Jumanne, 01 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Barakoa Zimepomoka: Miaka 76 ya Ukaliaji Kimabavu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Jarida la ‘Economist’ liliripoti mnamo Mei 14, 2024 kwamba, “Uwashaji wa mwenge ambao kwa kawaida hufungua Siku ya Uhuru wa "Israel" ulitangazwa mnamo jioni ya Mei 13 kama kawaida. Lakini badala ya kuonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni kama kawaida, hafla hiyo ilirekodiwa mapema. Serikali ilisema hii ni kwa sababu ya hali tete ya kufanya sherehe hiyo wakati taifa liko vitani. Sababu halisi, hata hivyo, ilikuwa hofu ya wanasiasa kwamba ingevurugwa na waandamanaji, waliokasirishwa na kufeli kwao katika kushughulikia vita.”

Ingawa umbile la Kiyahudi liko katika msukosuko wa ndani leo, uanzishwaji wake wa asili ni utengezaji ambao ulidunga moyo wa Ulimwengu wa Kiislamu. Damu ilimwagika katika nchi takatifu kama ilivyokuwa wakati wa vita vya msalaba vya karne ya 11. Kuzaliwa kwake kuliwezekana tu kwa kufukuzwa kwa lazima kwa watu ambao walikuwa tayari wanaishi huko na usaliti wa watawala wa Kiarabu katika eneo hilo. Waislamu na Wakristo ambao walikuwa wameishi huko kwa karne nyingi walifukuzwa na magenge ya kigaidi ya Kizayuni, katika kile kinachojulikana kama Nakba, janga. Waislamu na Wakristo walifukuzwa katika nyumba zao, vijiji vilichomwa moto, na wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia walichinjwa na walowezi wa Kizayuni, waliokuja kutoka Ulaya kudai ardhi hiyo kuwa ni yao. Maelfu ya Mayahudi kutoka duniani kote walipewa ardhi ambayo ni mali ya wengine. Palestina ikawa mahali pa ukaliwaji kimabavu. Wapalestina waliolazimishwa kuondoka hawajawahi kuruhusiwa kuregea.

Barakoa ya uvamizi wa kikatili wa Wazayuni, unaoungwa mkono na Marekani, imepomoka. Marekani iliwapa nguvu Wazayuni na kufumbia macho yote waliyoyafanya. Marekani ilitumia uwezo wake wa kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa kuwakinga Wazayuni dhidi ya vikwazo vyovyote au adhabu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Kwa muda wa miaka 76, Wazayuni wameendelea kunyakua ardhi na kueneza ugaidi, wakifanya mamia ya vizuizi na kuzuia maisha ya utulivu kwa Wapalestina. Miaka sabiini na sita baadaye, mabadiliko pekee katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni teknolojia ya hali ya juu yenye kulipua nyumba, shule na hospitali. Uhalifu usioelezeka, kama vile makaburi ya halaiki yaliyofichuliwa kwenye misingi ya hospitali baada ya wiki kadhaa za uvamizi wa Wazayuni. Kuhama kwa lazima, njaa ya kulazimishwa, na kuporomoka kabisa kwa miundo ya jamii inayofanya kazi kumesababisha hali ya kutisha zaidi huko Gaza. Kwa muda wa miezi saba, tumeona mauaji ya halaiki yakitokea mbele ya macho yetu. Inatupa taswira ya ukandamizaji wa Wapalestina katika kipindi cha miaka 76 iliyopita.

Sura mbaya, isiyofichika ya uvamizi huo wa kikatili sasa imeuamsha Ummah. Uvamizi wa hapo awali wa jeshi la Kizayuni huko Gaza ulikuwa habari za muda mfupi. Lakini wakati huu, ni tofauti. Safari hii Waislamu wameamka. Kutoka Morocco hadi Malaysia, Umma wa Kiislamu unahamasishwa na kusonga mbele. Nguzo za kirongo za Magharibi zimeanguka. Waislamu hawana matumaini katika suluhisho la Magharibi kwa Palestina. Unafiki unadhihirika. Mikono iliyolowa damu ya Marekani na dola za Ulaya haiwezi kufichwa.

Barakoa za taasisi za wakoloni wa Magharibi zimepomoka. Umoja wa Mataifa, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) hutumikia maslahi ya Marekani. Umoja wa Mataifa, ulioundwa na Marekani mwaka 1945, ulionyeshwa kama chombo kisichoegemea upande wowote kilichoundwa kulinda watu wote na kuzuia vita vyote. ‘Never again’ ndiyo iliyokuwa kauli mbiu. Ilidaiwa kuwa kamwe hataruhusiwa tena mtu yeyote kuwaua watu wengi kutokana na kabila au dini. Lakini ilikuwa ni Umoja wa Mataifa uliokuwa skrini ambayo nyuma yake kulikuwa na mpango wa kuwaibia Ummah wa Kiislamu Qibla chao cha kwanza. Mpango ambao ulibuniwa kumpumbaza mtu wa kawaida kufikiri kwamba ni suala la muda tu kabla ya amani kupatikana na Waislamu, Wakristo, na Mayahudi wataishi bega kwa bega. Wahusika wa tamthilia hii tata walikuwa ni wale walioitwa wapenda amani wa Magharibi ambao wangeleta pande tofauti pamoja. Wachezaji wa pembeni walikuwa ni watawala wa Waislamu walioamriwa kujilinda kama vibaraka viziwi na mabubu, kusema tu wanapozungumzishwa na kusema tu kile ambacho maandishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliwaambia waseme.

Maazimio na makubaliano mengi ya Umoja wa Mataifa yametiwa saini kuhusu ukiukaji wa sheria za Kimataifa wa dola ya Kizayuni huko Palestina. Bado wameshindwa kusuluhisha uvamizi na ukandamizaji mkali wanaopitia Waislamu wa Palestina. Badala yake, wamezidisha hali na hali ya wale wanaoishi katika Ardhi hii Iliyobarikiwa. Wamerefusha muda wa uvamizi. Maazimio yasiyo na maana yaliyopendekezwa na Umoja wa Mataifa kulaani kitendo cha kikatili cha "Israel" yalikataliwa na Marekani, kupitia kura yake ya turufu. Yale yaliyopitishwa yalivunjwa na Wazayuni, bila matokeo yoyote. Kwa hivyo, barakoa ya UN imepomoka. Iliundwa na Marekani kutumikia maslahi yake.

Kadhia ya Palestina kamwe haiwezi kutatuliwa na shirika la makafiri kama UN au makafiri waliovalia suti na tai zao wakiwa wanaonyesha tabasamu za uongo. Hakuwezi kuwa na binadamu mwenye akili timamu ambaye bado angetetea kukabidhi kadhia hii kwa Umoja wa Mataifa kutafuta suluhu. Zaidi ya hayo, Qur’an Tukufu ilituonya miaka 1400 iliyopita ili tujue ni nani alikuwa adui yetu na tusidanganywe nao. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلْكَـٰفِرِينَ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا۟ لِلَّهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَـٰنًۭا مُّبِينًا]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?” [Surah An-Nisa 4: 144].

Barakoa za watawala wa Waislamu zimepomoka. Wanaendelea kukataa kutuma majeshi ya Waislamu kukomesha mauaji ya halaiki nchini Palestina. Erdogan anaendelea kusambaza silaha, vifaa, na chakula kinachohitajika kuendeleza mauaji ya halaiki. Misri, chini ya dikteta katili Al-Sisi, inafunga Kivuko cha Mpakani cha Rafah. Abdallah wa Jordan anatoa daraja la anga, pamoja na ukanda wa ardhini pamoja na Saudia na Imarati, ili kusafirisha vifaa vya kijeshi vya Marekani kwa Wazayuni. Watawala wa Waislamu wanaoizunguka Palestina ni watetezi wa Wazayuni pekee. Wamewafunga na kuwatesa walioandamana kupinga mauaji ya halaiki. Viongozi wote 57 wa nchi za Waislamu wanashiriki katika mauaji ya halaiki kupitia kukataa kwao kupeleka majeshi. Wana uwezo zaidi wa kuwaponda Wazayuni, lakini wanachagua kuwatumikia mabwana zao. Ni kana kwamba hawakusikia maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

«مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ»

“Hakuna (Muislamu) mtu yeyote atakayemtelekeza Muislamu katika sehemu ambayo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika sehemu ambayo angependa nusra Yake. Hakuna (Muislamu) mtu yeyote atakayemnusuru Muislamu katika sehemu ambayo heshima yake inavunjwa utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru katika sehemu ambayo angependa nusra Yake.” [Abu Daud]

Kabla ya watawala wa sasa, kwa miaka 1300, Khilafah ilikuwa imeilinda na kuihami Ardhi Iliyobarikiwa. Khilafah ya Umar al-Farooq (ra) iliifungua Palestina kwa Uislamu. Khilafah ilituma vikosi vya Salahudin kwenda kuikomboa kutoka kwa makruseda. Khilafah ya Abdul Hamid II iliilinda Palestina kutokana na majaribio ya Wazayuni ya kupora ardhi yake. Kwa kukosekana Khilafah, Palestina imebakia chini ya uvamizi.

Barakoa zote zimepomoka. Viongozi wa Magharibi na mfumo wao batili wa maisha wamefichuliwa. Taasisi na mahakama zao zimefichuliwa. Khiyana ya watawala wa Waislamu umefichuliwa. Washawishi na watu mashuhuri wamefichuliwa. Waliokaa kimya wamefichuliwa. Hatuwezi kuwa na tumaini lolote kwa yeyote kati yao. Kufanya hivyo itakuwa ni kukataa uhalisia. Mujahidina wa kweli wametimiza ahadi yao na Mwenyezi Mungu (swt). Wanaume, wanawake, watoto wadogo na wachanga ambao hawajazaliwa huko Gaza wametimiza ahadi yao na Mwenyezi Mungu (swt). Sisi tunafanya nini ndugu zangu na dada zangu? Mitandao ya kijamii na maandamano lazima yatumike kulingania suluhisho sahihi.

Palestina haitakombolewa kwa kujifunza kuhusu historia yake. Kususia, kutengwa na vikwazo havitaikomboa Palestina. Palestina haitakombolewa kwa msaada wa chakula. Palestina itakombolewa wakati wana shupavu wa Umma katika majeshi ya Waislamu watakapowaasi watawala wasaliti, wakavunja minyororo yao na kuandamana kuelekea Al Quds. Suluhisho la Palestina ni kupeleka majeshi yetu ya Waislamu Aqsa. Suluhisho la Palestina ni kwa maafisa shupavu wa Ummah kuwang'oa watawala na kutoa Nusrah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida. Ni Khilafah ndiyo itakayoikomboa Palestina na Al Aqsa. Dori yetu ni kuyataka majeshi yaende kuulinda Ummah. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad 47:7].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Maryam Ansari

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu