Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muda wa Khilafah Umewadia

Katika mwezi huu wa Rajab, 1441, itatimia miaka 99 tokea kuvunjwa kwa Khilafah kupitia ushirikiano wa wasaliti miongoni mwa Waarabu na Waturuki pamoja na maadui wakoloni. Katika Ulimwengu wote wa Waislamu, kukosekana kwa utekelezaji wa hukmu zote za Mwenyezi Mungu kunahisiwa, kunakotupelekea kukata tamaa. Pakistan haina tofauti, kwani matumaini ya mwisho ya nidhamu ya utawala nchini Pakistan imetuvunja moyo na kuvunjwa vipande vipande. Bila shaka, serikali ya “mabadiliko” imeshindwa kuzuia ufisadi, kuharibiwa uchumi wetu na kuteketezwa usalama wetu na wakoloni hivi leo.

Tumekata tamaa kwani ufisadi umepata maisha mapya, kukiwa hakuna pesa iliyorudishwa kutoka kwenye safu ya majenerali na wanasiasa mafisadi, waliojaza matumbo yao kwa fedha zetu na kukaribia kupasuka. Tumekata tamaa kwa kuwa Pakistan imezamishwa hadi shingoni ndani ya madeni, yaliyo na riba inayochukiza, ambayo ni wito wa vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Tumechanganyikiwa kutokana na masharti ya kikoloni kuhusiana na mikopo ya kigeni inayo nyonya rasilimali zetu, huku ikitoa kipigo kwa viwanda vyetu vya ndani, kilimo na sarafu kuifikisha kwenye kiwango kisichostahiki ili kudumisha ubabe wa uchumi wa kigeni.

Tunatikisa vichwa vyetu kwa huzuni wakati vilio vya Waislamu wa Kashmir iliyotawaliwa vikikumbana na “kizuizi”, kauli zisizo na meno na hatua za ishara tu, sambamba na sera ya Amerika kuruhusu kuibuka Dola ya Kihindu kama ni Akhund Bharat, “India Kuu”. Na tumekuwa wenye wasiwasi huku utawala unaangusha nyundo juu ya miguu yetu, kwa kuwa kama wasaidiaji tulioajiriwa kuhifadhi uwepo wa “Raymond Davis” mwanakandarasi binafsi wa Amerika wa masuala ya kijeshi nchini Afghanistan, wakikaribia vifaa vyetu vya nyuklia, chini ya kisingizio cha mpango unaopigiwa tarumbeta wa uondoaji mchache wa vikosi vya kijeshi vya kawaida.

Hakuna mwisho wa kukata tamaa kwetu, isipokuwa tuangalie mbele zaidi ya nidhamu iliyobuniwa na wanadamu kuelekea Dini yetu Tukufu, iliyofunuliwa na Bwana wa Ulimwengu, Mwenyezi Mungu (swt). Tumeshuhudia namna gani mtu mmoja, aliyeungwa mkono na jeshi letu, hawezi kuchukuwa hatua za kurekebisha ufisadi wa asili wa Demokrasia. Tumekuwa kama watu tuliogandishwa, hatuwezi kusonga mbele kwa uongozi uliopo, wala kurudi nyuma kwenye uongozi uliopita. Katika hali hii, lazima tujiulize: kwani hakuna njia ya jeshi letu kutoa Nussrah yake kwa Hizb ut Tahrir kwa kurejesha tena Khilafah kwa njia ya Utume?

Bila shaka, Khilafah ni njia ya utawala katika Uislamu, kuchunga mambo yetu kwa mujibu na Qur’an na Sunnah, kiasi kwamba kila sheria na kifungu cha katiba yake ni kwa mujibu wa dalili ya wahyi. Zaidi ya hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameweka ufaradhi wa Bay’ah (ahadi ya utiifu) kwa Khalifah kwa kuufunga kwa kutokuwepo kwake na kifo kibaya zaidi kati ya vifo vyote, kufa kwa kisichokuwa Uislamu,

  «مَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Yeyote anayekufa bila kuwa na Bay’ah (ahadi ya utiifu) shingoni mwake amekufa kifo cha kijahiliya” (Muslim). Ni faradhi juu ya kila mmoja wetu kuwa na Bay’ah kwa Khalifah iwepo katika kipindi chetu. Hakika, huu ni muda wa Khilafah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Pakistan

#TurudisheniKhilafah   

#YenidenHilafet     

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu