Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Wakati Sasa kwa Majeshi ya Waislamu Kuonyesha Misimamo Yao

Kashfa dhidi ya matukufu ya Uislamu imekuwa ni jambo la kuendelea kwa Makafiri kuonyesha ghadhabu na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wanatamani Uislamu umalizike kwa kuuvunjia hesima kwa kufuru, wakati kwa kweli Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi kuulinda Uislamu na matukufu yake licha ya chuki za makafiri dhidi ya Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapokuwa Makafiri watachukia.” [Surah Tawba: 32]

Kashfa za karibuni za Ufaransa na raisi wake Macron dhidi ya Mtume wetu mpendwa (saw) hazitopunguza hadhi ya Mtume wetu mpendwa (saw) katika dunia hii na Akhera kama Mwenyezi Mungu (swt), Bwana wa mbingu na ardhi, alivyomsifu na kumnyanyua kwenye hadhi ya juu, kama alivyosema,

[إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا]

“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlioamini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.” [TMQ Surah Al-Ahzab: 56].

Bali, huo ni mtihani tu kwa waumini kuonyesha misimamo yao, ima wako pamoja na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake au wako na Wamagharibi na mfumo wao. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[مَّا كَانَ اللَّهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ]

“Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema.” [TMQ Surah Al-Imran: 179].

Aya imeteremshwa kipindi cha Vita vya Uhud wakati wanafiki walipowaacha Waislamu na thuluthi moja ya jeshi, kuchukua msimamo dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa kuchagua kuwaangalia tu waumini wakipigana na maadui wa Kiqureshi. Imam Tabari amelitaja hili katika tafsiri yake ya aya kwa kusema,

﴿مَّا كَانَ ٱللَّهُ لِيَذَرَ ٱلْمُؤْمِنِينَ﴾ ما كان الله ليدع المؤمنين على ما أنتم عليه من التباس المؤمن منكم بالمنافق، فلا يعرف هذا من هذا ﴿حَتَّىٰ يَمِيزَ ٱلْخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيّبِ﴾ يعني بذلك: حتى يميز الخبيث، وهو المنافق المستسر للكفر، من الطيب، وهو المؤمن المخلص الصادق الإيمان بالمحن والاختبار، كما ميز بينهم يوم أُحد عند لقاء العدو عند خروجهم إليه

 Mwenyezi Mungu hatowaacha waumini katika [hali] hiyo [uliyoko sasa]” yaani, Mwenyezi Mungu hatowaacha waumini katika hali ambayo Wewe (Mtume wa Mwenyezi Mungu na maswahaba zako) kuwa katika hali ambapo waumini na wanafiki wamechanganyika kiasi cha kuwa hawajitengi. “Hadi awatenganishe waovu miongoni mwa wazuri”, hii ina maana: hadi awatofautishe waovu yaani wanafiki walioficha ukafiri wao kutokana na wazuri yaani waumini wakweli waaminifu kwa imani yao wakati wa majaribio na mitihani, kama wote walivyojitenga siku ya Uhud walipoondoka na kuacha kukutana na maadui zao”. Katika aya hii, Mwenyezi Mungu (swt) anatujuza kuwa atawatenganisha waumini kutokana na wanafiki kupitia mitihani na dhiki kama ilivyotokea wakati wa Vita vya Uhud.

Kutokana na haya, matusi dhidi ya Mtume wetu mpendwa (saw) ni mtihani kwa Waumini kujua msimamo wao waliouegemea. Hakutokuwa na msimamo wa kati na kati ambapo Muumini analaani matusi wakati huo huo anaukubali Usekula ambao ndio unaoshajiisha makafiri kumtusi Mtume wetu mpendwa (saw) kupitia uhuru wa maoni. Watawala wa Waislamu wamejiweka upande wa mabwana zao Wamagharibi na fikra zao kwa kuelezea tu lawama zao bila kufanya matendo yoyote stahiki kama kuwaita mabalozi, kukata mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia, kutuma majeshi yao dhidi ya wale wanaomtusi Mtume wetu mpendwa (saw). Waislamu wa kawaida wameonyesha mapenzi yao kwa Mtume (saw) kwa kuandamana dhidi ya Ufaransa na kususia bidhaa zao, kulingana na uwezo wao. Hivi sasa, ni muda kwa majeshi ya Waislamu kuonyesha misimamo yao, ima kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) au kujiweka upande wa makafiri katika hali ya udhalilifu. Hakuna nafasi ya kati na kati kwa jeshi la Waislamu kuonyesha mapenzi yao ya Mtume (saw) bila ya kumnusuru Yeye na Dini yake. Matendo ya sawa yanayostahiki kwa jeshi la Waislamu ni kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) kwa kutoa Nusra kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume na kusonga mbele dhidi ya wale wanaomdhuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Enyi majeshi ya Waislamu, hivi sasa ni zamu yenu kuonyesha upande wenu kwa kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuinusuru Dini Yake kama walivyokuwa ‘Hawariyun’ ambao wamemnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu, Issa (as) wakati alipowalingania dhidi ya makafiri.

 [فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَى مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّهِ آمَنَّا بِاللَّهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ]

“Issa alipohisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.” [Surah Aali-Imran: 52].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammad bin Faruuq

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu