Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 498
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut-Tahrir/Wilayah Tunisia imeandaa matembezi kwa kichwa “Enyi, Jeshi la Misri, Kinana... Adui yuko Machoni pako... Amemwaga Damu yenu na Kuwaua Ndugu zenu, Umefika Wakati kwenu Kuchukua Hatua!” baada ya swala ya Ijumaa yaliyoanza kutoka Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis hadi barabara ya Al-Thawra kama ilivyo kila Ijumaa.
Mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 27/5/2024, Wizara ya Afya huko Gaza ilitangaza kwamba idadi ya waliouawa kutokana na mauaji yaliyofanywa na vikosi vya uvamizi dhidi ya waliokimbia makaazi yao katika kambi ya mji wa Rafah imeongezeka hadi 45, wakiwemo wanawake 23, watoto na wazee, na waliojeruhiwa kufikia 249.
Kufuatia kampeni inayoendelea dhidi ya mauaji ya kihaiki, maumivu na dhulma za Waislamu wa Gaza zinazofanywa kikatili na umbile nyakuzi la Kiyahudi kwa msaada wa Marekani na mataifa mengine ya Kimagharibi, Hizb ut Tahrir / Tanzania imejitolea Ijumaa ya leo katika kuendesha dua maalum kwa Waislamu wa Gaza katika misikiti mbalimbali ya Tanzania.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Juni 2024 M.
Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, alitangaza ongezeko la bei ya mkate iliyofadhiliwa kutoka piaster 5 hadi piaster 20 kuanzia Juni ijayo. Madbouly aliongeza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwamba gharama ya mkate kwa serikali inafikia piasters 125, lakini iliuzwa kwa piaster 5 pekee, hivyo serikali ina gharama ya ruzuku ya pauni bilioni 120.
Mwanajeshi mmoja wa Misri aliuawa katika makabiliano ya risasi kati ya wanajeshi wa 'Israel' na Misri kwenye kivuko cha Rafah mnamo siku ya Jumatatu, kama ilivyothibitishwa na Shirika la Utangazaji la 'Israel'. (Sky News Arabia, 27/5/2024).
Takriban Kizazi (Gen Z) milioni 10 nchini Indonesia hawana ajira au wanajulikana kama NEET (wasio katika ajira, elimu na mafunzo). Ukweli huu unatokana na data ya BPS (2021-2022) ambapo kulikuwa na watu 9,896,019 mnamo Agosti 2023, ambayo ni karibu 21% ya idadi ya watu waliozaliwa kati ya 1997 na 2012.
Kamari ya leo sio juu ya ukoloni, wala afisi za balozi za Magharibi, bali ni juu ya Uislamu, ambao unatabikishwa na dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo muda wake ni umekuwa mrefu, na ambayo alfajiri yake iko karibu, Mwenyezi Mungu akipenda.