Jumapili, 14 Rabi' al-thani 1442 | 2020/11/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ushuhuda wa Abdul Majeed Bhatti Kuhusu Naveed Butt

#MjueNaveedButt
#MwacheniHuruNaveedButt

Nilikutana na Naveed Butt kwa mara ya kwanza mnamo 2000, na mara moja nikatekwa na ukweli, ushujaa na mvuto wake. Naveed alibarikiwa na zawadi ya kipekee ya kuacha hisia isiyofutika kwa watu kuhusu kurudi kwa Khilafah nchini Pakistan.

Tulifanya kazi kwa karibu kuanzisha Hizb ut Tahrir nchini Pakistan. Alitumia masaa mengi kuandaa kwa bidii mikutano ya waandishi wa habari, na ziara za kibinafsi na watu maarufu. Angeweza kutarajia maswali na kutayarisha majibu kuhakikisha kuwa maelezo yalikuwa na ufasaha na hayakuwa ya kutoeleweka. Wakati wa ziara za kibinafsi, alikuwa akisikiliza kwa uangalifu na kuchukua muda wake kushughulikia vidokezo daima akijaribu kuhakikisha kuwa upande wa pili umeridhika vya kutosha na jibu.

Katika mikutano ya waandishi wa habari jijini Lahore, Islamabad, Karachi na Peshawar, Naveed angeonyesha msimamo huo huo na kila wakati alijitahidi kuwa na adabu lakini wakati huo huo alikuwa anaushawishi sana. Aliweka wazi ajenda ya chama na kwenda kwa undani juu ya njia ya amani ya chama. Kuhusu suala la Khilafah, kwa bidii alifuta madai mengi ya uongo yaliyosambazwa na vyombo vya habari vya Magharibi, na alikuwa mzuri sana katika kuichora Khilafah kama badali halisi na ya kivitendo kwa Demokrasia ya Kiliberali na Urasilimali.

Wakati wa vipindi vya maswali na majibu, tabia ya utulivu ya Naveed daima iliangaza. Akiwa na waandishi wa habari, alikuwa mwangalifu kuelezea hoja sahihi na akanyanyuka juu ya siasa za shakhsiya za watu. Aliposhirikisha hadhira, Naveed daima alikuwa akizingatia kuelezea utekelezwaji wa Khilafah uliofungamanishwa na shida za sasa zinazowakabiliwa Waislamu nchini Pakistan. Akiwa na maafisa wa serikali, haswa wale kutoka kwa vyombo vya ujasusi, Naveed alikuwa mpole kwao, lakini imara na asiyeyumba, akiwakumbusha jukumu lao la kusimamisha tena Khilafah Rashida na kwamba watahesabiwa na Mwenyezi Mungu Allah (swt) kesho Akhera kwa kupuuza jukumu hili.

Namuombea Naveed Butt kuachiliwa kwa haraka kwani Ummah unastahili umahiri wake wa kisiasa na uongozi. Yeye ni mtu mkubwa kati ya wale ambao wanatafuta kwa dhati kurudisha hukmu ya Mwenyezi Mungu kupitia kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa ajili ya Pakistan. Mwenyezi Mungu (swt) amsamehe na ampe fursa ya kuona juhudi zake zikizaa matunda katika mustakbali wa hivi karibu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Novemba 2020 22:27

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu