Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali Mpya Nchini Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Taliban hivi karibuni imetangaza serikali mpya ya mpito baada ya mabatilisho na ucheleweshaji wa mara kadhaa. Dunia imekuwa ikiiangalia Afghanistan kwa karibu zaidi tokea Taliban wauondoe utawala ulioungwa mkono na Amerika jijini Kabul. Taliban imekuwa ikifanya mikutano na mataifa ya kieneo na viongozi wa idara za kijasusi. Kwa kutekwa mkoa wa Panjshir na kushindwa kwa Natinal Resistance Front (NRF), Taliban hatimaye imejihakikishia kutangaza serikali yake mpya ya mpito.

Walinzi wa zamani wa Taliban wameihodhi serikali mpya licha ya ahadi ya kuweka serikali shirikishi. Kati ya wahusika 33 waliotangazwa, 14 ni maafisa wa zamani wa Taliban wa wakati wa utawala uliopita 1996-2001, watano ni wafungwa wa zamani wa Guantanamo na waliobaki 12 ni maafisa kutoka kizazi cha pili cha harakati hiyo. Baraza lote la wanaume litaongozwa na Mullah Muhammad Hassan Akhund, mmoja ya waasisi wa harakati na naibu Waziri Mkuu na waziri wa mambo ya nje wa wakati wa kipindi cha miaka mitano ya kujinyima ya Taliban ilipokuwa ikitawala. Akhund yupo kwenye vikwazo vya UN kutokana na jukumu lake katika kipindi hicho. Sirajuddin Haqqani, aliye katika orodha ya wanaosakwa na FBI ataongoza wizara ya mambo ya ndani. Mtandao wa Haqqani ulikuwa nyuma ya baadhi ya mashambulizi mabaya zaidi dhidi ya Amerika na vikosi vya washirika wakati wa vita vya miaka 20.

Mtoto wa muasisi wa Taliban Mullah Omar, aitwaye Mullah Yaquub, atakuwa waziri wa ulinzi, na waziri wa mambo ya kigeni atakuwa Amir Khan Muttaqi ambaye ni kiongozi wa ngazi ya juu. Mullah Abdul Ghani Baradar, mmoja wa washiriki waazilishi, atakuwa mmoja ya wasaidizi wawili wa Waziri Mkuu. Baradar mwanzoni alikuwa kiongozi wa afisi ya kisiasa ya Taliban, iliyopo Doha na alisimamia utiaji saini wa mkataba wa amani na Amerika mwaka jana. Baradar alitolewa gerezani mnamo 2018, baada ya kutumikia kwa miaka minane, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kufanikisha Mchakato wa Amani. Mnamo 2020, Baradar akawa kiongozi wa mwanzo wa Taliban kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na raisi wa Amerika baada ya kuwa na mawasiliano na Donald Trump.

Taliban inajikuta ikikabiliana na changamoto nyingi hivi sasa inapounda serikali. Wanahitaji kuvuka kutoka katika harakati ya msituni kuelekea kwenye serikali. Taliban inahitajia hivi sasa kutoa huduma za serikali, kuhudumia miundo mbinu na kuzalisha uwekezaji wa umma kusaidia ukuaji katika uchumi wa Afghanistan unaotegemea misaada kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa ripoti ya Februari ya 2021 iliotolewa na Kundi la Uchunguzi la Afghan la serikali ya Amerika, kiwango cha umasikini nchini Afghanistan hivi sasa kinakisiwa kuwa ni zaidi ya asilimia 72, kutoka asilimia 55 mwaka 2017.

Taliban itahitaji msaada wa maafisa wa utawala wa zamani, angalau kwa viwango vya chini, kuhakikisha uendeshaji mzuri wa usimamizi wa mambo ya kila siku. Hili bado halijatekelezwa licha ya mkono mrefu wa Taliban. Maafisa waliotumikia utawala wa Ghani wametakiwa kurejea Afghanistan na Waziri Mkuu Akhund wa Taliban akiahidi “itahakikisha usalama na amani yao.” Pia shirika la Amnesty limeahidiwa (usalama) kwa kila aliyefanya kazi pamoja na Amerika na idara zilizopita zilizoungwa mkono na Amerika baada ya uvamizi wa 2001.

Taliban imeelezea hamu yake ya kutambuliwa kimataifa na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia ikielezea kuwa wanataka “mahusiano imara na mazuri pamoja na majirani zetu na nchi nyengine zote yakizingatia kuheshimiana na maingiliano” wakiongezea kuwa wataheshimu sheria na mikataba ya kimataifa “ambazo hazigongani na sheria za Kiislamu na maadili ya kitaifa ya nchi .”[4] Jamii ya kimataifa, kwa upande mwengine, maingiliano baina yao yamekuwa ya polepole. Taliban imeiweka China kuwa ni mshirika muhimu katika eneo. Kwa kuzingatia haya, China imetangaza kutoa dolari milioni 31 za misaada ya dharura inayojumuisha nafaka, mahitaji ya kipindi cha baridi pamoja na dozi milioni tatu za chanjo ya Covid-19.

Hakukuwa na taarifa zinazohusiana na sera na vipaumbele vya serikali mpya ya mpito hasa ikizingatiwa ukweli kuwa nchi hiyo inategemea misaada ya kigeni. Licha ya kutangaza serikali yake mpya, Taliban inakabiliwa na changamoto lukuki.

أفغانستان#          #Afganistan            #Afghanistan

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu