Jumatano, 01 Rajab 1446 | 2025/01/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ziara ya Haraka ya Trump ya Ulaya, Uingereza na Urusi

Ziara ya haraka ya Trump ya Ulaya, Uingereza na Urusi imeuacha ulimwengu ukishangaa ikiwa Amerika iko makini kuhifadhi mfumo wa uhuru ulioko kwa sasa. Trump kumsifu Merkel kuwa mateka wa Urusi na kushutumu wazi wazi mipango ya May ya kuiondoa Uingereza katika Muungano wa Ulaya (Brexit) inaashiria zaidi ya sintofahamu nyepesi katika kitovu cha muungano wa nchi zilizopakana na bahari ya Atlantiki. Kuongeza chumvi kwenye kidonda, Trump alisonga mbele na kuuita Muungano wa Ulaya adui huku akitarajia mkutano usiokuwa wa kawaida wa kirafiki na Putin mjini Helsinki. Licha ya Trump kupata upinzani nchini kwake na majaribio yalojaa dosari ili kuficha kufurahishwa kwake na Urusi, mtazamo wake wa kiulimwengu uliojengwa juu ya Amerika kwanza unazungumza kwa upana kuhusu aina ya ulimwengu ambao furaha yake ingependa kuuona.       

Siku za nyuma, majina kama umoja wa vilele, ukwepaji, kujitolea, ubwana, na kichaa mara nyingi yalitumika kuisifu dola ya Amerika katika kuunda na kulinda mfumo wa uhuru. Neno dola ya hali halisi liliizunguka hali hii kwa ustadi. Zile dola zisizo ridhishwa na mfumo wa kiulimwengu wa Amerika – mithili ya Urusi na China – ziliorodheshwa kama dola za kisasa. Leo, tabia ya Amerika inaonyesha kwa upana miondoko hii ya dola hii ya kisasa kuliko kuwa ni dola ya hali halisi.

Huku wengi wakishindwa kuitambua Amerika kama dola ya kisasa, baadhi wanakiri kuwa Trump ni raisi wa kisasa. Lakini hata uorodheshaji huu ni wa kimakosa na unaopotosha. Kwa vyovyote vile, Waamerika milioni 60 hawaridhiki kamwe na mfumo wa uhuru na kumchagua Trump kuugeuza, na mpaka sasa bado hajawavunja moyo. Uungwaji mkono huu mpya alioupata unatoa motisha muhimu nyuma ya Trump anayeonekana kuwa mwana mamboleo matata mwenye balagha kuanzia katika biashara hadi katika mabadiliko ya hali ya anga.   

Licha ya vimbwanga na vurugu lote linalonasibishwa na uraisi wa Trump inaonekana kana kwamba kuna mkakati wa kichini chini wa kuunga mkono mwito wa idara wa Amerika kwanza. Kuasi kwa Trump makubaliano baina ya nchi mbali mbali ni ishara ya kwanza kwamba Amerika haitaki kujifunga kwa sheria za mfumo wa uhuru na wala haijali kuhusu matokeo yake. Badala yake, Trump anatafuta kubadilisha makubaliano baina ya nchi mbali mbali kwa makubaliano baina ya nchi yake na nchi nyenginezo. Katika ziara yake ya Ulaya ya hivi majuzi, alisisitiza katika mahojiano na gazeti la The Sun kwamba Amerika itaingia tu katika muungano wa kibiashara na Uingereza endapo Waziri Mkuu May atachagua kujiondoa barabara katika Muungano wa Ulaya (Brexit) – kujiondoa kikamilifu katika Muungano huo. 

Mbali na biashara, idara ya Trump inatamani wazi wazi kuingia ndani ya bara Ulaya. Lengo kuu ni kuunda na kushajiisha mahusiano na wazalendo wa Ulaya ili kuuvunja Muungano wa Ulaya. Kwa mtazamo wa Trump, kuwepo na mkusanyiko wa mataifa ya Ulaya yanayogombania ubwana ni bora zaidi kuliko kuwepo kwa Muungano wa Ulaya na hili litaisaidia Amerika katika kufanya mikataba kati yake na nchi nyenginezo tofauti tofauti za Ulaya.    

Kwa miongo kadhaa, muungano kati ya nchi zinazopakana na bahari ya Atlantiki umehudumu kama msingi wa mfumo wa uhuru, ambao Amerika imeuongoza. Lakini, idara ya Trump inatafuta kuitelekeza Ulaya na kuasisi miungano mipya na washirika wa Ulaya na dola mahasimu wa zamani mithili ya Urusi. Jaribio hili shupavu la kuitupilia mbali miungano ya zamani limewatia tumbojoto viongozi wengi wa Ulaya. Waziri wa Kigeni wa Ujerumani alisema hivi majuzi kuwa Ulaya haiwezi tena kuitumainia Amerika kikamilifu.  Kwengineko katika eneo la Mashariki mwa Ulaya, nchi zilizo jirani na mpaka wa Urusi zina wasiwasi kuhusu usalama wa Amerika wa kudumu. Kutotabirika kwa Trump juu ya NATO na kutoweza kwake kumhisabu Putin juu ya kuunganishwa kwa Crimea na Urusi na uvamizi wake kwa Ukraine unatilia nguvu wasiwasi huo.   

Muamala wa Trump kwa nchi za kisasa pia unavutia. Kuhusu Urusi, inazidi kuwa ni kawaida kwamba Trump anatafuta kufufua vita baridi vya ushirikiano ambavyo Kissinger alivianzisha. Putin na washauri wake wapambe wanasubiri kwa hamu kupanua ushirikiano wa Urusi na Amerika kuanzia nchini Syria hadi viwanja vyenginevyo vya kivita na ushawishi. Ama kuhusu China, mwelekeo wa Trump umekuwa ni kufanya vita vya kibiashara na China na wakati huo huo kuomba ushirikiano wa Beijing juu ya suluhu ya matarajio ya kinuklia ya Korea Kaskazini. 

Shaka iliyopo ni chache kuwa ukarabati mpya wa miungano ya dola kuu chini ya Trump umevuruga mfumo wa uhuru na kuubadilisha kwa nidhamu ya kimataifa chini ya shinikizo la kudumu. Kukabiliana na mvurugiko huu ni changamoto kwa mataifa mengi kwani mengi yao hayawezi kuhimili hatari na fursa zilizomo ndani ya kipindi hiki cha mpito. Ilhali kuna nchi ambazo ziko katika nukta muhimu za ramani ya mabadiliko lakini zinashindwa kuchukua fursa hiyo.  

Ulimwengu wa Kiislamu unajumuisha nchi bandia hamsini na tano, unaoanzia upande wa Mashariki hadi Magharibi, unaomiliki maeneo muhimu mno ya kijiografia na uliobarikiwa na rasilimali na utajiri kochokocho. Lakini katika mkorogo huu wa mabadiliko katika nidhamu ya kimataifa uliosababishwa na Trump, Waislamu bilioni 1.6 wamesalia kuwa mateka wa viongozi wenye maono finyo wanaopendelea kubakia kuwa mawakala wa dola kuu kuliko kuwa mawakala wa mageuzi.  

Yaweza kujadiliwa kuwa Trump anazitumia rasilimali za ulimwengu wa Kiislamu kupanga kuvuruga kwake mfumo wa kiliberali. Kujiondoa kwa Amerika kutokana na makubaliano ya kinuklia ya Iran na shinikizo la Trump juu ya Saudi Arabia kuzalisha mafuta zaidi ili kufidia mafuta ya Iran yaliyopotea kunatilia nguvu usahali ambao Amerika inaweza kuzitumia rasilimali za Waislamu ili kuzishinikiza dola kuu katika kubadili miondoko yao. Muungano wa Ulaya na Urusi hazina nguvu ya kuisaidia Iran, huku udhibiti juu ya Iran wa uuzaji mafuta ukipandisha bei za mafuta, ambapo inaudhuru uchumi wa China ulio na njaa ya mafuta.

Kwa muda mrefu sana ulimwengu wa Kiislamu umekuwa ni chombo cha dola za kigeni. Una uwezo mkubwa sana wa kuungana na kuwa dola moja na kutekeleza uhuru wake kamili. Dola kama hiyo itamvuruga mwenye kuvuruga na kuufinika mfumo mpito wa kiulimwengu. Je, yupo shujaa yeyote kamili wa kuinyakua fursa hii, kuupindua mfumo wa kiulimwengu ulioko leo na kuufanya ulimwengu wa Kiislamu kuwa dola ya hali halisi duniani?     

﴿قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَى مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَنْ تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ

“Sema, "Enyi watu, fanyeni muyawezayo, hakika mimi nafanya. Na mutakuja kujua ni nani atakaye kuwa na makaazi mema mwishoni. Hakika madhalimu hawatafanikiwa.”

[Al-An’am:135]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:36

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu