: kuondolewa kabisa kwa uvamizi na ukombozi wa Palestina yote kwa nguvu za kijeshi.

Hakuna mashtaka yanayo chochewa kisiasa, hakuna vitisho au ushurutishaji, vitakavyotuzuia kusema ukweli na kuwatetea ndugu na dada zetu wanaokandamizwa.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu