Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni Khilafah Pekee Ndiyo Iwezayo Kuchukua Nafasi ya Mpango wa Uchumi wa Amerika Unaosambaratika

(Imetafsiriwa)

Katika usikilizwaji wa Kamati ya Seneti ya Benki wa tarehe 28 Septemba 2021, Waziri wa Fedha, Janet L. Yellen, aliwaonya watunga sheria wa Amerika mnamo Septemba 28 juu ya matokeo ya “msiba mkuu”, pindi Bunge la Marekani likishindwa kuongeza au kusitisha ukomo wa kisheria wa deni hadi Oktoba 18, 2021, akisema, kuchelewa kutapelekea mporomoko wa kujiumiza wenyewe wa kiuchumi na mgogoro wa kifedha. Baadaye mnamo Oktoba 3, 2021, Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari Wachunguzi (ICIJ), ulianza kuchapisha “Karatasi za Pandora” zikiweka wazi ukwepaji kodi na ufisadi. Kisha, katika tamko la Oktoba 4, Afisa Mkuu na Msemaji wa ikulu ya White House, Jen Psaki, alirudia tena kauli ya Rais Joe Biden ya kujifunga kwake “kupambana na ufisadi kuwa ni maslahi muhimu zaidi ya usalama ya taifa.” Psaki pia alikariri ahadi ya Biden “kufanya kazi pamoja na wadau na washirika kuzungumzia masuala kama matumizi mabaya ya makampuni ya shell na ulanguzi wa pesa…”

Usakaji huo wa fedha za kodi zilizofichwa umefanyika kabla na utaendelea kufanyika mbeleni, lakini kasoro za asili katika mfumo wa kirasilimali zitabakia. Pamoja na udhaifu wa ukusanyaji kodi na malipo makubwa ya riba, deni la Amerika limeendelea kupanda katika viwango visivyo vya kawaida, katika namna inayohatarisha hali ya baadaye ya Amerika kuwa dola kuu isiyopingwa. Kwa muda sasa, Amerika imekuwa ikitafuta hifadhi kubwa za mitaji kote duniani, kwa lengo la kudai au kutoza kodi, ili kuzuia kufilisika kwa serikali ya Amerika. Mwanzoni ilivunja ngome ya usiri wa benki za Uswizi, ikizitaka kufichua mafaili yao ya raia wa Amerika kwa serikali ya Amerika. Mashirika makubwa ya Amerika yameendelea kuficha mamia ya mabilioni ya dolari katika mafichio ya kodi, ikiepuka Mfumo wa Akiba ya Serikali ulioshikwa na hofu.

Zaidi ya hayo, mfumo wa sasa wa uchumi unahakikisha kuwa pindi Amerika inapochemua basi dunia yote inashikwa na mafua. Kutokana na mamlaka ya dolari kwa biashara ya kimataifa, mgogoro wa deni la Amerika unahatarisha uchumi wa ulimwengu. Wakati kuchapisha dolari zaidi hutoa afueni kwa deni la ndani la Amerika, kushuka thamani kwa dolari humaanisha dunia yote hulipia deni la Amerika. Huongeza gharama za deni kwa nchi nyengine, kupunguza mapato yao kwenye bidhaa wanazouza nje na kuongeza bei ya bidhaa zinagoagiza.

Mawindo ya Amerika ya kukusanya fedha huenda yakaruhusu mfumo wake wa riba kuendelea kuchechemea kwa muda, hadi wakati wa mgogoro mwengine, huku wengine duniani wakilipia deni linaloendelea kukua la Amerika. Hata hivyo, huo sio utatuzi wa matatizo ya asili. Ni sawa kabisa, dunia haina matumaini kwa Amerika kuwa na afueni kutokana na mashaka ya kiuchumi. Kwa hakika, hakuna tamaa kwa nchi yoyote katika mataifa makubwa yaliyopo kwa kuwa yote yamejifunga na mfumo ule ule kama Amerika. Ni Ummah wa Kiislamu pekee ndio uwezao kuleta utulivu duniani, kupitia Dini tukufu, Uislamu, kama unavyotabikishwa na dola ya Khilafah.

Khilafah kwa njia ya Utume itakomesha umiliki wa dolari kwa kutoa sarafu inayoegemea juu ya fedha na dhahabu, huku ikisisitiza juu ya kuwa dhahabu na fedha kuwa msingi wa biashara ya kimataifa. Khilafah itapiga marufuku uovu wa riba ambao umezalisha kimelea cha mfumo wa kifedha kinachochuruzisha damu ya biashara halisi na kukausha uzalishaji. Khilafah pekee ndio itayoziunganisha Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati na maeneo mengine ya Ulimwengu wa Kiislamu kumakinisha nishati iliojaa na rasilimali za madini, pamoja na njia kuu za kibiashara za dunia, kuiwezesha kuuchanachana muundo wa kiuchumi wa Kimagharibi. Ili kuyaanzisha hayo yote, hivi sasa imebakia kwa Ummah wa Kiislamu kusisitiza vijana wake katika watu wanaomiliki nguvu kuipatia Hizb ut Tahrir Nussrah yao kwa ajili ya kuirejesha Khilafah na ubwana wa Uislamu kwa ulimwengu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu