Jumatatu, 11 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mabadiliko Yanawajibisha Utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), Kuhukumu kwa Yale Yote Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) kupitia Khilafah

(Imetafsiriwa)

Quran tukufu inaelezea habari za mataifa tafauti na sababu za kushindwa kwao. Kuna sababu moja tu, nayo ni kuwa, hawakumtii Mwenyezi Mungu (swt). Ima wawe ni watu wa Nuh (as), watu wa Lut (as), Aad au Thamud, ambapo suala la kutomtii Mwenyezi Mungu (swt) kwao lilitafautiana. Hata hivyo, suala la kuwa wao hawakuwa wakimtii Mwenyezi Mungu (swt) lilikuwa ndio sababu msingi ya kuteremshiwa adhabu.

Hivi leo, tunakabiliana na hali ngumu, ikiwemo mfumko mkali wa bei, kuongezeka kwa maovu, fujo na machafuko, uingiliaji kutoka nje na udhibiti wa wakoloni. Hata hivyo, badala ya kuchukua mafunzo kutoka kwenye Quran Tukufu na kuregea katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), bado kuna baadhi yetu wanaoendelea kupigania na kufanya kampeni kwa wanasiasa wanaokataa kwa uwazi utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) wanapokuwa madarakani. Kwa nini kuna kati yetu anayefuata wale wanaoachana na utekelezaji wa Shariah na kuifunga kwenye miito hadaifu au “hisia za Kiislamu”? Kwa vipi kunapatikana mtu kati yetu anayewafuata wale wanaotii na kujisalimisha kwa mataifa ya kigeni, bali kwa makusudi wanakiuka sheria za Mwenyezi Mungu (swt).

Yeyote kati yetu hapaswi kufanya kampeni kwa ajili ya katiba na kuikubali, katiba ambayo inatoa maamuzi kwa Bunge kuwa juu ya Sheria za Mwenyezi Mungu (swt), ambapo rai za walio wengi huweza kufuta hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) na ambapo Sheria za Mwenyezi Mungu (swt) hazitoweza kutekelezwa hadi walio wengi waidhinishe! Laa Hawla wa Laa Quwata Ila Billah. Vipi tunaweza kufuata watawala wanaoendelea kugeukia demokrasia, udikteta, ufalme, Amerika, IMF na UN, japokuwa twaghut zilizoharamishwa, mamlaka zinazohukumu kinyume na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt)? Vipi?!

Kwa uasi wote huu, maafa haya hutarajiwa kutokea. Ni maonyo kwetu. Katika muktadha wa bei za petroli, je, hatukuondosha utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuhusiana na hukmu za Sharia ya Kiislamu kwa rasilimali kama hizi kuwa ni mali ya umma na kuharamishwa kodi juu ya matumizi kama haya? Je, hatukujiingiza wenyewe katika matata haya kwa kuendelea kuishi katika dola tafauti tafauti zaidi ya 55, badala ya dola moja ya Khilafah, isiyo na mipaka kama ilivyoagizwa na Uislamu? Ni mgawanyiko huu wa dola za kitaifa ndio unaozigawanya rasilimali na kuyafanya maisha kuwa magumu kwa kila nchi ya Waislamu, huku ukitufanya dhaifu mbele ya dola za kikoloni! Je, matendo haya sio uasi kwa Mwenyezi Mungu (swt)?

Quran Tukufu imeweka wazi kuhusiana na mataifa yaliopita kwamba uasi kwa Mwenyezi Mungu (swt) matokeo yake ni udhalilifu tu duniani na Akhera. Mabadiliko yanawajabisha utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) Ambaye amesema,

[إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Surah Ar Raad :11]. Kama alivyoifasiri Sa’ady kwenye tafsiri yake,

[إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ] من النعمة والإحسان ورغد العيش [حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ] بأن ينتقلوا من الإيمان إلى الكفر ومن الطاعة إلى المعصية، أو من شكر نعم الله إلى البطر بها فيسلبهم الله عند ذلك إياها. وكذلك إذا غير العباد ما بأنفسهم من المعصية، فانتقلوا إلى طاعة الله، غير الله عليهم ما كانوا فيه من الشقاء إلى الخير والسرور والغبطة والرحمة “[إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ]

Kwa hakika Mwenyezi Mungu habadili yalioko kwa watu.” Katika neema na ihsan na furaha ya maisha,

[حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“mpaka wabadili wao yaliomo nafsini mwao.” Kupitia wao kubadilisha kutoka kwenye iman hadi kwenye ukafiri, na kutoka kwenye utiifu hadi kwenye maasia, au kutoka kwenye kushukuru neema za Mwenyezi Mungu hadi kwenye utovu wa shukrani, basi Mwenyezi Mungu huwaondoshea yote hayo. Vivyo hivyo waja watakapo badilisha yale yaliyoko katika nafsi zao katika maasia, wakaelekea kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu huwabadilishia yale walionayo katika mateso kwenda kwenye kheri, furaha, starehe na rehma.”

Kutokana na hali hizi za migogoro hii, basi na ituchochee kuregea kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kusimamisha Shariah Zake juu yetu. Dini yetu na itulazimishe kusimama dhidi ya watawala hawa, dhidi ya katiba hizi zisizokuwa za Kiislamu na dhidi ya mfumo wa kiulimwengu wa kirasilimali. Na tufanye kazi sote kubadilisha hali hii ya utovu wa utiifu kwa mfumo wa Khilafah tuliobashiriwa na Mtume. Lakini, endapo yeyote kati yetu bado anafikiri kuwa kubadilisha mtawala mmoja asiyekuwa wa Kiislamu kwa mtawala mwengine, na kuendelea kuishi chini ya katiba hii isiyokuwa ya Kiislamu kutaleta mabadiliko, basi kwa hakika huyo hajajifunza funzo lililo nyuma ya simulizi za mataifa yaliyotangulia, kama zilivyoelezwa katika Quran Tukufu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdur Rehman Saeed – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu