Jumapili, 04 Rabi' al-awwal 1448 | 2026/08/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Makongamano ya Kimataifa, Mipango ya Amani, Pasi na Kukomesha Wala Kupunguza Mashambulizi ya Mabomu ya Urusi!

Matukio ya umwagikaji damu yanayojiri Mashariki mwa Ghouta na Idlib; Mtandao wa Kutetea Haki za Kibinadamu wa Syria umesema kwamba raia wapatao 370 wameuwawa Mashariki mwa Ghouta tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ukitaja kuwa miongoni mwa wafu ni watoto 63 na wanawake 72. Katika eneo la Idlib, hususan mji wa Sarakib, ambao ndio uliolengwa kwa dhoruba hii tangu mnamo 25 Disemba, Warusi na serikali ya kihalifu ya Syria zimemwaga chuki zake dhidi yake, ikitangazwa na baraza lake la mji kuwa eneo lililo kabiliwa na janga, ambapo idadi ya vifo mwezi Januari ilikuwa ni watu wapatao 30 na zaidi ya raia 60 kujeruhiwa. Hii ni ikiongezewa na kulengwa kwa mashule na mahospitali, ambazo idadi yake kubwa haziendeshi tena shughuli zake.

Soma zaidi...

“Msafara Wenye Utu” Kwa Ajili ya Wanaodhulumiwa Syria na Wanawake Waliokamata Huku Viongozi na Majeshi ya Waislamu Wakiutelekeza Utu Wao kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali

Mnamo Jumanne, Machi 6, wanawake kutoka nchi 55 walitoka katika “msafara wenye utu” kuanzia Istanbul mpaka Hatay. Lengo lao likiwa ni kunyanyua rai jumla juu ya wanawake 6,736 wakiwemo wasichana 417 wanaoteseka katika magereza ya serikali ya Assad, wakisubiri kifo chini ya mateso na ubakaji wa kila siku. Magereza hayo yamejaa wanawake wazee, waja wazito na wanawake waliojifungua punde tu kabla ya vifungo vyao. Inajulikana kuwa wanawake wanaopitia uchungu wa ubakaji na mateso aghalabu hujiua wanapo pata fursa ya kufanya hivyo.

Soma zaidi...

Watoto wa Iraq … Uhalisia Unaoogofya na Mustakbali Unaotoa Bishara ya Miaka Mingi ya Kuzorota!

Hazina inayoshughulikia maswala ya watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema katika ripoti iliyotolewa mnamo Ijumaa 19/1/2018 kuwa watoto 270 waliuwawa nchini Iraq mwaka jana kwa sababu ya vita vilivyo anzishwa na serikali ya Iraq dhidi ya ISIS. Vita hivi pia vilisababisha watoto 1.3 milioni kukosa makao miongoni mwa 2.6 milioni waliokosa makao kutokana na vita hivi vya miaka mitatu. Kulingana na taarifa hiyo, watoto milioni nne katika mikoa ya Nineveh na Anbar waliathirika na ghasia hizo na watoto wengi walilazimika kushiriki katika vita safu za mbele. Taarifa hiyo ilifichua kwamba umasikini na mizozo ilisababisha kusita kwa mchakato wa elimu kwa watoto milioni tatu kote nchini Iraq, baadhi yao wakikosa kabisa fursa ya kukaa ndani ya darasa katika maisha yao yote, huku zaidi ya robo ya watoto wa Iraq wakiishi ndani ya umasikini.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu