Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  19 Sha'aban 1444 Na: 05 / 1444 H
M.  Jumamosi, 11 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Denmark Inashiriki katika Kuwakandamiza Waislamu wa China

(Imetafsiriwa)

Vyombo kadhaa vya habari vya Denmark vimeripoti kuwa kampuni kubwa ya kutengeneza pombe ya Denmark, Carlsberg, imeshiriki katika ukandamizaji mkali wa Waislamu wa Uighur nchini China.

Kampuni tanzu ya Carlsberg ya China ina viwanda vitano vya kutengeneza bia katika mkoa wa Kiislamu wa Xinjiang wa China (Turkestan Mashariki) na inachukua asilimia 85 ya mauzo yote ya bia. Pia ndio wafadhili rasmi wa tamasha la bia linalotumiwa na utawala wa China kuwafuatilia na kuwakandamiza Wauyghur.

Serikali ya China, pamoja na mambo mengine, imetumia kifungo, kufunga kizazi kwa nguvu, ufuatiliaji mkubwa wa watu, ubakaji na kuwalazimisha Waislamu kunywa pombe, hata wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Yote haya, kwa sababu tu wanaitakidi Uislamu.

Carlsberg sio tu ni kampuni ya Denmark, lakini inachukuliwa kuwa kinara wa kiuchumi wa Denmark na mafanikio ya biashara ya kimataifa.

Zaidi ya hayo, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya shirika la kushawishi la Danish Breweries na kipote cha kisiasa nchini Denmark, vikiwemo vyama vya serikali. Uhusiano ambao umefichuliwa kuwa kama ufisadi wa kitaasisi.

Habari kuhusu kuhusika moja kwa moja kwa Carlsberg katika unywaji pombe wa kulazimishwa na ukandamizaji wa kikatili wa Waislamu bila shaka zinapaswa kutoa mwitikio wa kisiasa, endapo kuna hata chembe ya ukweli katika wasiwasi rasmi wa Denmark kwa kile kinachoitwa "haki za binadamu".

Lakini kwa mara nyengine tena serikali ya Denmark inathibitisha kwamba sivyo hivyo, hasa wakati ambapo ni Waislamu ndio wanaokabiliwa na uhalifu na wakati ambapo maslahi ya kifedha yanapokuwa hatarini.

Haya yanajiri baada ya ufichuzi wa hapo awali wa jinsi baadhi ya kampuni kubwa zaidi za betri za miale ya jua (solar) nchini Denmark zinavyotengeneza betri zao za jua kwa kutumia nguvukazi ya kulazimishwa inayofanywa na Wauyghur waliowekwa katika kambi za kazi ngumu na serikali ya China.

Hatua hizi za kinyama zimekuwa na faida kubwa kwa makampuni makubwa ya Denmark, na zimefanyika kwa idhini ya serikali ya Denmark, ambayo kwa hiyo inahusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa Wauyghur.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir, tunauchukulia ushirikiano na utawala wa China juu ya ukandamizaji wa Wauyghur kama uadui wa wazi dhidi ya Waislamu duniani na njia nyengine tu ambayo kwayo serikali ya Denmark inaupiga vita Uislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu