Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ummah wa Kiislamu Sio Dhaifu Kusimamisha Khilafah

Mamia ya miaka imepita tokea kuvunjwa kwa ngao ya Ummah, Khilafah. Tokea muda huo, makafiri wakoloni wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kuzuia kurudi tena kwa Khilafah. Walipoiangusha Khilafah, walitamani Khilafah isirejee tena, kama Curzon, aliyekuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza aliyewahi kusema katika Bunge la Wananchi “Hali sasa ni kuwa Uturuki imeshavunjwa na haitoinuka tena, kwa sababu tumevunja nguvu yake ya kiroho: Khilafah na Uislamu”. Kinyume na matamanio yao, wakoloni makafiri imewalazimu kufanya kazi bila kuchoka hadi leo kuzuia kurudi kwa Khilafah. Wakati walipoiangusha Khilafah, waliona wamefaulu katika kuuengua Uislamu kutokana na masuala ya Waislamu kwa kuwapandikiza watawala vibaraka wao katika ardhi za Waislamu. Waliona wamefaulu walipokomesha na kuigeuza miito na hamasa miongoni mwa Ummah wakiwemo Maulamaa wakati wa kuvunjwa kwa Khilafah.

Majaribio yote ya mwanzo yaliyotekelezwa na Ummah kuipata tena Khilafah iliyowatoka yalitoweka kwa haraka. Makongamano ya kimataifa ya Khilafah (makongamano ya Kiislamu nchini Misri, Makkah 1926, Jerusalem 1931) hayakuzaa matunda kwa Ummah, isipokuwa kusisitiza kwake tu juu ya wajibu wa kusimamisha Khilafah. Kwa upande mmoja, dhana mpya ya kigeni ya dola za kitaifa iliingizwa ndani ya Ummah. Huku kwa upande mwengine, shauku na hamasa iliibuka miongoni mwa Ummah uliogawanyika zilitulizwa na umoja bandia chini ya bendera ya makongamano ya Kiislamu na ushirikiano (kama: Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu). Umbile la Kiyahudi limepandikizwa ndani ya moyo wa ardhi za Waislamu ili kuzuia moja kwa moja kuja pamoja  kwa mataifa ya Kiislamu kwa  kupoteza nguvu zao kutokana na vita na mivutano ya kuendelea. Viongozi wa bandia wa Kiislamu kama Gamal Abdul Nasser, Erdogan na wengineo walitambulishwa ili kuipotosha njia ya Ummah ya Uislamu. Licha ya jitihada zao zote za kuupindisha Ummah kutokana na wito wa Khilafah, wito huo umeukumba Ummah kama upepo mwanana na dhoruba kali. Hivyo makafiri wakoloni wamechukua hatua kwa ukali kusitisha kuinuka kwa Ummah kwa miradi kama ya vita dhidi ya ugaidi, mipango ya kuondosha siasa kali na mengineyo. Uislamu ambao hata hautekelezwi kivitendo umekuwa ni kitisho kikubwa kwa Wamagharibi, ikiongezea kuongezeka kwa kitisho chenye kuonekana kama Umoja wa Kisovieti, ikifuatiwa na Uchina. Kitisho kwa usekula wa kimagharibi sio tu Uislamu wa kisiasa bali ni Uislamu wenyewe, ambao umeipelekea Ufaransa kuweka vizuizi juu ya matendo ya kidini kwa Waislamu wa Ufaransa na ulioipelekea China kuwaweka Waislamu wa Uighur kwenye kambi za mateso hadi waachane na Uislamu. Juhudi zote hizo zinazoendelea za makafiri hazikuweza kuung'oa Uislamu na Waislamu, japokuwa Uislamu hauna dola hivi sasa inayoutekeleza.

Enyi Waislamu! Mnaweza kushangazwa na nguvu kubwa za kijeshi za Wamagharibi hasa Amerika na kufikiri kuwa Waislamu ni dhaifu kuweza kusimamisha tena Khilafah, dhidi ya nguvu zao za kijeshi. Inaweza kuwahofisha Waislamu wanapoona ndege za jeshi la Amerika za Lockheed Martin Fighter zikiranda juu ya anga la ardhi zao. Inaweza kuwahofisha Waislamu wakati meli zao za kubebea ndege za Makuffar zikiwa katika zikiranda randa kwenye bahari za Waislamu. Enyi Waislamu! Licha ya maendeleo ya kiteknolojia katika uwezo wao wa Kijeshi, hawangeweza kuzimiliki ardhi zenu bila ya msaada wa watawala Waislamu vibaraka. Ndege zao zenye uwezo mkubwa zinahitaji kambi katika maeneo jirani kwa mapambano, ambapo haiwezekana bila ya watawala vibaraka wao. Meli zao kubwa za kubebea ndege zinahitaji ruhusa kuingia kwenye bahari zenu, ambazo zinaachwa wazi na watawala vibaraka. Wamagharibi hawawezi kupigana ardhini na kukushindeni. Kushindwa kijeshi kwa Amerika nchini Afghanistan katika vita virefu dhidi ya Taliban ni ushahidi wa wazi kwa hili.

Enyi Waislamu! Mnaweza kushangazwa na udhibiti wa kiuchumi wa wamagharibi na kufikiri kuwa Waislamu ni dhaifu kuirejesha tena Khilafah. Mtu anaweza kufikiri matokeo ya vikwazo vya kiuchumi vya wamagharibi dhidi ya Khilafah ijayo. Enyi Waislamu! Licha ya udhibiti wa kiuchumi duniani kote kupitia taasisi, dolari za mauzo ya mafuta na nyenginezo, ni rasilimali za ardhi za Waislamu ndizo zinazowaendesha. Nyingi ya njia za biashara na maeneo nyeti yapo katika ardhi za Waislamu. Bila ya msaada wa watawala vibaraka wa maeneo hayo, wamagharibi hawangeweza kuzitumia njia hizo na maeneo hayo. Hivyo basi, waathirika halisi wakubwa kwa Khilafah inayokuja ni Wamagharibi, mbali na migogoro ya sasa ya kiuchumi inayowashtua watu wao wenyewe.

Zaidi ya yote, Waislamu wana Imani, Aqida na mfumo ambao hauwezi kulinganishwa na wa Wamagharibi. Hivi leo, Magharibi imekuwa na mfumo usio na ushindani. Lakini bado imekuwa ni dola dhaifu (sick man) ya ulimwengu kutokana na kushindwa kutatua migogoro inayozuka mmoja baada ya mwengine. Kinyume chake, Waislamu wana mfumo usio na dosari kutoka kwa Muumba uliotawala ulimwengu kwa zaidi ya karne kumi na tatu bila ya tofauti. Waislamu watakaposimamisha dola yao, iliojengwa kwa msingi wa uongozi wa Wahyi ili kuuongoza ulimwengu, hadhara ya kimagharibi haitoweza kuhimili mapambano yake na dola ya Kiislamu.

Enyi Ummah wa Kiislamu! Nyinyi sio dhaifu wala dhalili hadi muwache Imani yenu ambayo Wamagharibi wameshindwa kwa mamia ya miaka baada ya kuivunja dola yenu, Khilafah. Enyi Waislamu! Nyinyi mna Imani yenu ilio na nguvu na hivyo mtakuwa wa juu zaidi, hata kama itachelewa kwa muda. Enyi Waislamu! Simamisheni Khilafah kwa nguvu zenu na Imani ili mtekeleze uadilifu wa Uislamu na kuubeba ulimwenguni.

(وَلَا تَهِنُوْا وَلَا تَحْزَنُوْا وَاَنْتُمُ الْاَعْلَوْنَ اِنْ كُنْتُمْ مُّؤْمِنِيْنَ‏)

“Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.” [TMQ 3:139]

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammad bin Faruuq

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu