Jumanne, 14 Rajab 1446 | 2025/01/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  9 Shawwal 1444 Na: 1444/24
M.  Jumamosi, 29 Aprili 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Njama za Usekula Dhidi ya Watoto wetu na Wokovu wao uko Mikononi mwetu
(Imetafsiriwa)

Nchi za Magharibi za kikoloni hazikuacha kufuata siasa za kuutusi Umma wa Uislamu ili kuuzuia mwamko wake na uregeshaji wa dola yake na izza yake, zikisisitiza kuufanya ulipie gharama ya mapinduzi yake dhidi yake, hivyo zina shauku kubwa ya kuwafanya watoto wetu kukua chini ya mfumo uliosukwa na fikra za kihamasa, chafu, za kisekula kupitia udhibiti wake mkali juu ya vyombo vya habari na taasisi za elimu kwa jina la usasa unaodaiwa. Hii ni chini ya mwavuli wa kifiniko cha kisheria unaotokana na makubaliano potovu ya kimataifa.

Na mbele ya utamaduni unaoendelea wa mashambulizi ya kimfumo juu ya maadili ya Uislamu na nanga za kitambulisho katika nafsi za watoto na vijana wetu kupitia njia chafu za mawasiliano ambazo zimesawazishwa na uhalifu, uzinzi, kukiuka matukufu, na kushambulia mamlaka na sura ya mchungaji kama baba, mama na mwalimu...

Na kwa kuzingatia hali ya uchovu na mkanganyiko uliowakumba Waislamu nchini Tunisia kati ya kukimbilia maisha, kukata nyenzo msingi, na kuwanyima watoto elimu endelevu kwa kuzingatia mfumo wa elimu usio na miundombinu na unaotawaliwa na vurugu na misukosuko, ambapo mwalimu anadhalilishwa kimaadili na kimada mbele ya sera ya utaratibu wa kutojali ya dola ya kisasa inayofuata sera ya kutorokea mbele. Katika kutafuta tiba ya mgogoro ndani ya mfumo ambao ulikuwa ndio chanzo cha ugonjwa...

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia, tunatangaza, kwa baraka za Mwenyezi Mungu Mtukufu, uzinduzi wa kampeni chini ya kichwa: "Njama za Usekula Dhidi ya Watoto Wetu na Wokovu wao uko Mikononi mwetu."

Programu ya kampeni inajumuisha nukta mbili:

Nukta ya kwanza: Elimu ya kisekula ndiyo chanzo cha ugonjwa na chanzo cha kuporomoka kwa maadili nchini.

Nukta ya pili: Uislamu ni tiba kwa Ummah kwa jumla na hasa vizazi vichanga.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْراً لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” [Aali-Imran:110].

Msemaji wa Kike wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu