Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Matumaini Yanayon’garisha Ummah Wetu

Na ni Vipi Kuomba Nusra Kama Ilivyoahidiwa na Mwenyezi Mungu kwa Kufuata Nyayo za Watu Adhimu kama Muhammad al-Fatih

Muhammad al-Fatih amekitowa kilicho bora kwa ummah wetu wakati tukikumbuka zama tukufu zilizopita pamoja na watu waliokuwa viongozi na sio watawala ambao Ummah unawatweza.

Tunaposoma aya za Quran, tunakutana na aya kama, ahadi ya Mwenyezi Mungu ni Haki:

 [إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ * وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّـهِ أَفْوَاجًا* فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا]

“Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi. Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi. Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umuombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba”.  [An-Nasr:1-3]

 Ushindi ni kwa wale wanaoutafuta na kutaka msaada wa Mwenyezi Mungu.

[وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

“Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirie Waumini!” [As-Saff: 13]

Tukimchukuwa akiwa bado kijana, Muhammad al-Fatih kama ni kigezo, baba yake na washauri walielewa nini uzito wa Maneno ya Mwenyezi Mungu… kuwa sio kisomo tu cha kawaida cha aya, lakini uchunguzi wa ndani wa utambuzi wa Maneno Yake huibua kile kinachohitajika ili kupata ushindi … ushindi ulio na heshima ya kutajwa na Mtume (saw) mwenyewe pamoja na baraka kwa kiongozi huyo. Mtume (saw) amesema,

« لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Hakika mtaifungua Konstantinopli, basi kiongozi bora zaidi ni kiongozi huyo, na jeshi bora zaidi ni jeshi hilo!”

 [وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ]

“Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa miongoni mwenu wenye kutowa kabla ya ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walio toa baadaye na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Al-Hadid:10]

Maagizo ya Ayah iliyotangulia, ni kuwaandaa waumini katika hali zote kuanzia kijeshi, ikiwemo zana, mikakati na nguvu watu, na uchajimungu unaohitajika kutimiza tendo la kijasiri lenye kushangaza katika zama.

 [يَوْمَ تَرَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ يَسْعَىٰ نُورُهُم بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِم بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

Siku utakapo waona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao, na kuliani kwao; Furaha yenu leo – Bustani zipitazo mito kati yake mtakaa humo milele. Huku ndiko kufuzu kukubwa. [Al-Hadid:12]

Hata hivyo Ayah hii na nyingine nyingi zimetoa mwanga wa matumaini na nuru kwa Waislamu wa leo … kukwea kamba ya kututoa kwenye kiza, kushindwa, na mazingira ya kuhuzunisha na kuzishinda himaya za wakati huu hata kama wanakataa kuitwa hivyo lakini ukweli unaonyesha kinyume. Utanuzi wa Marekani, Uingereza, Urusi, na/au Uchina katika ardhi za Waislamu wakivuka bahari, milima, na majangwa ili kuvamia na kupora maeneo japokuwa mara nyingi madhara yanadai haki na “wa kuwajibika hayupo” kama ilivyozoeleka na maafisa wa Marekani wanapotoa taarifa kuhusiana na oparesheni zao. Matamko yasiyozingatia maisha ya mwanadamu na upotevu wa maisha na uharibifu mkubwa unaopatikana kwa wale wanaobakia baada ya kutekeleza matendo yao.

Wakimbizi waliotawanyika, waliokatwa viungo na kubaki bila uwezo wa kimaisha, wajane, wenye makovu ya kubakwa, mateso na njaa… Hizi ni athari za himaya za leo. Lakini nini kinachowabakisha Waislamu kuwa wakweli katika imani yao, na katika itikadi yao?

Itikadi ya ‘la illah illah Allah Muhammad Rasuul Allah’ humfanya mtu kuangalia zaidi ya hali ya sasa ilivyo na kujaribu kutafuta namna ya kuimaliza hali hii ya kuhuzunisha… itikadi hii ndio msuli wa Ummah wa Kiislamu unaotembea kwa nguvu ndani ya mishipa ya Ummah. Itikadi hii lazima irutubishwe kwa matendo kama yalivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Haya huonekana kwenye upinzani wa Ummah wa Waislamu japo kuwa wenziwao katika majeshi ya Waislamu wakibaki wamepooza na kutosimama pamoja nao na kukataa tawala zenye kuburuzwa. Quran ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni lazima zikamilishwe kwa uoni mpana kuuruhusu Ummah kuweza kuvuka mitihani bila ya kuacha Dini yao na kutaka malipo yanayotokana na mateso bila ya kuangukia kwenye kukata tamaa mbele ya Himaya.

Nini kinachotakiwa? Kwa nini Muhammad al-Fatih aliweza kupata utukufu katika kurasa za historia na kukumbukwa katika dua za Waislamu hadi leo? Quran inazungumza na kila mtu pindi tunapozingatia maneno…

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيًّا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto¸ ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisaa: 75]

[الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا]

“Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapigana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shetani. Hakika hila za Shetani ni dhaifu.” [An-Nisaa: 76]

Ushindi ni kwa wale wenye kumnusuru Mwenyezi Mungu…ulio ahidiwa na Muumba Mwenyewe kwa Waumini. Ahadi hii kutoka kwa Muumba ni Itikadi yetu, imani ya yaqini ya ndani.

Kinachohitajika hivi sasa ni matayarisho … kuipa nguvu Aqeedah … kuisoma hali halisi ya maisha, ya sasa na iliyopita, na kuendeleza ilimu changamano ya kisasa na matayarisho ya kusimama mbele ya himaya za leo bila uoga wala shaka ya kutoweza. Kwa kuwa itikadi ni sehemu isiyotenganishwa na matayarisho, na bila yake hakuna malipo wala ushindi. Kuomba kuwa wapokezi wa bishara njema za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw), Mwenyezi Mungu (swt) anatuagiza,

[وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّـهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّـهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ]

Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamuwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa. [An-Anfal: 60]

Na hivyo Muhammad al-Fatih ameweza kufanikisha moja ya bishara njema za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) katika mwaka 1453 Miladi, kuna nyingine mbili bado zinahitaji kufikiwa. Nani atatangaza kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume duniani? Dola itakayovunja pingu za himaya za leo katika ardhi za Waislamu? Nani atapata utukufu wa jambo hili kubwa ardhini na mbinguni? Mambo matatu ambayo Mtume (saw), ameyasema kutokana na Wahyi, ameyataka kwa Ummah. Thawban amepokea kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwamba alisema:

«إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الأَحْمَرَ وَالأَصْفَرَ وَإِنِّي سَأَلْتُ رَبِّي لأُمَّتِي أَنْ لاَ يُهْلِكَهَا بِسَنَةٍ عَامَّةٍ وَأَنَّ لاَ يُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُوًّا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ وَإِنَّ رَبِّي قَالَ يَا مُحَمَّدُ إِنِّي إِذَا قَضَيْتُ قَضَاءً فَإِنَّهُ لاَ يُرَدُّ وَإِنِّي أَعْطَيْتُكَ لأُمَّتِكَ أَنْ لاَ أُهْلِكَهُمْ بِسَنَةٍ عَامَّةٍ وَأَنْ لاَ أُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُوًّا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ وَلَوِ اجْتَمَعَ عَلَيْهِمْ مَنْ بِأَقْطَارِهَا أَوْ قَالَ مَنْ بَيْنَ أَقْطَارِهَا حَتَّى يَكُونَ بَعْضُهُمْ يُهْلِكُ بَعْضًا وَيَسْبِي بَعْضُهُمْ بَعْضًا»

Kwa hakika Mwenyezi Mungu amenikusanyia ardhi basi nikaona mashariki yake na magharibi yake. Na hakika Ummah wangu utafikia utawala wake kote niliko onyeshwa. Na nimepewa hazina mbili; nyekundu na nyeupe. Na nimemuomba Mola wangu kuwa Ummah wangu usihilikishwe na ukame unaoenea, na usisalitiwe na adui mbali na wao, kufikia katikati ya utawala. Na Mola wangu amesema: Ewe Muhammad! Ninapohukumu jambo basi halirudi. Na hakika Mimi nimekupatia kwa Ummah wako kwamba hawato angamizwa na ukame unaoenea na kuwa hawatosalitiwa na maadui mbali na wao wenyewe kufikia katikati ya utawala wao japokuwa watawakusanyikia kutoka sehemu zote. Au akasema: ‘Miongoni mwa maeneo. Lakini baadhi yao watawaangamiza baadhi, na baadhi yao watawashika wengine.’

Wakati da’wah ilipokuwa katika hatua ya mwanzo Makkah. Khabbab bin al-Arat (ra) alikuja kwa Mtume (saw) wakati wa udhaifu na mateso walipokuwa bado wapo Makkah

عَنْ خَبَّابِ بْنِ الأَرَتِّ، قَالَ شَكَوْنَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ مُتَوَسِّدٌ بُرْدَةً لَهُ فِي ظِلِّ الْكَعْبَةِ، قُلْنَا لَهُ أَلاَ تَسْتَنْصِرُ لَنَا أَلاَ تَدْعُو اللَّهَ لَنَا قَالَ «كَانَ الرَّجُلُ فِيمَنْ قَبْلَكُمْ يُحْفَرُ لَهُ فِي الأَرْضِ فَيُجْعَلُ فِيهِ، فَيُجَاءُ بِالْمِنْشَارِ، فَيُوضَعُ عَلَى رَأْسِهِ فَيُشَقُّ بِاثْنَتَيْنِ، وَمَا يَصُدُّهُ ذَلِكَ عَنْ دِينِهِ، وَيُمْشَطُ بِأَمْشَاطِ الْحَدِيدِ، مَا دُونَ لَحْمِهِ مِنْ عَظْمٍ أَوْ عَصَبٍ، وَمَا يَصُدُّهُ ذَلِكَ عَنْ دِينِهِ، وَاللَّهِ لَيُتِمَّنَّ هَذَا الأَمْرَ حَتَّى يَسِيرَ الرَّاكِبُ مِنْ صَنْعَاءَ إِلَى حَضْرَمَوْتَ، لاَ يَخَافُ إِلاَّ اللَّهَ أَوِ الذِّئْبَ عَلَى غَنَمِهِ، وَلَكِنَّكُمْ تَسْتَعْجِلُونَ»

Tulimlalamikia Mtume (saw) (juu ya mateso kutoka kwa washirikina) akiwa amekaa katika kivuli cha Ka’ba, ameegemea juu ya Burd (guo la kujifunika). Tulimwambia, “Kwani hututakii sisi nusra? Kwani hutuombei sisi kwa Mwenyezi Mungu?” Akasema, “Alikuwa mtu wakati wa kabla yenu akichimbiwa shimo akitiwa na kuwekewa msumeno juu ya kichwa chake na kukatwa vipande viwili; lakini hilo halikumfanya kuachana na Dini yake. Mwili wake ukichanwa kwa shanuo la chuma ambapo huondoa nyama yake kutoka kwenye mifupa na mishipa, lakini hayo hayakumfanya kuachana na Dini yake. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, jambo hili (yaani Dini ya Uislamu) itaenea ambapo mtu atasafiri kutoka Sanaa (Yemen) hadi Hadhramaut bila kumhofu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, au mbwa mwitu kuhofia wanyama wake, lakini nyinyi mna pupa.”

Kiapo ambacho Mtume (saw) ameapia: “Naapa Kwa Mwenyezi Mungu, Jambo hili (yaani Dini ya Uislamu) itaenea,” amesema “Mwenyezi Mungu” kuhakikisha na kusisitiza kuwa ushindi utakuwa wa uhakika kwa waumini. Bila shaka waumini wanakumbana na huzuni, kutokuwa na subra, uchovu; lakini kutokana na Ayaat na Hadith nyoyo zetu hujazwa na kushajiishwa kukamilisha bishara ya pili ya Mtume (saw),

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

 “…Kisha itakuwa tena Khilafah kwa njia ya Utume”

Maneno yaliyotamkwa na ulimi uliobarikiwa kutokana na Wahyi.

Hapa Aya na Hadith hizi zina sanifu kupitia fikra zetu kujenga misuli ya vijana wa leo watakao vunja kizuizi cha ukimya na kwa majeshi ya Waislamu kuondokana na hali ya usingizi mzito na kuheshimika leo na kesho. Uislamu utakuwa ndio mshindi bila shaka, lakini kwa mikono ya nani haya yatafikiwa?

Hapa kuna mashindano ya kukimbilia heshima hiyo tukufu. Hii itatupa matumaini – utulivu ambao Uislamu utaurejesha. Ili nusra (ushindi) ipatikane – sisi tukiwa Waislamu tunapaswa kutekeleza jukumu letu kwa uwezo wetu wote; hichi ndicho tutakachohisabiwa juu yake – kutenda dhidi ya kutotenda – sio kuhisabiwa juu ya muda (wa kupatikana mafanikio) kwa kuwa uko kwenye milki ya Mwenyezi Mungu Pekee. Hivyo kwa kuihisi furaha ya Nuru ya Uislamu inayodhihirishwa katika Dola yake,

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّـهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

 “Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.”  [Ar-Rum: 4-5]

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari na

 Manal Bader

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu