Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ukamataji Mkubwa wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir Nchini Urusi na Uzbekistan – ndani ya muundo wa ushirikiano wa Wanachama wa SCO

(Imetafsiriwa)

Mnamo asubuhi ya Septemba 15 wakati wa kile kiitwacho “operesheni maalum”, kwa uchache Waislamu 18 waliwekwa kizuizini na FSB na Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Moscow na jimbo la Moscow. Haya yameripotiwa na Kituo cha Kumbukumbu cha Haki za Binaadamu kwa marejeo ya mwanaharakati maarufu wa haki za binaadamu Bakhrom Khamroev.

Kwa mujibu wa jamaa za waliowekwa kizuizini, harakati za uchunguzi zilianza mnamo saa 11 asubuhi katika wilaya tatu za jimbo la Moscow kwa wakati mmoja. Wakati wa upekuzi, vikosi vya usalama vilijaribu kuona kama watu wale wana matoleo ya Hizb ut Tahrir, simu zilizoporwa na vyombo vya habari vya kielektroniki, pamoja na machapisho ya thaqafa ya Kiislamu, ikiwemo Quran. Takriban wote waliowekwa kizuizini ni Wauzbek, na mmoja kati yao ni raia wa Urusi.

Mnamo Septemba 16, Kurugenzi Kuu ya Kupambana na Ugaidi na Msimamo Mkali ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uzbekistan imeripoti juu ya “kuzima shughuli za tawi la wanawake la shirika la kimataifa la kigaidi la Hizb ut Tahrir” katika mji mkuu wa Uzbekistan. Waislamu wa kike 29 katika Tashkent na jimbo la Tashkent waliwekwa kizuizini. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, “walikuwa wakijihusisha kikamilifu katika kukuza fikra za harakati yenye msimamo mkali “Hizb ut Tahrir” na kuwasajili wafuasi. Nyenzo zenye umbile la msimamo mkali zilionekana katika nyumba na katika simu za mkononi za waliowekwa kizuizini.” Kisha ikaripotiwa kuwa watu 10 waliwekwa kizuizini katika wilaya ya Almazar ya Tashkent, wakishukiwa kushiriki katika harakati za Hizb ut Tahrir. Na mnamo Septemba 17, idara ya habari ya Kurugenzi Kuu ya Mambo ya Ndani ya mji mkuu wa Uzbekistan ilitangaza juu ya kuwekwa kizuizini watu 12 zaidi wanaoshukiwa kushiriki katika harakati za Hizb ut Tahrir. Walituhumiwa kuwa na mahusiano na bloga maarufu mwenyeji wa Kyrgystan, Mahmudjon Kholdarov. Nchini Uzbekistan, zaidi ya watu 50 walizuiliwa kwa makosa ya kushiriki katika harakati za Hizb ut Tahrir katika kipindi cha siku mbili, 29 kati yao ni wanawake.

Wakati huo huo, Septemba 17 katika mji wa Dushanbe nchini Tajikistan kulifanyika mkutano wa Baraza la Wakuu wa Mataifa ya nchi wanachama wa SCO ukiongozwa na Emomali Rahmon. Raisi wa shirikisho la Urusi V.V. Putin alishiriki kupitia njia ya video.

Ni wazi kuwa ukamataji huu jijini Moscow na Tashkent “ulipangiliwa muda wake” sambamba na mkutano wa SCO uliofanyika Septemba 17, 2021. Mada kuu ya mikutano ya SCO muda wote imekuwa ni ju ya kile kiitwacho “vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali”. Na baada ya Taliban kushika madaraka Afghanistan, Urusi imeihofisha Tajikistan dhidi ya Taliban na imeanza kuunda vikosi vyake katika kambi zake za kijeshi: Kitengo cha 201 Motorized Rifle Division, kimewekwa katika nchi hii, kuimarisha uwepo wake katika nchi za Asia, ikipatiliza fursa ya kujiondoa kwa Amerika kutoka Afghanistan na kudhoofisha nafasi yake. Hivyo, kwa mara nyengine Waislamu wamekuwa wahanga katika mapambano ya dola za kibeberu ya kung'ang'ania ushawishi katika nchi zilizokoloniwa za Waislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran:

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ]

“Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji” [Al-Baqara 2:11].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shaikhetdin Abdullah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu