Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  7 Muharram 1445 Na: 01 / 1445 H
M.  Jumanne, 25 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uchomaji Quran na Miitiko ya Kisiasa ya Kinafiki

(Imetafsiriwa)

Uchomaji moto wa hivi karibuni wa Quran nchini Denmark na Sweden, na miitiko iliyofuata nyumbani na nje ya nchi, inatoa wito wa utambuzi muhimu:

- Uhuru wa kusema ni chombo cha nguvu ya kisiasa na kifuniko duni cha ukosefu wa maadili ya kweli.

- Ni sera endelevu ya kupambana na Uislamu ya serikali mtawalia ambazo zimekuza chuki ya Uislamu katika sehemu za jamii na kuunda mvutano na mgawanyiko kati ya vikundi vya watu.

- Tangu michoro ya kuchukiza iliyoshajiishwa kisiasa, mnamo 2005, serikali ya Denmark imechochea na kuwezesha vitendo vichafu zaidi vya chuki vilivyoelekezwa kwa Waislamu, licha ya athari mbaya kwa jamii.

- Jaribio la serikali lisiloaminika kabisa la kuosha mikono yake kwa "kulaani" kwa Waziri wa Mambo ya nje Lars Løkke Rasmussen, baada ya maandamano makubwa ya ulimwengu, ni la kinafiki na linaloonekana kwa urahisi.

- Hatua na matamko tasa kutoka kwa serikali katika nchi za Waislamu hayana maana. Serikali hizi zinafanya uhalifu dhidi ya Quran mchana na usiku.

- Hatua zinazofaa dhidi ya ukiukwaji huu unaoendelea katika ngazi ya serikali; kidiplomasia, kiuchumi, na ikibidi kijeshi, kamwe hazitaonekana kwa kukosekana kwa nguvu ya kisiasa katika ulimwengu wa Kiislamu ambayo kwa kweli inawakilisha utashi wa Waislamu.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu