Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Marekani Yausukuma Ushawishi wa Urusi nje ya Armenia

(Imetafsiriwa)

Nancy Pelosi anazuru Armenia kuhusiana na kuadhimisha mapatano ya Azerbaijan, kituo cha televisheni cha Qatari cha Al Jazeera kinaripoti.

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amewasili Armenia, ambako usitishaji mapigano unashuhudiwa kufuatia kuzuka kwa uhasama na taifa jirani la Azerbaijan na kusababisha mamia ya wanajeshi kuuawa kwa pande zote mbili.

Ubalozi wa Marekani ulisema kuwa ziara ya Pelosi itajumuisha mkutano na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan. Siku ya Ijumaa, Pelosi aliwaambia waandishi wa habari jijini Berlin kwamba safari hiyo "ni kuhusu haki za binadamu na heshima kwa utu na thamani ya kila binadamu."

Spika wa Armenia Alen Simonyan aliwaambia waandishi wa habari kwamba ziara ya siku tatu ya Pelosi "itacheza dori kubwa katika kuhakikisha usalama wetu."

Kituo hicho cha Televisheni kilitoa kumbukumbu ya vita viwili vya Armenia na Azerbaijan vya 1990 na 2020, na vile vile mapigano makali ya mwisho ambayo yalimalizika usiku wa kuamkia kuwasili kwa Pelosi huko Yerevan. Armenia imeishutumu Azerbaijan kwa uchokozi usio na msingi, lakini maafisa wa Baku wamesema jeshi lao linajibu mashambulizi ya Armenia.

Pashinyan alisema kuwa takriban wanajeshi 135 wa Armenia waliuawa katika mapigano hayo, huku Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan ikisema kuwa imepoteza watu 77. Mapigano hayo, ambayo yamesababisha vifo vya wanajeshi zaidi ya 200 kwa pande zote mbili, yalimalizika siku ya Alhamisi kwa upatanishi wa "jumuiya ya kimataifa", maafisa wa Yerevan walisema.

Urusi ilichukua jukumu la kusitisha mapigano. Rais wa Urusi Vladimir Putin aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa kwamba mapigano ya hivi karibuni yamekuwa "ya kienyeji" chini ya "ushawishi" wa Moscow.

Hata hivyo, Marekani inapinga madai ya Urusi. Afisa mmoja wa Marekani aliliambia shirika la habari la Reuters wakati wa usitishaji mapigano kwamba Washington "haioni dalili kwamba juhudi za Urusi zimetoa mchango chanya katika kufanikisha usitishaji mapigano wa hivi majuzi zaidi."

Simonyan, spika wa bunge la Armenia, alielezea kutoridhishwa wiki iliyopita na jibu la muungano wa kijeshi unaoongozwa na Urusi kwa ombi la msaada la Yerevan, shirika la habari la Interfax liliripoti. Armenia imeomba Jumuiya ya Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO) inayoongozwa na Moscow kuingilia kati, lakini hadi sasa imetuma timu ya kutafuta ukweli katika eneo hilo.

“Bila shaka hatuna furaha sana. Matarajio tuliyokuwa nayo hayakuwa halali,” Simonyan aliiambia televisheni ya taifa, akilinganisha CSTO na bastola ambayo hairushi risasi, inaripoti Interfax. Akibainisha kuwa Armenia pia ina makubaliano ya usaidizi wa pande zote na Urusi, alisema kuwa "tunatarajia hatua za mashiko zaidi kutoka kwa washirika wetu wa Urusi, na sio tu taarifa au maneno nusu."

Ziara ya Nancy Pelosi nchini Armenia, dhidi ya hali ya mazingira ya kukola kwa hivi punde kwa mzozo wa Armenia na Azerbaijan, inaweza kuzingatiwa kama mukhtasari wa matokeo ya katikati ya Vita vya Pili vya Karabakh. Mnamo Septemba-Novemba 2020, wakati wa mzozo mkubwa wa siku 44 wa kisilaha, Azerbaijan iliweza kupata tena udhibiti wa maeneo mengi yaliyopotea mwaka wa 1994. Hii iliwezekana kutokana na uungaji mkono wa kisiasa na kijeshi wa Azerbaijan kutoka Uturuki.

Matokeo ya vita hivyo yalikuwa mabadiliko katika hali ya mambo katika eneo hilo, iliyojaa mizozo isiyoweza kusuluhishwa kati ya Armenia na Azerbaijan, isiyopendelea Urusi.

Kushindwa kwa haraka na karibu kabisa kwa wanamgambo wa Armenia waliojitangaza NKR na jeshi la Azerbaijan kulionyesha wazi kupotea kwa ushawishi wa zamani wa Urusi juu ya jamhuri hizi mbili za baada ya Usovieti za Transcaucasia, ambao ulihifadhiwa kutokana na ushindi wa Armenia katika vita vya kwanza vya Karabakh vya 1992-1994.

Licha ya ukweli kwamba mnamo Novemba 2020 Urusi ilifanya kazi kama mpatanishi na hata ikatuma askari 2,000 wa "kulinda amani" katika sehemu ya Nagorno-Karabakh ambayo ilibaki chini ya udhibiti wa Armenia, bado haikuwa na ushawishi wowote juu ya mwendo na mwisho wa vita hivyo. Katika kujibu wito kutoka kwa Waarmenia wa kuwaunga mkono ndani ya mfumo wa CSTO, ilihalalisha kutochukua hatua kwa kusema kwamba Nagorno-Karabakh, ambako uhasama ulifanyika, ni eneo linalotambulika kimataifa la Azerbaijan.

Pia, kushindwa kwa mamlaka za NKR na Armenia kushawishi hali hiyo hakuwezi kuhusishwa na sababu halisi za kumaliza vita vya pili vya Karabakh.

Udhaifu na kutokuwa na uwezo kwa Waarmenia vilikuwa dhahiri, ikijumuisha upande wa Azerbaijan, ambayo inaweza, kupatiliza fursa hiyo, hatimaye kutatua tatizo la Nagorno-Karabakh na maeneo mengine yaliyochukuliwa. Kwa mujibu wa Rais wa NKR Arayik Harutyunyan, "kama uhasama ungeendelea, Artakh yote ingepotea ndani ya siku chache, kungekuweko na waathiriwa zaidi."

Kwa uwazi, uamuzi wa kumaliza vita ulilazimishwa juu ya Baku kutoka nje, ambayo ni kutoka Uturuki, ambayo msaada wake wa kijeshi na kiufundi ulilipa jeshi la Azerbaijan faida isiyo na masharti kwenye uwanja wa vita. Kwa kuzingatia dori ya serikali ya sasa ya Uturuki kama kibaraka wa Amerika, inaeleweka pia kuwa mapatano haya yanaendana na maslahi na mipango ya Amerika hatimaye kuiondoa Urusi kutoka Transcaucasia na kuliweka kikamilifu eneo hilo chini ya ushawishi wake.

Ukweli kwamba, licha ya mafanikio ya kijeshi ya muungano wa Kituruki-Azerbaijan, makubaliano ya kusitisha vita yalihitimishwa, kwa uhifadhi wa uvamizi wa Waarmenia wa sehemu ya Nagorno-Karabakh, kwa maslahi kamili ya Amerika. Kuendelea kwa mzozo ambao haujatatuliwa huruhusu Marekani, endapo kuna haja, kutumia shinikizo kwa pande zote. Kwa kuongezea, lengo la Amerika halikuwa uharibifu wa Armenia, lakini ni onyesho tu la uongozi na uwezo wake usio na shaka, dhidi ya mazingira ya udhaifu wa Urusi na EU, uliofungika kwa wito wa suluhu ya kisiasa na kidiplomasia. kuvunja upinzani wa serikali yake tawala. Na, inaonekana, Yerevan ilijifunza somo hili, akipendelea kuwa upande wa wenye nguvu.

Baada ya mapumziko ya takriban miaka miwili baada ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Karabakh, Marekani inaanza kumakinisha matokeo yake kisiasa kwa niaba yake. Ziara ya wajumbe wa Marekani wa ngazi ya juu kama hii inakusudiwa kuonyesha kwa Armenia uzito wa nia na kiwango cha juu cha maslahi ya Marekani katika kuanzisha mahusiano ya kina na ya karibu. Na ziara ya Pelosi kwenye jumba la kumbukumbu la Tsitsernakaberd inatumika kama onyesho la uaminifu na ukaribu. Uwepo wa mkuu wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Biashara katika ujumbe huo unaonyesha utayari wa Amerika kuiondoa Armenia kutoka kwa utegemezi wa nishati kwa Urusi na vizuizi vya kiuchumi na nchi jirani.

Inaonekana kwamba Amerika inakusudia kutoa ushirikiano kwa Armenia sawa kama ule wa Amerika na "Israeli". Yaani, pamoja na usaidizi wa kisiasa na kiuchumi, pia wako tayari kutoa msaada wa kijeshi na kiufundi. Hivi ndivyo unavyoweza kuitazama kauli ya mwenyekiti wa Bunge la Armenia, Alen Simonyan, kwamba ziara ya siku tatu ya Pelosi "itacheza dori kubwa katika kuhakikisha usalama wetu."

Licha ya mikutano ya hadhara ya kupinga Urusi katikati mwa Yerevan, iliyofanyika chini ya bendera za Marekani usiku wa kuamkia ziara ya Pelosi, pamoja na ukweli kwamba alikutana na kuandamana na spika wa bunge la Armenia Alen Simonyan, Amerika bado haijaimarisha kikamilifu duara zake za kisiasa nchini Armenia. Kwa hiyo, Pelosi, akiwa bado Berlin, alitangaza kwamba safari yake ilikuwa "imejitolea kabisa kwa haki za binadamu," ambayo inaashiria nia ya Marekani, chini ya mwamvuli wa vyama vingi vya kisiasa, kulinda watu watiifu kwao nchini Armenia kutokana na shinikizo kutoka kwa koo zinazounga mkono Urusi pamoja na wanaliberali wanaounga mkono Ulaya.

Kwa kuongezea, Amerika inafanya kazi ili kuimarisha ushawishi wake juu ya Mujtamaa wa Armenia, ikijiweka sio tu kama rafiki na mshirika, lakini pia kama mlinzi. Hii inathibitishwa na kuongezeka kwa mzozo hivi karibuni kwenye mpaka wa Armenia na Azerbaijan, katika hali ambayo Pelosi alichukua upande wa Armenia, akiweka jukumu lote kwa Baku. Na hii, pamoja na ukweli kwamba, kama Reuters inavyosema, "kulaumiwa huko kwa mzozo kwa moja ya pande husika ni mbali na msimamo wa dhahiri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika, ambayo hapo awali ilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, lakini haikuwataja waliohusika na kuongezeka kwa mzozo huo."

Wakati huo huo, wawakilishi wa mamlaka za Urusi, wakihalalisha kupuuza maombi ya Waarmenia ya usaidizi kwa kutofautiana na desturi na kanuni za CSTO, wanawatuhumu kwa kuanzisha nia za uchochezi na fujo. Kwa hivyo, kulingana na mtaalamu wa kijeshi wa Urusi Igor Korotchenko: “Nikol Pashinyan na duara lake la ndani walichagua njia ya upambaji moto wa kisiasa. Ni dhahiri kwamba kuongezeka kwa masuala haya yote kunahusishwa na ujio ujao wa Nancy Pelosi huko Yerevan ili kucheza pamoja na Washington na kuashiria upendeleo dhidi ya Urusi katika sera ya sasa ya Yerevan.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mustafa Amin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu