Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  22 Jumada I 1446 Na: HTS 1446 / 26
M.  Jumapili, 24 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waziri wa Masuala ya Kidini na Wakfu awa Mgeni wa Hizb ut Tahrir

(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha (Abu Ridha), Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, na pamoja naye Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), Msemaji Rasmi wa Hizb utTahrir katika Wilayah ya Sudan, na msaidizi wake, Ustadh Muhammad Jameh (Abu Ayman) ulimpokea Ndugu Dkt. Omar Bakhit Muhammad Adam, Waziri wa Masuala ya Kidini na Wakfu wa Kifederali katika afisi ya Hizb mjini Port Sudan, jana, Jumamosi, 21 Jumada al-Awwal 1446 H sawia na 23/11/2024 M.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Ustadh Nasser alimkaribisha Waziri, akawatambulisha wajumbe, kisha akazungumza kwa kuitambulisha Hizb ut Tahrir, ambacho ni chama cha kisiasa, kinachotaka kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, akitilia mkazo faradhi ya kuifanyia kazi Khilafah, na kwamba hizb inafuata njia ya Mtume, (saw), katika kusimamisha dola; kuanzia kusimamisha chama chenye msingi wa Uislamu, kisha kuingiliana na jamii kupitia mivutano ya kifikra na mapambano ya kisiasa, kisha kutafuta nusra kutoka kwa watu wenye nguvu na uwezo.

Kisha Ndugu Nasser akazungumza juu ya kile ambacho Magharibi, haswa Marekani, inapanga kuifanya misikiti na jumuiya za Kidini zifanye kazi kwa mujibu wa matamanio yake, na anachokusudia kafiri ni kubadili mazungumzo ya kidini.

Kisha yule ndugu waziri akazungumza, akithamini dori ya Hizb ut Tahrir, lakini anaona kwamba wakati unahitaji kusimama pamoja Jeshi. Ndugu Nasser alieleza ruwaza ya kisheria na kisiasa ya vita hivi.

Mwishoni mwa mkutano huo, ilisisitizwa kuendelea kwa mikutano hii.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu