Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  26 Ramadan 1444 Na: 1444 / 19
M.  Jumatatu, 17 Aprili 2023

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)

Kwa kuamini qadhaa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Jordan inaomboleza pamoja na Umma wa Kiislamu kwa jumla na watu wa Jordan hasa Shab wa Hizb ut Tahrir, mmoja wa waaminifu wake, wenye subira na wenye matumaini.

Ndugu mtukufu:

Ustadh Omar Faleh At-Tal (Abu Abdullah)

Aliyeaga dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu jioni ya Jumapili, tarehe 25 Ramadhan 1444 H sawia na tarehe 16 Aprili 2023, akiwa na umri wa takriban miaka 70, ambayo aliitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Na yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alijiunga na Hizb ut Tahrir katika ujana wake, akibeba mwito wa haki na kheri, akivumilia kwa subira mateso, kukamatwa na kufungwa jela kwa ajili yake. Aliingia kwenye magereza ya madhalimu mara 16 kati ya hukumu za dhulma na kukamatwa kwa dhulma, akitarajia malipo kwa Mwenyezi Mungu, akitegemea ushindi Wake, Azza wa Jal. Aliteswa katika kifungo cha upweke na aliadhibiwa sana, na yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alibaki imara juu ya haki anayoibeba, akikaidi kwa wazi.

Mji wa Irbid unashuhudia kwamba alikuwa shujaa wa misikiti, na sisi hatumsifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakuacha msikitini wowote bila ya kutangaza haki ndani yake kwa sauti yake ya kuvuma. Hakuogopa lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na alitoa wito wa kuregeshwa upya kwa maisha ya Kiislamu na kuasisiwa kwa Dola ya Khilafah Rashida.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu, maiti wa Ummah, kwa rehema zake, na ampokee kwa mapokezi mema, na ayajaalie makaazi yake yawe ni Firdaws ya juu kabisa peponi pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, watu wema na hao ndio marafiki wema, na kumlipa kwa niaba yetu, Uislamu na Waislamu malipo bora, kama ambavyo tunamuomba Yeye (swt) kwa ajili yetu na jamaa zake, subira, faraja, na rambirambi njema. Na hatusemi ila tu aliyotuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah:156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

- Kalima ya Sheikh Abu Salem Al-Sakhri katika Kikao cha Tanzia cha Ustadh Omar Faleh At-Tal (Abu Abdullah) -

- Kalima ya Ustadh Bilal Al-Qasrawi (Abu Ibrahim) katika Kikao cha Tanzia cha Ustadh Omar Faleh Al-Tal (Abu Abdullah) -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu