Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 24 Dhu al-Hijjah 1444 | Na: 1444/26 |
M. Jumatano, 12 Julai 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutokana na Kuongezeka kwa Mawimbi ya Wahamiaji Wasio wa Kawaida, Ufaransa imeigeuza Tunisia kuwa Nchi ya Kimbilio
(Imetafsiriwa)
Kwa mara ya tano mfululizo, Rais Kais Saied alitoa wito upya wa kufanya kongamano la kikanda ili kujadili suala la uhamiaji usio wa kawaida na kuanzisha mpango wa pamoja wa hatua za kutatua mgogoro huo. Amesisitiza kuwa, Tunisia haitakubali makaazi ya wahamiaji katika ardhi yake. Mwaliko wa kuitisha kongamano hili la kikanda, kwa kushirikisha nchi zinazohusika, ulifanywa kwa njia ya simu na Rais wa Ufaransa, kama ilivyoelezwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Afisi ya Rais wa Jamhuri mnamo 03/06/2023.
Hakika, Mshauri wa Rais wa Tunisia, Walid Al-Hajjam, alithibitisha wakati wa uingiliaji kati wake kwa Chaneli 9 mnamo 22/05/2023, kwamba mwaliko wa kongamano la kimataifa la uhamiaji usio wa kawaida ni wazo na mpango kamili wa Tunisia, unaotokana na mawazo ya Rais Kais Said.
Ingawa kuufanya mgogoro huo kuwa wa kimataifa si hatua ya kijanja inayostahili kusifiwa, wazo la kufanya kongamano kuhusu uhamiaji usio wa kawaida lilipendekezwa hapo awali na Chama cha Kuunga mkono Walio Wachache mnamo Machi 6, 2023. Hii inaonyesha kwamba wazo hili limekuwa likifichwa nyuma ya matukio kwa baadhi ya watu kwa muda, chini ya uangalizi wa duara za kikoloni, ili kuwasilishwa hadharani kama mpango kamili wa Tunisia.
Sambamba na maandalizi ya kongamano la kimataifa, ambao hapo awali lilipewa jina la mkutano wa pamoja na kisha kongamano la kikanda, Tunisia, Jumuiya ya Nchi ya Wakimbizi imeweka juhudi kubwa katika kuendeleza miradi kadhaa ya makaazi mapya ya Waafrika, kwa msaada wa ukarimu kutoka kwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), kwa mujibu wa taarifa za mkurugenzi wa chama mwenyewe. Inafaa kutaja kwamba chama hiki ni tawi la Tunisia la chama cha Ufaransa, Ardhi ya Kimbilio, ambayo inalenga kuvutia na kutumia uwezo wa bara la Afrika kwa manufaa yake yenyewe.
Kwa hivyo, ushahidi na viashiria vinaendelea kukusanyika siku baada ya siku, kuthibitisha kwa kila mtu kwamba mgogoro wa uhamiaji wa Afrika kupitia Tunisia ni mgogoro wa kupikwa, kama alivyokiri rais mwenyewe. Makaazi mapya ya Waafrika kutoka nchi za pwani, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Chad, na Sudan katika nchi hii inayosambaratika ni ajenda iliyolazimishwa kwa serikali dhaifu za kisiasa, kwa ushirikiano na wale waliofungua milango ya kuingia na kupita. Biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu iliyotajwa na rais ni sekta ya kibepari na bidhaa ya hali ya juu. Ni nani anaamini kwamba masuluhisho yatatoka kwa wapikaji wa migogoro na wanyonyaji wa utajiri wa Afrika na damu ya watu wake? Ni nani anaamini kwamba kujifungamanisha na mabaki ya ukoloni wa Ufaransa kutaleta ustawi kwa mataifa haya yanayokandamizwa? Na je, kuna njia adilifu zaidi kuliko kuregesha sheria za Mwenyezi Mungu au kuna mafungamano yenye nguvu zaidi kuliko mafungamano ya Al-Aqida?
Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia, tunathibitisha kwamba hakuna njia ya kutoka katika mtego wa kikatili wa ubepari na utumwa wake kwa watu, wala sera za kikoloni zinazolenga kugeuza vikosi vya usalama na jeshi kuwa walinzi na watumishi kwa manufaa ya Magharibi na ajenda zake. Nchi yetu inageuzwa kuwa sehemu ya kuchagua na kuchuja wale wanaovuka kuelekea Bara la Afrika. Hakuna njia ya kutoka katika hili isipokuwa kwa kuregesha mamlaka kamili ya Uislamu na kuifungua Tunisia kwenye mazingira yake ya kieneo na kuukumbatia Ummah wake. Ni Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu, unaostahiki kuwa umma bora kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Ni Khilafah Rashida iliyoahidiwa, Khilafah inayosimamia haki za raia wake na haiwadhulumu hata kidogo, wala kuwaacha jangwani wakiwa na njaa na kiu katika joto kali. Bali inawapa haki zao kamili, bila ya kupambanua kati ya mweusi na mweupe isipokuwa kwa Taqwa.
Ama kusafirisha matatizo yetu kwa wakoloni makafiri na kuwahusisha katika mambo yetu, hata katika usalama wetu, na kuyafunga kwa maneno matupu yasiyolisha wala kushibisha njaa, ni kujiua kisiasa wenyewe. Huu ni ushahidi zaidi wa ufisadi wa serikali iliyo katika hali kuporomoka isiyo na uwezo wa kushughulikia mambo ya watu wake na kuwapa mahitaji yao ya kimsingi, achilia mbali kuchunga mahitaji ya wanaokuja kwake. Bila shaka, ni ishara ya utepetevu kamili. Je, kuna mtu yeyote anayezingatia hili?!
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ]
“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” [Ar-Rum: 41].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |