Ijumaa, 12 Sha'aban 1445 | 2024/02/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Khilafah: Utajiri Wenye Uwezo

Katika mwezi wa Rajab 2020 Miladia, itakuwa ni kumbukumbu ya miaka 99 Hijria tokea kuangushwa kwa Khilafah. Baada ya kuonja matunda machungu wa Usoshalisti katika miaka ya 1950 na kisha njozi za uhuru katika kipindi cha miaka 1960 na 1970, hali ya Ummah kote ulimwenguni imebakia kuwa ni ile ile kama sio mbaya zaidi. Matokeo yake, matatizo yanayoukumba Ummah yameongezeka kuwa masuala mengi zaidi.

Ummah unakumbana na changamoto kadhaa tokea kuvunjwa kwa Khilafah ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa ajili ya mabadiliko. Changamoto kama umasikini, maendeleo, afya pamoja na ukuaji wa uchumi, mgawanyo wa utajiri na maendeleo ya viwanda. Kwa bahati mbaya mjadala kama huo umepindisha mjadala wa mabadiliko, na wakati huo huo vikwazo vingi vya kimada vinahitaji kutatuliwa na Ummah, mabadiliko kutoka baadhi ya mitazamo imebaki ni kizuizi cha kisaikolojia zaidi kuliko cha kimada, yaani, je Ummah unaamini kuwa mabadiliko yanawezekana?

Utashi wa Kisiasa

Kuzaliwa kwa taifa lolote kunahitaji wale wanaounga mkono mabadiliko na wale wanaoshiriki katika kuchipuza kwake, kutathmini nguvu na manufa ya taifa. Mambo hayo huzingatiwa ni muhimu lakini kukosekana kwake kutahitaji maendeleo ya sera ili yaweze kutatuliwa.

Otto Van Bismarck alisimamia uunganishaji wa Ujerumani ambao uliiweka nchi katika njia ya kufikia ubwana wa kiviwanda. Kuanzia mwaka 1884, Ujerumani ilianzisha makoloni kadhaa nje ya Ulaya ili kukabiliana na uhaba wa rasilimali za madini. Bismarck aliweza kufanikisha muungano wa ardhi za Ujerumani ambapo wengi walijaribu kwa takribani miaka elfu. Muungano huo ulimaanisha rasilimali na madini ya Ujerumani yote yalifuata sera moja iliyounganishwa, na mara moja Ujerumani iliweza kujiinua nchini mwao bila kukumbana na miito yoyote ya kujitoa kwenye shirikisho.

Hivyo hivyo Japani tokea mwanzoni mwa karne ya 20 iliweza kuendeleza viwanda vyake, hata hivyo ukuwaji wa haraka wa uchumi umeifanya Japan kuwa na huzuni kwa kuwa kwake na rasilimali chache. Japani imetatua udhaifu huo kupitia programu ya kijeuri ya utanuzi wa maeneo kwa kuiteka ardhi ya Korea na kusonga ndani zaidi katika maeneo ya Uchina ili kupata nguvu kazi na rasilimali. Kwa namna kama hiyo Himaya ya Uingereza ilivamia maeneo ya kigeni kwa ajili ya masoko ya bidhaa zake na kutumia nguvu za watumwa kwa kutatua tatizo la wafanyakazi ndogo ndogo.

Mifano hii inaonyesha kuwa mataifa yote yanahitaji baadhi ya vitu msingi ili kuibuka kuwa mataifa yenye nguvu na yakaweza kwa haraka kuwa na kiwango bora cha hali ya maisha kwa watu wake ndani ya mipaka salama. Muendelezo wa miundo mbinu, viwanda vya ulinzi na nguvu ni vya msingi kwa taifa lolote, hivyo umiliki wa rasilimali za madini huwa ni nguvu ya kimikakati na fursa adhimu kwa kuibuka kwa taifa. Mifano ya Ujerumani na Japan ni mifano ya mujtama – sahihi au zisizo sahihi, zilizoweza kutatua uhaba wa matofali msingi kwa ujenzi wa taifa jipya.

Uwezo wa Ummah  

Mtu anapoangalia uwezo wa Ummah, ardhi za Waislamu sio tu humiliki sehemu nyeti za ujenzi kwa taifa jipya, lakini ni zaidi na mbele ya huu uhalisia wa Khilafah kuibuka kuwa ni taifa lenye nguvu kubwa kutokana na vitegemezi vingi itakavyorithi vilivyomo katika ardhi za Waislamu.

Ardhi za Waislamu zinamiliki asilimia 74 ya hifadhi ya mafuta, ni zaidi ya hifadhi yote ya ulimwengu iliyobakia.

Zinamiliki asilimia 54 ya hifadhi ya gesi, ina hifadhi ya dhahabu ya dola trilioni 1 na askari wa kudumu milioni 4.7. Yote haya huiwezesha Khilafah kuchukua nafasi ya juu katika masuala ya kijeshi na kuwa na msingi imara katika kuunda.

Ummah wa Kiislamu kwa ujumla unamiliki zaidi ya mapipa bilioni 700 ya mafuta na nusu ya gesi yote duniani. Vikiwa vyote ni vyanzo muhimu vya nishati. Katika hali hii nchi za Waislamu zinazalisha nusu ya mahitaji ya mafuta ya kila siku ya ulimwengu na asilimia 30 ya mahitaji ya gesi duniani. Pamoja na hayo Saudi Arabia inamiliki eneo kubwa zaidi la visima vya mafuta duniani, wakati Qatar na Iran zinamiliki eneo kubwa zaidi la gesi duniani.

Ummah wa Kiislamu ndio unaokuwa kwa kasi zaidi duniani unaokaribia bilioni 2, muhimu zaidi ni kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Ummah ni chini ya umri wa miaka 28. Suala la umuhimu wa idadi kubwa ya watu kwa maendeleo ya kiuchumi nchini na ulinzi ni la maana sana. Ukusanyikaji huu wa wafanyakazi humaanisha nchi inaweza kujengwa kwa kasi zaidi bila kuchukua miongo kadhaa kabla ya kuweza kujitegemea.

Pamoja na haya Ummah utarithi faida nyingi. Mtawanyiko wa kijiografia wa Ummah na ardhi za Waislamu humaanisha kuwa baadhi ya maeneo nyeti ya kimikakati ya njia za majini na anga zitakuwa chini ya mikono ya Waislamu. Asilimia 40 ya mafuta duniani hupitia mlango bahari wa Hormuz ambayo njia yake ya maji imeenea baina ya Ghuba ya Oman upande wa kusini mashariki na Ghuba ya Kifursi upande wa kusini magharibi. Ukweli huu pekee unaifanya kuwa ni njia muhimu zaidi katika ulimwengu. Mfereji wa Suez unaopitia Misri huzingatiwa ni moja ya njia muhimu zaidi za majini kwani inaunganisha masoko ya Asia kuelekea upande wa Mediterranean na Ulaya. Asilimia 7.5 ya biashara ya ulimwengu inapitia kwenye mfereji huu. Hali kadhalika Muhammad (saw) alihakikisha kuwa njia nyeti za biashara katika Hijaz zilikuwa chini ya udhibiti wa Waislamu, ambapo iliwadhoofisha vibaya maadui wa Uislamu katika kufanya harakati za kijeshi na kuudhoofisha Ummah.

Wakati wengi katika Ummah wanaishi kwenye umasikini wa kutupwa, hii si kwa kingine isipokuwa ni kutokana na kuwa kilimo katika ardhi za Waislamu kimeachwa. Kwa hakika, kwa kutumia sera sahihi Khilafah inaweza kuwa mlishaji mkuu wa ulimwengu. Kilimo nchini Misri kinafanyika katika kiasi cha ekari milioni 6 za ardhi yenye rutuba kwenye bonde la Mto Nile na Delta. Imeifanya Misri kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa za kilimo na ni mzalishaji mkubwa zaidi wa tende, mzalishaji wa pili mkubwa wa nyama ya bata bukini na mzalishaji wa tatu mkubwa wa nyati na nyama ya ngamia. Pakistan sio tu humwagilia ardhi kubwa zaidi kuliko Ulaya yote kwa pamoja, lakini pia Pakistan ni mzalishaji mkuu wa pili wa njegere, nyama ya nyati na maziwa, mzalishaji mkuu wa nne wa apricot, pamba, nyama ya mbuzi na embe na ni ya tano kwa uzalishaji wa vitunguu na miwa. Wakati huo huo Uturuki ni mzalishaji mkubwa zaidi wa hazelnut, tini, apricot, cheri na makomamanga. Ummah unastahili kuwa mlishaji mkuu wa dunia. Lakini kutokana na uwekaji wa sera za muda mfupi na ufisadi, licha ya kuwa na uwezo huu bado Ummah unateseka katika umasikini.

Ardhi za Waislamu pia zinamiliki kiyayusho kikubwa zaidi cha aluminium nchini Bahrain, kilicho na umuhimu mkubwa kwa uendelezaji wa viwanda, mgodi mkubwa zaidi duniani wa dhahabu katika Jangwa la Qizilqum Uzbekistan, kiwanda kikubwa zaidi duniani cha aluminium nchini Tajikistan, mgodi mkubwa zaidi wa makaa ya mawe katika jangwa la Thar Pakistan na mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa tini nchini Indonesia.

Tatizo Halisi   

Swali la kiukweli linalohitaji kuulizwa ni vipi kwa watu walio na utajiri na wingi wa rasilimali kiasi hicho, katika hali halisi kuwa masikini kiasi hicho? Kuna sababu moja kwa hili nalo ni kuwa watawala wa ardhi za Waislamu hawakuwa na nia kabisa ya matumizi mazuri ya utajiri huo mkubwa kwa ajili ya watu wake. Ardhi zetu zinaendeshwa na watawala dhalimu waliowekwa kwa nguvu za wakoloni, ambao baada ya kuondoka kwao walihakikisha ardhi ndogo inamilikiwa na watu wa daraja kubwa au familia zinabakia katika nafasi yake. Lengo lao la msingi ni kumiliki nchi wanazozitawala, kuwaingiza jamaa katika kabila, watu wa familia na watiifu kwa serikali ili kuwa na udhibiti mzito wa nchi. Kutokana na haya, maendeleo, uchumi na kusonga mbele kiteknolojia ni kipaumbele cha pili kwao, kwa kuwa suala la kwanza kwao ni kushika hatamu za madaraka.

Kinyume chake ni kuwa rasilimali za Ummah huu zitatumika na Khilafah kuuendeleza Ummah huu kuwa dola kiongozi katika nyanja zote za kimaisha, kama tulivyokuwa mwanzoni wakati ardhi zetu zikitawaliwa kwa mfumo wa kiwahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Ardhi za Waislamu zinamiliki vitu vyote muhimu vinavyohitajika kuyabeba mambo yetu kwa mikono yetu wenyewe, kunahitajika sasa kiongozi atakaye timiliza uwezo wa Ummah huu. Ummah hauna haja ya kutawala watu wengine au kuingia katika utanuzi wa maeneo kama zilivyofanya nchi za Ujerumani na Japan na Himaya ya Uingereza, kwa kuwa zina vitu vyote muhimu vilivyo ndani ya mipaka yake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:40

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu