Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 12 Dhu al-Qi'dah 1444 | Na: 1444/25 |
M. Alhamisi, 01 Juni 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia Yawasilisha Barua ya Wazi kwa Waziri wa Sheria
(Imetafsiriwa)
Asubuhi ya Alhamisi, tarehe 01/06/2023, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, akiwemo Mkuu wa Afisi ya Kisiasa Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Yassin bin Yahya, na mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Mwanasheria Fathi Al-Khamiri, na mjumbe wa Afisi ya Habari Ustadh Ahmed Al-Tatar, walimkabidhi Waziri wa Sheria, Bi Leila Jaffal, barua ya wazi kuhusu kukithiri kwa kukamatwa mara kwa mara kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Tunisia.
Barua hiyo ilijumuisha ukumbusho wa mtazamo wa Hizb katika kazi ya kisiasa na uthibitisho kwamba ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu na kinafanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kupitia kutabanni mvutano wa kifikra na kisiasa na haitendi vitendo vyovyote vya kisilaha, bali inaharamisha kufanya vurugu au kutafuta msaada wa kigeni, kwa kuzingatia kwamba jambo hilo limeharamishwa na Sharia.
Barua hiyo pia ilijumuisha maregeleo ya kesi za dhulma ambazo Mashababu wa Hizb ut Tahrir walikabiliwa nazo chini ya utawala uliokuwepo, iwe kabla au baada ya mapinduzi, ikithibitisha kwamba suala hilo baada ya Julai 25 lilizidi kuwa hatari zaidi, lisilo la haki na la kiholela, kwa hali haikufungika tena na baadhi ya vitendo vya polisi badala yake wawakilishi wa Afisi ya Mashtaka ya Umma, licha ya hadhi yao ya kimahakama, walikuwa na dori hasi na mara nyingi walienda sambamba na vitendo hivi vya kubahatisha, ambapo baadhi ya waendesha mashtaka walipeleka ripoti za utafiti kwenye nguzo ya mahakama ya ugaidi, ambayo ilikuwa sehemu ya hatari ya mabadiliko ya sera ya adhabu ambayo inaegemea upande wa kuifunga na kuzingira shughuli ya Hizb ut Tahrir na kujaribu kuwatisha Mashababu wake, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kutiwa hatiani kwa Mkuu wa afisi ya eneo ya Hizb ut Tahrir katika eneo la Kelibia, Ustadh Adel Al-Ansari, kwa "kukiuka sheria ya dharura na kusambaza vipeperushi ambavyo vitavuruga amani ya utulivu wa umma." Mahakama ikakimbilia kutoa kifungo cha miaka miwili jela na utekelezwaji wa mara moja!
Kupitia risala hii, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia ilishutumu utiifu wa mahakama kwa amri zisizo za haki za kisiasa, kwa kuzingatia kwamba tabia hizi zinaakisi kufeli kwa mfumo wa mahakama katika nchi yetu na kupuuza kwake viwango vya chini vya uhuru na usawa, na kwamba mahakama inaweza tu kuwa huru na adilifu chini ya mfumo wa sheria za Kiislamu na ndani ya mfumo wa utawala ulioongoka kwa msingi wa Uislamu, ambao haujui upendeleo au kunyenyekea kwa dhalimu au dikteta, katika utabikishaji wa kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ للهِ شُهَدَاء بِالْقِسْطِ وَلاَ يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلاَّ تَعْدِلُواْ اعْدِلُواْ هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى وَاتَّقُواْ اللهَ إِنَّ اللهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ]
“Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Al-Ma’idah 5:8].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |