Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  19 Dhu al-Qi'dah 1437 Na: 1437 / 03
M.  Jumatatu, 22 Agosti 2016

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Fahamu ya Utaifa Inafichuka Zaidi

Amri iliyotolewa na hayati Aboud Jumbe, aliyekuwa rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyefariki wiki iliyopita akiwa na miaka 96, ya jinsi mazishi yake yatakavyo fanywa imeonyesha zaidi uovu wa fahamu ya utaifa machoni mwa kila mmoja.

Licha ya hayati Jumbe wakati mmoja kuwahi kushikilia nyadhifa za juu katika Jamhuri ya Muungano na katika serikali ya Zanzibar, alitoa amri ya mwisho azikwe ndani ya jenezi lisilo finikwa na bendera bila ya alama yoyote ya serikali mazishini kwake akikataa mazishi yake kujitokeza aina yoyote ya ukafiri.

Msimamo huu wa mwendazake unafunzo kubwa kwa Waislamu wote, wawe wanasiasa, wasomi na watu wa kawaida juu ya dhambi kubwa la fahamu ya 'utaifa' ambayo imeharamishwa kwa dalili za kukatikiwa katika Uislamu.

Sisi Hizb ut Tahrir / Tanzania kwa mara nyingine tena tunawakumbusha Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kuwa licha ya fikra ya utaifa kuharamishwa katika Uislamu, vilevile ni silaha hatari ya kikoloni ya kuwakoloni na kuwagawanya Waislamu na wanadamu kwa jumla.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu