Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuporomoka kwa Lazima Kulikokaribia

(Imetafsiriwa)

Mfalme Abdullah II wa Jordan hivi majuzi alitembelea Ikulu ya White House kupokea maelekezo kuhusu dori yake katika mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza. Biden alikuwa makini kuushirikisha utawala wa Jordan katika mipango yake ya kusuluhisha usitishaji vita kati ya umbile la Kizayuni na Hamas. Amejitolea kufikia makubaliano. "Mambo muhimu ya mpango huo yapo mezani," Biden alisema pamoja na mfalme, ingawa "kuna mapungufu yanayosalia." Alisema Marekani itafanya "kila linalowezekana" kuyafanya makubaliano yafanyike ikiwa ni pamoja na kusitisha mapigano kwa angalau wiki sita na kuachiliwa kwa mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas. Vile vile alisisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Palestina katika kuchukua majukumu huko Gaza endapo Hamas haipo tena madarakani, na kusema, "lazima wajiandae kujenga dola inayokubali amani, isiyohifadhi makundi ya kigaidi kama Hamas na Jihad ya Kiislamu. ”

Hii ilifuatia raundi ya mikutano pamoja na wanasiasa wa Marekani akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken, Waziri wa Ulinzi Austin, na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa, ambao wamekuwa wageni wa mara kwa mara katika Mashariki ya Kati, na kusisitiza uungaji mkono wao mkubwa wa kijeshi kwa umbile la Kizayuni. Ziara hizi pia zilitoa shinikizo la kisiasa kwa viongozi wa mrengo wa kulia katika serikali ya Netanyahu kuafikiana na malengo ya Marekani ya suluhisho la dola mbili.

Kupuuza huku kwa wazi kwa Marekani kwa Ummah ni jambo ambalo halifichiki tena. Imeianika wazi Marekani mbele ya ulimwengu. Kiburi na uchokozi usio na kifani unaoonyeshwa katika kuunga mkono ugaidi na mauaji ya halaiki huku wakidai kuwezesha mazungumzo ya amani ni unafiki ambao ulimwengu unashuhudia na kuona. Misimamo hii inaweka shinikizo kubwa kwa vibaraka wanaoning'inia katika guo la Magharibi.

Suala sio tena kwamba utawala wa Jordan unashiriki katika mapambano ya kubakia hai kwake, ambayo ni dhahiri katika ushirikiano wake na Marekani na Uingereza na mikutano yao ya mara kwa mara. Hii inasisitiza hofu yao na kuyumba kwa tawala zao. Utawala wa Jordan unaamini kimakosa kwamba ushirikiano wake na umbile la Kizayuni na nchi za Magharibi unaweza kuzuia kuanguka kwake kunakokaribia.

Ummah mzima unalaani misimamo mibaya inayochukuliwa na Marekani na kutochukua hatua kwa utawala wa Jordan. Unatafuta kutoroka kutoka kwa viongozi wao na mfumo mbovu wa kilimwengu. Mabadiliko ya kweli yanaweza kupatikana tu kupitia kuanguka kwa vibaraka na vyombo vya kisiasa vya Magharibi na kukumbatia kwa kina mfumo wa Kiislamu, kupitia kusimamishwa tena kwa Khilafah ambayo itaweka ukombozi wa Palestina kama kipaumbele na kusambaratisha mtandao wa vibaraka na serikali zinazokalia ulimwengu wa Kiislamu.

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-'Ankabut: 41]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb utTahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu