Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 517
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Siku chache zilizopita, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) viliwakamata Sheikh Aws Abu Arqoub na Sheikh Muhammad Manasrah, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kwa kuwakamata wale wanaosema ukweli, PA na vikosi vyake vinasisitiza kuwa kiongozi wa Mayahudi, wakidunga visu watu wote wa Palestina.
Ni zaidi ya uhaini, kwamba Mamlaka ya Ndani ya Palestina inatangaza uadui wake kwa watu wa Palestina, kama inavyotokea kwa kuwasaka Mujahidina wa Tubas, kuwakamata na kuwapiga risasi, kuwatawanya watu huko kwa gesi ya machozi, kuwaua Mujahidina na kuwatia nguvuni kama wafanyavyo Mayahudi, sawa kwa sawa, na kutenda kwa niaba yake kwa kujaza pengo wakati inashughulika na uvamizi wake dhidi ya Gaza na Lebanon.
Mwaka mmoja umepita tangu Kimbunga cha Gaza, ambacho kimetikisa misingi ya hadhara ya Magharibi na kuponda ponda simulizi ya jeshi lisiloweza kushindwa. Mwaka mmoja wa uchinjaji na mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza yametekelezwa na nchi za Magharibi zenye chuki na zingali zinaendelea kutekeleza kwa kulitumia umbile nyakuzi. Mwaka mzima wa kula njama na kufanya biashara ya umwagaji damu ambayo watawala wa Waislamu wamegeuka kuwa waovu, na kuwaongezea fedheha.
Baada ya swala ya Ijumaa, matembezi ya hamsini na tatu yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, mbele ya Msikiti wa Al-Fatah, matembezi makubwa yaliyoitishwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia, kwa watu wa Al-Khadra, na yenye kichwa “Kwa Khilafah, Majeshi yatasonga kuikomboa Palestina.”
Mtazamo wa Kimagharibi kuhusu jinsia unasalia kuwa umejaa ukinzani na unafiki, hasa unapotazamwa kupitia jicho la matukio ya hivi majuzi kama vile sintofahamu inayomhusisha bondia wa Algeria kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris. Bondia huyo ambaye ni mwanamke kibaiolojia, amekosolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na mamlaka za michezo kwa madai ya kumiliki viwango vya juu vya homoni za “kiume” na kupendekeza kuwa asiruhusiwe kushindana na wanawake wengine.
Ni moja ya mambo ya ajabu, na ya kushangaza sana, kwamba waziri katika nchi ambayo ilikuwa kubwa kwa muda mrefu hajui historia ya nchi yake, kuelezea hisia zake za mshangao na hasira kwa madhihirisho ya kusherehekea kurushwa makombora dhidi ya umbile la Kiyahudi.
Mmoja wa Mashababu aliyebeba Dawah ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, akistahamili madhara ya madhalimu jeuri mpaka yakini ilipomjia jana, Alhamisi, tarehe 30 Rabi ' al-Awwal 1446 H, sawia na 3/10/2024, kwenye Kisiwa cha Tuti jijini Khartoum.
Ni muhimu kwamba vijana wa Kiislamu wa leo wakumbushwe juu ya misheni waliokabidhiwa na Mtume wa mwisho (saw), na ukumbusho huu lazima utoke misikitini. Enyi Maulamaa, ni nani mwingine zaidi ya nyinyi anayeweza kutekeleza kazi hii muhimu?
Mwaka mzima umepita tangu tarehe 7 Oktoba 2023. Mwaka wenye mauaji ya halaiki na jinai zisizoelezeka dhidi ya Waislamu wa Palestina zinazoshuhudiwa na wote wenye macho ya kuona. Ni mafunzo gani tunaweza kupata tukitazama nyuma mwaka huu wa umwagaji damu na kutazamia mustakabali mwema kwa Palestina na Umma wa Kiislamu?