Afisi ya Habari
Tanzania
H. 27 Dhu al-Qi'dah 1437 | Na: 1437 / 04 |
M. Jumanne, 30 Agosti 2016 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Je, Mumemuona Mtetezi wa Demokrasia (Amerika)?
Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam umewaonya raia wake juu ya mzozo wa sasa wa kisiasa kati ya serikali na vyama vya upinzani. Umewaonya kujiepusha na maeneo ambayo huenda yakafanyika maandamano na kuchukua tahadhari kubwa katika sehemu za mijumuiko mikubwa ya watu na maandamano kufuatia maadamano yaliyo pangwa kufanyika kote nchini kuanzia Septemba 1, 2016.
Chama cha upinzani Chadema chini ya mwito wake UKUTA, ufupisho wa (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) kilitangaza Septemba 1 kuwa siku ya uasi ili kuonyesha kutoridhika kwao kwa kile wanachosema Rais Magufuli anazikanyaga haki za kidemokrasia na nyendo zake za kidikteta kupitia kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamo hadi 2020.
Amerika, inayoitwa mtetezi wa demokrasia na haki za kibinadamu imeyasukuma mataifa yanayo endelea kujifunga na demokrasia, badala ya kuzima taharuki juu ya mzozo wa sasa wa kisiasa kati ya serikali na chama hicho cha upinzani inaonekana kuwa wasiwasi wake pekee ni kwa raia wake huku maisha ya Watanzania yakiwa hayana thamani.
Fauka ya hayo, taarifa ya Amerika inaashiria waziwazi msaada wake kamili na kuunga mkono msimamo wa serikali wa kuahidi kupambana vikali na waandamanaji wa upinzani kwa nguvu ya mkono wa dola. Amerika kamwe haioni aibu, licha ya majibu ya serikali juu ya kampeni zilizo nuiwa za UKUTA kukashifiwa na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuwa ukiukaji wa haki za kibinadamu na mapendeleo dhidi ya upinzani. http://www.ippmedia.com/en/news/chadema-holds-magufuli-spits-fire.
Hizb ut Tahrir Tanzania inawaonya Waislamu na wasiokuwa Waislamu kuwa Amerika na mataifa yote ya kirasilimali kamwe hayajali isipokuwa maslahi yao, vilevile kadhia hii inafichua aibu, hadaa na batili ya demokrasia. Ala ya ukoloni mambo leo inayo sukumwa na mataifa ya kirasilimali katika mataifa yanayo endelea ili kurahisisha ufujaji wa rasilimali zake na kuwapurukusha watu kutokana na mfumo mbadala … Uislamu.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |