Jumatatu, 23 Shawwal 1443 | 2022/05/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Matakwa ya Kuachiliwa Huru kwa Mhandisi Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah, Ambaye Angali katika Utekaji Nyara tangu 11 Mei 2012

11 Mei 2019 ni miaka saba tangu Mhandisi Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, alipotekwa nyara na maafisa wa usalama, mbele ya watoto wake na majirani. Katika miaka saba mirefu, Naveed hajaruhusiwa kuwasiliana na familia yake kwa vyovyote vile, hata mara moja, iwe kwa simu au ana kwa ana. Hakika, utekwaji nyara ni mateso ya hali ya juu, yenye kuiadhibu familia pamoja na muumini.

Soma zaidi...

Mwacheni Huru Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah Utekaji Nyara wa Miaka Mitano Hautazuia Kurudi kwa Khilafah kwa Njia ya Utume

Ni miaka mitano sasa tangu Ijumaa tarehe 11 Mei 2012, wakati majambazi wa watawala wa Pakistan walipomteka nyara Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan. Kile kinachoitwa "uhalifu" wa Naveed Butt ni kwamba alikuwa ni sauti yenye ushawishi mkubwa nchini Pakistan kwa ajili ya kusimamishwa tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

Soma zaidi...

Waacheni Huru Watetezi wa Khilafah: Haki inadai Kuachiliwa Huru Mara Moja kwa Wale Wanaolingania Khilafah kwa Njia ya Utume.

Mnamo tarehe 24 Disemba 2016, Jaji Mkuu Mteule wa Mahakama ya Upeo, Mian Saqib Nisar, alisema, “Ninaahidi hakutakuwa na shinikizo kwa idara ya mahakama na hakuna anayeweza kuthubutu kuhoji uwazi wetu. Siwezi kuutoa muhanga uhai wangu kesho Akhera kwa manufaa yoyote ya kidunia.” Hakika hakimu aliyeongoka ni yule anayehukumu kwa Uislamu ili apate Jannah. Na ole wake yule anayehukumu kwa yasiokuwa Uislamu!

Soma zaidi...

Naveed Butt Alitekwa Nyara baada ya Kuwafichua Wasaliti katika Uongozi wa Jeshi Juu ya Shambulizi la Amerika la Abbotabad

Mnamo tarehe 27 Aprili 2016, dondoo za kitabu kimoja cha mwandishi wa habari maarufu wa Marekani, Seymour Hersh, zilichapishwa katika gazeti la Kiingereza la Dawn, ambamo alisema kwamba amekinai sana zaidi kuliko hapo awali kwamba Pakistan iliisaidia Marekani kumpata Osama.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu