- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kwa Nini Xinjiang ni Muhimu kwa Uchina
Ukandamizaji wa Uchina wa kupita mipaka dhidi ya Waislamu haujawahi kushuhudiwa duniani kote. Mwaka uliopita umeshuhudia matukio ya ripoti na video zikionesha Waislamu wa Uyghur wakijazwa ndani ya kambi zilizotapakaa ndani ya magharibi ya Uchina. Huku shinikizo zikizidi kutoka katika vyombo vya habari vya Magharibi, ambavyo vina ajenda yao, sasa utawala wa Uchina umekubali kuwa inatekeleza unyama huo: kisiwa cha kambi kimejengwa. Shirika la habari linaloendeshwa na serikali ya Uchina la Xinhua siku ya Jumamosi 13 Oktoba 2018 lilimnukuu afisaa rasmi kuwa lazima dini zipitie "mchakato wa kuzifanya mujtamaa zisizokuwa za Kichina kuwa chini ya athari ya thaqafa ya Kichina." Licha ya Uchina kuinuka kiuchumi kimiujiza, inaendelea kutapatapa dhidi ya eneo hili ambalo halijamakinika, lakini ni muhimu kwa Uchina na sio tu kimikakati bali hata kwa maisha yake.
Eneo Huru la Xinjiang la Uyghur (XUAR) lipo upande wa kaskazini magharibi ya Uchina na limetapakaa kwa kilomita mraba milioni 1.6. Eneo hili linajumuisha moja kwa sita ya eneo la Uchina na linapakana na nchi nane. Leo Xinjiang ni nyumbani kwa watu milioni 21 wanaotoka katika makabila kumi na tatu na kubwa likiwa ni la Waislamu wa Uyghur. Kihistoria eneo hili limekuwa kitovu msingi cha kiuchumi na kubadilishana thaqafa kati ya Mashariki na Magharibi, Xinjiang ilikuwa kitovu muhimu cha Barabara ya Siliki. Kuzidi kwa ukandamizaji wa Ulaya miaka ya 1800 kulipelekea kupanuka kwa Falme za Urusi na Uingereza ndani ya Asia ya Kati. Ufalme wa Urusi ulizidisha athari yake katika mipaka ya kaskazini mwa Uchina katika Karne ya 19 na kwa sababu hiyo Ufalme wa Qing ukalitia eneo hilo chini ya udhibiti wake na kubuni Xinjiang kama mkoa rasmi wa Uchina mnamo 1884. Lakini utawala huo ulipata mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa Waislamu wa eneo hilo na katika nusu ya Karne ya 19 ambapo Uchina chini ya Qing ilipoingia katika Vita vya Madawa ya Kulevya, muendelezo wa mashambulizi ya ndani na kuingiliwa na mkono wa nje; kwa hivyo haikuweza kuwekeza jeshi lenye nguvu ndani ya Xinjiang. Kuanguka kwa Ufalme wa Qing mwaka 1911 ukapelekea udhibiti wa Uchina katika eneo la Xinjiang kuondoka kabisa. Ikamchukua Mao Zedong hadi mwaka 1949 kupiga marufuku uhuru wa eneo hilo na kuliteka kuwa chini ya Jamhuri ya Zedong. Mara hii Mao alijaribu kuwatawanya katika mikoa mengine wakaazi wa eneo hili Waislamu kwa kutumia nguvu na kuwahamisha Wachina wa Han kwenda katika eneo hilo. Sera hii bado inaendelea hadi leo lakini imefeli kwa ukamilifu wake na kilele chake ni uasi wa Ürümqi mnamo 2009.
Xinjiang inawakilisha eneo moja kati ya maeneo manne kama ngao ya Uchina. Maeneo ngao yanaulinda moyo wa ardhi ya Uchina. Moyo wa ardhi ya Uchina umegawanyika vipande viwili, kaskazini na kusini ambayo zinawakilishwa na lugha mbili msingi, Kimandarini kutoka kaskazini na Kikantoni kutoka kusini. Moyo wa ardhi ya Uchina ipo katika mito miwili mikubwa –Mto wa Yelo kaskazini na Yangtze kusini. Moyo wa ardhi ya Uchina ni eneo la kilimo. Idadi ya waHan haikusambaa kote ndani ya moyo wa ardhi ya Uchina. Idadi kubwa ya watu iko mashariki kwa sababu magharibi ya Uchina haina mvua nyingi na hivyo haiwezi kuhimili idadi kubwa ya watu. Hivyo basi Uchina ni nchi nyembamba mno, ikiwa na idadi kubwa ya watu waliotapakaa. Mjumuiko wa maeneo yasiyokuwa ya waHan yanauzunguka moyo wa ardhi –Tibet, Mkoa wa Xinjiang, Mongolia ya Ndani na Manchuria. Haya ndio maeneo ngome ambayo kihistoria yamekuwa chini ya utawala wa Uchina wakati Uchina ilipokuwa na nguvu na yakajitenga wakati Uchina ilipokuwa dhaifu au yametumiwa na dola za nje zenye nguvu ili kuingilia kati ndani ya Uchina. Haya pia ndio maeneo kihistoria ambayo ni chimbuko la vitisho dhidi ya Uchina. Lakini kando na kuwa ni maeno ngome, kuyadhibiti yanaipa Uchina nguvu ya kujilinda. Hivyo basi Xinjiang ni moja ya maeneo manne ambayo ni muhimu kwa umakinifu wa himaya ya Uchina.
Maajabu ya uchumi wa Uchina yamehusishwa na kuwepo kwa kawi na bidhaa. Xinjiang ni eneo muhimu ambalo linalohitajika kuendesha uchumi wa Uchina na pia lipo mahali muhimu kimikakati kama njia ya usambazaji. Xinjiang ina asilimia 20 ya makaa, gesi ya kawaida, na hazina za mafuta. Xinjiang ina idadi kubwa ya hazina ya kawi kuliko maeneo yote nchini humo, Mafuta yaliyoko katika Karamay ni mengi ndani ya Uchina yote na eneo hilo lina makaa mengi, fedha, shaba, chuma, naitreti, dhahabu na zinki. Xinjiang ni eneo kubwa ndani ya Uchina linalotoa gesi ya kawaida na ndio kitovu cha biashara na njia za mabomba ya mafuta kutoka eneo la Asia ya Kati na kwengineko. Xinjiang pia ni sehemu ya Uchina ya kuwekeza zaidi rasilimali zake za mafuta kwa kuwa eneo hilo pia ni njia muhimu ya usafirishaji. Xinjiang ni eneo pekee ndani ya Uchina ambalo linapakana na jamhuri za Asia ya Kati, mafuta ya Asia ya Kati (na idadi kubwa ya mafuta ya Urusi) yanaingilia kwa kupitia mabomba ya Uchina yaliyoko Xinjiang. Bomba la kwanza la mafuta la kimataifa lililowahi kujengwa ni Bomba la Mafuta la Kampuni ya Sino-Kazakh ambalo lilianza kupiga mafuta kuanzia Julai 2006. Bomba hili lilianza kutoka Atasu kaskazini Kazakhstan likaingia eneo la Xinjiang katika mpaka wa Kazakh-Uchina katika Alashankou na kuishilia katika PetroChina Dushanzi. Ilhali Xinjiang haikujumuishwa katika miujiza ya Uchina lakini kiukamilifu hiyo ndio inayoimakinisha Uchina na kwa sababu hiyo ni eneo muhimu la kimikakati.
Kuinuka kwa Uchina ilipelekea kuundwa kwa Maeno Maalumu ya Kiuchumi (SEZ) katika meaneo ya pwani ya Uchina ambapo bidhaa zinatengenezwa kwa usafirishaji duniani kupitia bahari. Tatizo la Uchina ni kuwa limeufanya uchumi wake kutegemea njia za bahari lakini Uchina haina uwezo wa kijeshi wa kuweza kutoa ulinzi kwa njia zake za usambazaji baharini. Kwa sababu Jeshi la Bahari la Amerika linadhibiti bahari duniani na kufungiwa njia visiwa vinavyoizunguka Uchina katika eneo linatepelekea kusambaratika kwa uchumi wake. Hii ndio inaipelekea Xinjiang kuingia katika hesabu kwani kihistoria Uchina imekuwa ikiitumia kama njia ya ardhini kuelekea duniani. Magharibi ya Uchina inapeana nafasi kubwa njia za Bahari ya Arabia kupitia Pakistan hadi kwa Bahari ya India na Guba ya Fursi. Uchina inaweza kupitia Pakistan, Asia ya Kati, Mashariki ya Kati na eneo lote la Eurasia (mjumuiko wa Ulaya na Asia) na zaidi kupitia Xinjiang na kusafirisha rasilimali zake kwa njia ya ardhini na kuepuka kutegemea kupindukia kwa njia za bahari zisizotegemeeka. Ni kwa sababu hii ndio Uchina kupitia mkakati wake mkubwa wa Mpango wa Ukanda na Barabara (BRI) utakuwa na vitengo kadhaa vikipitia Xinjiang ili kuunganisha nchi yote na Eurasia na zaidi. Kwa kutumia njia hiyo, Xinjiang imekuwa kijiografia muhimu mno kufikia uunganishaji wa kiuchumi kwa Eurasia yote. Mpango mzima wa BRI unaahidi kuwa na athari kubwa juu ya mahusiano ya kibiashara ya Uchina na athari yake kimataifa na katikati ya hilo ni Xinjiang.
Sababu za kimikakati, kiuchumi, kibiashara, kiidadi ya watu na kisiasa zinaifanya Xinjiang kuwa ni suala la kimaisha (kufa kupona) kwa Uchina. Lakini licha ya kutumia pesa nyingi katika eneo hilo na hapo awali kutumia mkono wa chuma imefeli kuwavutia Waislamu katika eneo hilo. Ilhali vyombo vya habari vya kimagharibi hivi sasa ndio vimeangazia yanayofanywa na Uchina. Mikakati ya Beijing inafuata nyayo za Magharibi ambao wanamipango sawa na hiyo yakuwa shughulikia Waislamu, ambao kwa muda mrefu wameng'ang'ana kuwaunganisha. Njama hizi zimefeli huko Magharibi na haina shaka zitafeli ndani ya Uchina. Suala linalo waumisha vichwa viongozi wa Uchina ni kuwa uchumi na siasa zao za usoni zinapitia katika eneo ambalo lina idadi kubwa ya Waislamu ambao Beijing imekuwa ikiwapiga vita kwa zaidi ya karne.
Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahri na
Adnan Khan