Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itakabiliana na Ufisadi wa Kisiasa
(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَلَوْ اتَّبَعَ الْحَقُّ أَهْوَاءَهُمْ لَفَسَدَتْ السَّمَوَاتُ وَالأَرْضُ وَمَنْ فِيهِنَّ بَلْ أَتَيْنَاهُمْ بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَنْ ذِكْرِهِمْ مُعْرِضُونَ)

“Lau Haki ungalifuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga na ukumbusho wao.” [Al-Mu'minun: 71]

Hivyo basi, endapo Mwenyezi Mungu atafanya yale ambayo washirikina hawa wanayataka na kusimamia mambo kwa mujibu wa matakwa na matamanio yao na kuachana na haki wanayoichukia, mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake vingefisidika; hii ni kwa sababu hawajui matokeo ya vitu na wema na ufisadi wa usimamizi (tafsiri ya Tabari). Hali ya maisha haya sio sahihi, kutengea kwake kunawezekana pekee kupitia zile hukumu na tiba ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amezipitisha ambazo ameziteremsha kwa watu kama uongofu na rehema.   

- Uislamu ni itikadi ambayo kwayo huchipuza nidhamu inayo waongoza watu katika njia za kheri na mafanikio. Ulikuja kusahihisha ulimwengu na kutawala ulimwengu, na endapo utakosekana maishani mwao, ufisadi utatawala na watu watapotea. Ufisadi humaanisha kukengeuka kutokana na njia ya sawa, kuonyesha uasi kwa Mwenyezi Mungu (swt) juu ardhi na kutojisalimisha kwa Uungu wake (swt):

 (إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ وَمَا مِنْ إِلَهٍ إِلَّا اللَّهُ وَإِنَّ اللَّهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ * فَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ)

“Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Na hakika, Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Na kama wakigeuka basi Mwenyezi Mungu anawajua waharibifu.” [Al-i-Imran: 62-63].

- Kile ambacho Mwenyezi Mungu anakichukulia kuwa ufisadi basi ni hivyo, hata kama baadhi ya watu watakiona vyenginevyo. Mwenyezi Mungu (swt) asema: 

 (وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ)

“Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” [Al-Baqarah: 205]

Kwa hivyo, kuhukumu kitendo kuwa chema au fisidifu, ni lazima tuwe na kipimo. Kipimo hiki ni lazima kiwe cha Kisheria na sio cha kiakili; kwani endapo kitakuwa cha kiakili, kila mtu atadai kuwa kile anachokifanya ni wema na ilhali ni ufisadi, kama walivyo sema watu wa Firauni:

(أَتَذَرُ مُوسَى وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَك)

“Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? ...” [Al-A’raf: 127].

Wahemishwa miongoni mwa watu wa Firauni walimuhukumu Musa na watu wake kuwa wafisadi na kutoa hoja kuwa Firauni ndiye mtengezaji … Hukumu hii imejengwa juu ya matamanio na maslahi, ambazo hutoa hukumu ya kimakosa na fisidifu.

Kuiachia akili kuhukumu vitendo kwa wema au ufisadi hakutapelekea katika natija sahihi au hukumu sahihi. Sheria iliyotungwa na akili hukisifu kila kilicho nje ya upeo wake au hukiita chengine kisicho kuwa hicho kuwa fisidifu na chenye kufisidi: hivyo basi, Mrasilimali kwa mujibu wa wakomunisti ni mfisadi na Muislamu kwa mujibu wa warasilimali ni mfisadi … kwa msingi wa fahamu zinazo chipuza kutokana na imani hizi na hutofautiana kwa mujibu wa mfumo. 

 (وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَكِنْ لَا يَشْعُرُونَ)

“Na wanapoambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Hakika sisi ni watengenezaji. Tambueni! Hakika wao ndio waharibifu lakini hawatambui.”  [Al-Baqarah: 11-12]

- Ufusadi wa kisiasa (ufisadi katika uchungaji wa mambo ya watu) kwa ujumla ni ufisadi wa nidhamu inayo endesha mambo ya kimaisha ambayo hayawezi kuwa sawa isipokuwa yatawaliwe kupitia nidhamu ya Muumba wake:

 (وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ)

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.’”

[Ta-Ha: 124]

Ufisadi ni kuachana na sheria ya Mwenyezi Mungu na kutabanni sheria nyengineyo isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, Mtume (saw) alikuwa makini kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu duniani, ili yeye (saw) aeneze ujumbe huu, atekeleze amana na kuweka misingi ya dola inayo linda kheri na kupigana na maadui wake na kusimama wima kwa ajili ya kudumu kwake kupitia kuhasibu na kuzuia kila ufisadi ndani na nje ya Dola hiyo.  

Hivyo basi, vipi dola ya Khilafah itapiga vita ufisadi na watu wake?

- Kupitia Jihad, Khilafah imeeneza sheria ya Mwenyezi Mungu … na kupitia Jihad, kheri na wema zilitawala … na kupitia kwayo, watu walitolewa kutoka katika giza hadi katika nuru na iliwalingania kumuabudu Mola wa watu na kuachana na kila aina ya ufisadi uliokuwa nyuma yake … Haikulazimisha watu kuingia katika Uislamu, bali ilifanya kazi kuufanya ulimwengu usitawaliwe kwa chengine chochote isipokuwa kheri hii na kuwatabikishia watu sheria zake na uadilifu na rehema zilizomo ndani yake! 

Katika upande wa nje, Dola ya Khilafah imeeneza Kheri (Uislamu) kote duniani, hivyo basi eneo lake limepanuka … na ilizuia ufisadi (sheria zilizotungwa na binadamu) hivyo, kuzidunisha na kufanya kazi kuziondoa. Huku kindani, Khilafah ikipigana na ufisadi na wafisadi, na kuzuia udhalimu na madhalimu, na haikumruhusu yeyote kuwatawala Waislamu isipokuwa achaguliwe na Ummah, hivyo, mamlaka yako kwa Ummah na ni Ummah pekee ndio wenye haki ya kumteua yule wanayemuona kustahiki ili kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu.  

Hakuna yeyote anaye lazimishwa kuwa Khalifah kwa Ummah na hairuhusiwi kumlazimisha yeyote kumchagua nani atakaye kuwa Khalifah, hii ni kwa sababu “Khilafah ni mkataba wa khiyari na maridhiano” (Kifungu cha 25 cha Katiba Kielelezo ya Dola ya Khilafah iliyo tayarishwa na Hizb ut Tahrir).

Kila Muislamu ana haki ya kumchagua Khalifah na kumpa ahadi ya utiifu (Bay’ah). Mkataba wa Khilafah hufungwa kwa mtu kupitia bay’ah ya uteuzi ya wale waliochaguliwa na Ummah ili kuuwakilisha katika utoaji bay’ah hiyo ya uteuzi, huku bay’ah ya waliosalia katika watu ikiwa ni bay’ah ya utiifu na sio bay’ah ya uteuzi “yeyote anaye onekana kuwa na uwezo wa kuasi hulazimishwa kutoa bay’ah hiyo” (Kifungu cha 27 cha Katiba Kielelezo).  

- Endapo mtu atachukua Khilafah pasi na utiifu wa Ummah basi huyo atakuwa amenyakua haki yake na mamlaka na ameingia hatua ya kwanza katika njia ya ufisadi, na Ummah lazima wasimame dhidi yake, kumzuia na kuyaregesha mamlaka na kumchagua yule wanayemuona kustahiki mamlaka hayo, “Hakuna yeyote atakaye kuwa Khalifah isipokuwa ateuliwe na Waislamu, na hakuna yeyote atakaye miliki mamlaka ya lazima ya uongozi wa Dola hiyo isipokuwa baada ya mkataba naye kukamilishwa kwa mujibu wa Shari’ah, kama ulivyo mkataba wowote katika Uislamu.” (Kifungu cha 28 cha Katika Kielelezo).     

- Kumhisabu Khalifah ni jukumu juu ya Ummah; “Waislamu kuwahisabu watawala ni moja ya haki zao na wajibu toshelezi juu yao. 

Raia wasiokuwa Waislamu wana haki ya kutoa malalamishi yao kuhusiana na dhuluma ya mtawala kwao au utabikishaji wa kimakosa wa hukumu za Kiislamu juu yao.” (Kifungu cha 20 cha Katiba Kielelezo ya Dola ya Khilafah iliyo tayarishwa na Hizb ut Tahrir). Mtume (saw) asema:

«أَلاَ مَنْ ظَلَمَ مُعَاهِداً، أَوْ انْتَقَصَهُ، أَوْ كَلَّفَهُ فَوْقَ طَاقَتِهِ، أَوْ أَخَذَ مِنْهُ شَيْئاً بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسٍ، فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»

“Tambueni, yeyote mwenye kumdhulumu aliye hifadhiwa kwa mkataba, au akamkalifisha juu ya uwezo wake, au akampokonya kitu pasi na ridhaa yake, basi mimi nitakuwa mtetezi wake Siku ya Kiyama.” (Imesimuliwa na Abu Dawood). Hivyo basi, utabikishaji mbaya wa hukmu za Shari’ah huchukuliwa ni kitendo cha dhuluma, na kulalamika juu yake ni haki kwa Muislamu na Dhimmi, kwani Mtume (saw) amesema:

«وَإِنِّي لأَرْجُو أَنْ أَلْقَى رَبِّي وَلَيْسَ أَحَدٌ مِنْكُمْ يَطْلُبُنِي بِمَظْلِمَةٍ» “Na hakika mimi nataraji kukutana na Mola wangu na hali hakuna hata mmoja miongoni mwenu atakaye dai kutoka kwangu niliyomdhulumu.” (imeripotiwa na Al-Tirmidhi aliye sema riwaya hii ni Hasan Sahih).

«...مَنْ أَخَذْتُ لَهُ مَالاً فَهَذَا مَالِي فَلْيَأْخُذْ مِنْهُ، وَمَنْ جَلَدْتُ لَهُ ظَهْراً فَهَذَا ظَهْرِي فَلْيَقْتَصَّ مِنْهُ»

“... Yeyote niliyechukua mali yake, basi hii hapa mali yangu; na achukue kutoka kwayo, na yeyote niliyemchapa mjeledi mgongo wake, basi huu hapa mgongo wangu; basi na auchape mjeledi.” Hivyo basi, ili kupata utawala wa Mwenyezi Mungu na uadilifu duniani ni wajibu kwa Ummah – baada ya kutoa utiifu wake kwa Khalifah waliyemridhia kuwatawala kwa yale yote yaliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu– kumhisabu na kupeleka mambo yake Mahakama ya Madhalim (kupitia Baraza la Ummah) endapo atakataa kujiepusha kutokana na ufisadi wake na mahakama hiyo ina haki ya kumuuzulu.

- Rafiki na Swahaba wa Mtume (saw), Abu Bakr al-Siddiq alisema pindi alipochukua Khilafah kwa Waislamu:

إن أحسنت فأعينوني، وإن أسأت فقوّموني، الصّدق أمانة، والكذب خيانة، والضّعيف فيكم قويّ عندي حتّى أريح عليه حقّه إن شاء الله، والقوىّ فيكم ضعيف حتّى آخذ الحقّ منه إن شاء الله

“Nimetawalishwa juu yenu, ilhali mimi si katika wabora wenu. Nikifanya mazuri, nisaidieni; na nikikosea, ninyoosheni. Ukweli ni amana na urongo ni khiyana. Mnyonge kwenu kwangu mimi ni mwenye nguvu mpaka nimrudishie haki yake kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na mwenye nguvu kwenu kwangu ni mnyonge mpaka niichukue haki kutoka kwake kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.”

Hivyo basi, swahaba huyu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliuelewa ujumbe huu na kwa uongofu wa Mtume wake (saw), alitekeleza amana, na kuomba ushauri wa watu na usaidizi, na kwa njia yake hii Maswahaba na Tab’ieen waliifuata, hivyo walitawala na kunyanyua uadilifu na kueneza rehema na uongofu wa Mwenyezi Mungu. 

- Ujumbe wa Uislamu ni Ahkam za kiShari'ah zinazotekelezwa ardhini kwa ajili ya furaha ya wanadamu, na maagizo haya hutekelezwa kwa kupatikana Khalifah. Uwepo wake ni wajib ili kupata wema, na endapo atakosekana, ufisadi hutawala … Lakini Khalifah huyu au wengineo walio na jukumu la kutabikisha Hukumu wanaweza kufanya makosa – kwa kuwa wao ni binadamu – hivyo Uislamu umeweka vidhibiti ili kutotoa mwanya kwa dhuluma na kuenea kwa ufisadi … Katika Seera ya Mtume wetu kipenzi chetu kuna mafunzo bora, kwani yeye alijifunga na sheria ya Mola wake na hakukengeuka kutokana nayo … Alisimamisha adhabu za kisheria (Hudud), pasi na kulegeza msimamo au kubagua raia wake … Aliapa kwa Allah akisema:   

«وَايْمُ اللَّهِ لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا» “Naapa kwa Mwenyezi Mungu lau Fatimah binti Muhammad ataiba nitaukata mkono wake.”

Ikidhihirisha fikra safi na wazi ambayo yeye (saw) aliifuata na kwa hivyo akaongoka na kwayo akawaongoza wale waliomuamini Mwenyezi Mungu kama Mola wao na Muhammad kama Nabii na Mtume wao. Maswahaba na Tabi’een walimfuata katika hilo na wakafuata njia yake. Hivyo basi, Umar (r.a) alitekeleza adhabu ya kisheria ya unywaji (vilevi) juu ya mtoto wake kwa sababu alijua kuwa alikunywa aina fulani ya kinywaji ambacho kinalewesha.

- Omar bin al-Khattab (ra) amesema:

أرأيتم إن استعملت عليكم خير ما أعلم ثم أمرته بالعدل فيكم، أكنت قضيت ما علي؟ قالوا: نعم، قال: لا، حتى أنظر في عمله أعَمِل بما أمرته أم لا

“Mwaonaje lau nitamteua juu yenu mbora kati ya wale ninaowajua kisha nikamwamrisha kuwa mwadilifu kwenu, je, nitakuwa nimetimiza yale yaliyo juu yangu?” Wakasema: ndio. Akasema: “Hapana, hadi niangalie katika matendo yake – je, ametenda kwa yale niliyo mwamrisha au la.” Ingawa uangalizi wa Muislamu binafsi unaanza kwa kujitazama binafsi kunakotekelezwa na Muislamu mwenyewe, licha ya hivyo mwanadamu, ni mkosefu na ni watu wachache wanaoweza kukaa mbali na mtelezo huu.

Hivyo basi, matendo ya mtu yanahitaji kuangaliwa, na Mwenyezi Mungu amelifanya jukumu la uangalizi kuwa jukumu jumla la dola na jamii nzima ya Waislamu. “Ni wajib kwa Khilafah kuchunguza vitendo vya wasaidizi waliowekwa (Tafwidh) na usimamizi wao wa mambo, ili kuthibitisha kile kilicho sahihi, na kurekebisha makosa yoyote, kwani usimamizi wa mambo ya Ummah umewakilishiwa Khalifah na huamuliwa kupitia ijtihad yake” (Kifungu cha 46 cha Kielelezo cha Katiba ya Dola ya Khilafah). “Khalifah ni lazima achunguze vitendo vya magavana na kutathmini kwa kuendelea utendakazi wao kwa umakinifu. Ni lazima awape niaba watu kuangalia hali zao, kuwachunguza, na mara kwa mara kuwakusanya wote au baadhi yao, na kusikiza malalamishi ya raia kuwahusu” (Kifungu cha 60 cha Kielelezo cha Katiba ya Dola ya Khilafah). Watangulizi (Salaf) wa Ummah walifuata mwelekeo huu ili kung’oa ufisadi kutoka katika jamii ya Kiislamu na kuondoa alama zake.    

Hivyo basi, tatizo sio uwepo wa watu wafisadi ndani ya dola, bali tatizo ni kujitia upofu juu ya ufisadi na kutowaadhibu wafisadi, wanaofisidi. Kuna mwanya mkubwa kati ya mtawala mwadilifu anayepigana na ufisadi na kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) kumpa mafanikio ili kutabikisha hukumu zake, na mtawala mfisadi anaye kwepa na kuasi, bali, anapiga mahesabu pamoja na watu wafisadi na kuamiliana nao, na hivyo basi kumkhini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini, na atapokea kutoka Mwenyezi Mungu kile anachostahiki.  

- Katika “utawala wa kidemokrasia” watu wafisadi huhalalisha ufisadi wao, na ndani ya demokrasia hupitisha kanuni zinazotumikia maslahi yao na kuidhinisha maovu yao. Ili kupata hili, tunawaona wakitilia nguvu kampeni zao za uchaguzi, wakiwasiliana na watu na kutumia pesa ili kuhakikisha idadi ya juu zaidi ya kura, na baadaye, baada ya kuwatawala kwa “demokrasia” yao wanageuka na kukusanya viwango vikubwa vya pesa ili kufidia zile walizotumia maradufu. Huku tukiona kuwa chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu amana hii haipewi wale wanaoitafuta, kwa hofu kuwa huenda akapotoka na kudanganywa kuhusu Mwenyezi Mungu na mdanganyaji, na hivyo kupotea, kuwa mfisadi na kutenda ufisadi. Mtume (saw) amesema: 

«إِنَّا وَاللَّهِ لا نُوَلِّي عَلَى هَذَا الْعَمَلِ أَحَدًا سَأَلَهُ، وَلا أَحَدًا حَرَصَ عَلَيْهِ»

“Hakika sisi kwa Jina la Mwenyezi Mungu hatumteui yeyote kwa kazi hii anaye itafuta, wala yeyote anayeigombania.”

Yeyote anayetafuta wadhifa wa Khilafah na kuuomba na kuugombania anautafuta kwa ajili ya nafsi yake, na ana matarajio na manufaa ya kibinafsi, na yeyote aliye hivyo kamwe hata tafuta maslahi ya wengine na hatakuwa na hamu ya kuwanufaisha. Hivyo, Abu Dharr alipouomba, na yeye ni mwema na mwaminifu, akisema:    

 يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَا تَسْتَعْمِلُنِي؟

قَالَ:

«فَضَرَبَ بِيَدِهِ عَلَى مَنْكِبِي ثُمَّ قَالَ: يَا أَبَا ذَرٍّ إِنَّكَ ضَعِيفٌ وَإِنَّهَا أَمَانَةُ وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ إِلَّا مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا»

“Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mbona usiniteue (kwa wadhifa rasmi)? Akanipiga kwa mkono wake juu ya bega langu kisha akasema: “Ewe Abu Dharr hakika wewe ni dhaifu na hakika hii ni amana na hakika hii itakuwa ndio sababu ya fedheha na majuto siku ya Kiyama isipokuwa kwa atakayeibeba kwa haki yake na kutimiza yale aliyoteuliwa kwayo (kutekeleza majukumu yake ipaswavyo)”

Ufisadi wa kisiasa ambao umeukumbuka Ummah wa Kiislamu na ulimwengu kwa jumla chini ya demokrasia hii iliyooza, pamoja na sheria zake dhalimu, hauwezi kumalizwa na hauwezi kuondolewa isipokuwa kwa kupitia nidhamu ya utawala ya Kiislamu, “Khilafah kwa njia ya Utume”. Ndiyo pekee itakayo pambana na ufisadi, kwa sababu sheria zake huidhinishwa kwa mujibu wa maagizo ya Mwenyezi Mungu (swt), sio kwa mujibu wa matamanio na mapendeleo ya watawala wanaochimba mahandaki baina yao na Ummah, ambao hawaaminiwi kwa Dini ya Mwenyezi Mungu wala kwa maisha ya watu, na ambao wananufaishwa na makafiri katika kueneza ufisadi na kuuzuia Ummah kutokana na kushikamana na Uislamu na kutabanni hukumu zake na kuishi chini yake.  

Ili kuondoa ufisadi … na kuwaregeshea watu usalama, utulivu na ufanisi … ni wajibu kwa Waislamu kujiunga na kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu na kuishi chini ya hukumu adilifu za Mola wao, na kufanya bidii ili kuondoa demokrasia na ufisadi wake na mateso ya wanadamu hadi ahadi ya Mwenyezi Mungu ipatikane:

 (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آَمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kutenda mema atawafanya makhalifah katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifah wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao, Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55].

Na bishara ya Mtume (saw) isimame:

«...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“... kisha utakuwepo utawala wa mabavu, na utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha (saw) akanyamaza”. (Imesimuliwa na Ahmad).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zainah As-Saamit

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu