Afisi ya Habari
Tanzania
H. 4 Sha'aban 1437 | Na: 1437 / 01 |
M. Jumatano, 11 Mei 2016 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Mzozo wa Sukari Nchini Tanzania ni Njama ya Makusudi
Katikati mwa Februari 2016, serikali ya Tanzania ilitangaza rasmi kuwa haitaruhusu wafanyi biashara kuagiza sukari nchini isipokuwa wakiwa na leseni maalumu kutoka Ikulu. Hatua hiyo ilichukuliwa kwa msingi wa kile kinachoitwa 'kuvilinda viwanda vya ndani vya sukari'. Hili limepelekea mkurupuko wa bei ya sukari kupanda kwa zaidi ya asilimia 100 ikilinganishwa na bei ya kudumu ya serikali ya Tsh.1800. hali hii imesababisha wasiwasi kwa raia kutokana na gharama ya juu ya bidhaa hii huku sehemu nyinginezo za nchi bidhaa hii hata kukosekana.
Sisi, Hizb ut Tahrir Tanzania, tunaendelea kusema kinaga ubaga kuwa tatizo hili ni njama ya kimakusudi ambayo lengo lake kuu ni kuwalinda baadhi ya mabwenyenye wa kirasilimali ili wanawiri katika sekta ya sukari kwa jina la kulinda viwanda vya ndani vya sukari.
Vilevile, taarifa ya hivi karibuni ya serikali bungeni kutoka kwa Waziri Mkuu aliye thibitisha kuwa Tanzania ina upungufu wa sukari wa tani 100,000 katika matakwa yake ya tani 400,000, na kuahidi kuwa serikali itaagiza tani 100,000 ili kutatua upungufu huo kwani viwanda vya ndani vya sukari vimesitisha kuzalisha huku vikisubiri kuvunwa kwa mali ghafi ya miwa.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Vita-ya-sukari-sasa-kila-kona--wafanyabiashara-wakamatwa/-/1597578/3194804/-/vwohudz/-/index.html.#sthash.h9NEJVBT.dpuf
Taarifa hiyo imekosa haya na ni mwiba katika maisha ya raia. Kwa nini serikali ilisitisha uagizaji wa bidhaa hiyo ilhali kulikuweko na upungufu huo mkubwa? Ni udhaifu wa aina gani ambao viwanda hivi vinao, vimesitisha uzalishaji kutokana na kusubiri mavuno ya mali ghafi? Ikiwa serikali kweli ina ikhlasi katika kutatua upungufu huu, ni kwa nini haikufanya mapema?
Kadhia hii pia inaonyesha migongano ndani ya mfumo muovu wa kirasilimali ambao nchi yetu si sehemu yake. Mfumo huu unadai kutabanni sera ya 'soko huru' katika uchumi wake. Huku upande mwingine serikali ikiuchakachua kwa kuingilia kati kupitia kudhibiti bei, na kutowaruhusu wafanyi biashara kujihusisha katika uagizaji wa bidhaa fulani za chaguo lao, ikiwalazimu watumizi wa bidhaa kuganda katika bei zilizo wekwa na serikali juu ya bidhaa nk. Iko wapi hiyo sera ya biashara huru?
Ama vitendo vya serikali vya kuizuia shehena ya sukari ya baadhi ya wafanyi biashara kwa madai ya ufichaji wao wa bidhaa. Huo ni mpango mbaya wa serikali wa kuficha aibu ya kutotatua matatizo yaliyoko mkononi. Badala yake wanataka kutafuta umaarufu wa kisiasa na kuwahadaa raia wa kawaida ambao hawawezi kutathmini matukio. Tunauliza, ikiwa wafanyi biashara hao waliruhusiwa kuagiza bidhaa hizo; je yawezekana kuwepo na ufichaji wa bidhaa hizo ikiwa kweli kulikuwepo na kadhia kama hiyo?
Mfumo wa Kiislamu ni kinyume na mfumo wa kirasilimali, unashutumu vikali ufichaji wa bidhaa ili kusababisha upungufu usio wa kihakika. Wakati huo huo, unatoa mazingira mazuri ili kuzuia ufichaji bidhaa ikiwemo Dola kutoingiliakati katika uwekaji bei katika bidhaa zozote.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |