Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  20 Safar 1442 Na: : 1442 / 02
M.  Jumatano, 07 Oktoba 2020

 Tanzia
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki Yamuomboleza Vedat Kurnaz,
Mmoja wa Mashababu Wake Wenye Ikhlasi!
(Imetafsiriwa)

مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا﴿

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Ahzab: 23]

Vedat Kurnaz alijitolea maisha yake kama Muislamu mwenye ikhlasi na mwaminifu aliyefanya kazi ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu, kisha akamaliza maisha yake ambayo aliyatumia kubeba ulinganizi wa Kiislamu na yeye pia akiwa ni mbebaji ulinganizi huu, ambapo alikufa katika masaa ya jioni kutokana na shambulizi la moyo (angina pectoris) alipokuwa akitoa halqa (duara la masomo) kwa Mashababu.

Marehemu Vedat Kurnaz alizaliwa mnamo 1966, yeye ni mhandisi wa umeme na vifaa vya kielektroniki, na alikuwa ni mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilayah ya Uturuki. Alianza kufanya kazi ya da'wah huko Vienna na kisha Uturuki. Alitumia maisha yake katika da'wah ya kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Na vile vile aliondoka kwenda katika rehema ya Mwenyezi Mungu (swt) ilhali anatoa halqa ya masomo ya kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu katika ardhi, na sisi tunashuhudia hilo mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt) ammiminie ndugu yetu mpendwa rehma yake na aipe ilham familia yake kwa subra njema, na tunatanguliza rambi rambi zetu kwa jamaa zake, wapendwa wake  na wenzake walio katika njiani kwake.

إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿

"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea." [Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu