Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ghasia za Kyrgyzstan dhidi ya Wanawake na Watoto kama Njia ya Kupigana na Misimamo Mikali ni Zenye Kuendekezwa katika Ulimwengu wa Kisekula wa Kidemokrasia

Sio siri kuwa serikali ya Kyrgyz inafanya mengi dhidi ya Uislamu. Bali inajulikana kwa urafiki wake na Urusi na Putin, na uadui wake kwa Uislamu na Waislamu. Kwa hili ilitabanni Kifungu cha 299-2 katika Sheria ya Jinai mnamo 2010, kinacho kataza umilikaji wa nyenzo zenye misimamo mikali kwa mujibu wa kiigizo cha sheria ya Urusi ya kupambana na misimamo mikali. Ili kuwapa sura nzuri watawala na mamlaka za Kyrgyz, ufafanuzi wa nyenzo zenye misimamo mikali uliwekwa kwa njia ya kiholela na kuweza kufanyiwa mabadiliko kwa mujibu wa mtazamo wa maafisa wa uchunguzi, mwanasheria, na Kitengo cha Dola kinacho shughulikia Maswala ya Kidini, na hivyo hutofautiana katika kesi ya mtu kwa mtu. Mamlaka kwa kawaida huorodhesha nyenzo kuwa ni zenye misimamo mikali baada ya kufanya ukamataji. Hivyo ni jambo la kawaida mno nchini Kyrgyzstan kuwa mawakala wa usalama hupanga urongo au hata kupandikiza nyenzo wakati wa misako, na kisha kuitisha milungula ili kumaliza uchunguzi. Tangu 2013, marekebisho ya kifungu cha 299-2 yametia hatiani umiliki wa nyenzo zinazo dhaniwa kuwa zenye misimamo mikali hata kama mtuhumiwa hana nia ya kuzisambaza, na kukataa umilikaji wa hizo nyenzo zinazo semekana. Hivyo mamia ya Waislamu wasio na hatia wamehukumiwa kifungo cha kati ya miaka 3 hadi 10 gerezani kwa mashtaka ya kuzuliwa ya misimamo mikali na ghasia. Pia jambo la kawaida mno ni utesaji unaofanywa na maafisa wa utekelezaji sheria ili kulazimisha kuungama… (Kamati ya Umoja wa Mataifa Dhidi ya Mateso na Kituo cha Kitaifa cha Kyrgyzstan). Kwa mujibu wa HRW: "Katika kesi nyingi mamlaka nchini Kyrgyzstan zimekuwa zikitumia kifungu cha 299-2 ili kuwafunga gerezani washukiwa kwa tabia hata isiyo ya ghasia pia kama vile kumiliki fasihi au video marufuku au kutekeleza Uislamu asili." Rekodi za mahakama zilizo hakikiwa na HRW juu ya kesi za 299-2, vilevile stakabadhi za serikali, ripoti za vyombo vya habari, na machapisho ya mitandao ya kijamii kuhusu kesi kama hizo, yanafichua kwamba hakuna nyenzo yoyote katika hizo zilizo orodheshwa kama zenye misimamo mikali na dola zinajumuisha ghasia au uchochezi wa ghasia. Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, nyenzo nyingi zenye misimamo mikali zilizopatikana kwa watu walioshtakiwa chini ya Kifungu cha 299-2 ni hotuba na maandishi mengine kutoka kwa Hizb ut Tahrir, ambayo ni harakati isiyo ya vurugu inayotaka kusimamisha Khilafah kote katika ulimwengu wa Waislamu iliyojengwa juu ya sheria ya Kiislamu. Hizb ut Tahrir inakata hadharani juhudi za kufikia malengo yake kupitia njia za vurugu. (Ripoti yenye kurasa 78 ya Shirika la Human Rights Watch ya mnamo 2018: "Tunaishi kwa Hofu Siku Zote: Umilikaji wa Nyenzo Zenye Misimamo Mikali Nchini Kyrgyzstan)

Baada ya kuorodhesha hivi, ukamataji wa hivi karibuni wa watu wanane wasio na hatia, wanawake wa Kiislamu wasio na madhara yoyote nchini Kyrgyzstan haupaswi kufichika kwa ulimwengu! Wanawake hawa walikamatwa kwa sababu tu wao ni Waislamu. Wao pia wamesibiwa na mbinu hizo hizo za dola "zilizo kinyume na sheria" kama walivyosibiwa mamia kabla yao. Maafisa wa usalama waliwadhalilisha na kuwanyanyasa wakati wa msako, wakiwanyima haki ya kuvaa vazi lao la Kiislamu na hijab. Walipandikiza madaftari pamoja na nyenzo za tuhuma, ambazo si za yeyote katika wanawake hao waliokamatwa. Zaidi ya hayo walinyanyaswa, kuwekwa nje katika siku iliyokuwa na mvua na baridi kwa masaa kati ya 6 na 12 katika kipindi cha Covid-19, ikiathiri vibaya mfumo wao wa kinga mwilini na kuwaweka katika hatari ya maambukizi, na kuwanyima chochote cha kula. Matokeo ya hili, mmoja wa wanawake hao, Baktybek kyzy Mahabat (29), aliyekuwa na hali ya kiafya inayohitaji matibabu ya kila mara, alikuwa mgonjwa na alilazimika kupelekwa hospitali. Mwanamke huyu pia ana watoto wadogo wa chekechea wanaomtegemea mama yao. Hali hii vilevile ilikuwa kwa Meerim Ismailova, mama wa binti wanne, wenye umri wa miaka kati ya 6 hadi 12. Aliwekwa kifungo cha nyumbani, akitarajia kifungo gerezani wakati wowote. Siku ya kukamatwa Almagul Ajumudinova (51) alikuwa akimpa uangalizi mjukuu wake, aliye na maradhi ya kupooza ubongo. Matokeo ya kukamatwa kwake, msichana huyo, asiyeweza kuketi peke yake, alipata kifafa. Mmoja wa wanawake hao, Mamirkanova Amangul, alihojiwa kwa masaa mengi huku akimshughulikia mwanawe mwenye umri wa miaka minne aliyekuwa na maradhi ya 'Down Syndrome' na alikuwa amefanyiwa upasuaji wa moyo hivi majuzi. Arunova Erkingul (37) ambaye ni mchungaji wa babake mwenye umri wa miaka 90, na mamake mwenye umri wa miaka 80, aliyepata kiharusi hivi majuzi na yuko katika hali tete, hakuruhusiwa hata kuonana na yeyote katika familia yake tangu kukamatwa kwake.

Yeye na Baktybek kyzy Mahabat hata bado hawajafikishwa mahakamani na wanazuiliwa katika gerezani lililo na maambukizi ya korona. Archagul Ajumudinova (37) ni mama wa binti watatu na mtoto wa kiume mmoja, wenye umri wa 2, 6, 9 na 16. Meerim Kadyralieva (34) ni mama wa watoto wawili, wenye umri wa miaka 5 na 9. Na wapo wengine wenye hali sawa na hizi…

Hii bila shaka ikiwa ni pamoja na ghasia katika aina zake tofauti tofauti kwa wanawake hawa, watoto wao na wazazi wao wakongwe. Huu ni ugaidi wa dola kwa umbile lake dhahiri, unaoshajiishwa kupitia Umagharibi wenye misimamo mikali! Ghasia hizi zinazo fanywa na serikali ya Kyrgyz zinaendekezwa na ulimwengu wa kisekula wa kidemokrasia kama njia halali ya kupigana dhidi ya misimamo mikali!

Kwa hakika kunaibuka kazi na jukumu juu ya kila Muislamu kunyanyua utambuzi kuhusu ugaidi huu wa dola unaofanywa na serikali ya Kyrgyz. Kazi ya kwanza kabisa ya wale wanasiasa wote wa kike na wanaharakati katika ardhi za Waislamu kama Uturuki, hususan wanasiasa wa kike, mawaziri na wanaharakati wa AKP, wanaopigania kwa dhati haki za wanawake za kileo, na wanaoshikilia makubaliano na haki za kimataifa za wanawake kwa makucha na meno yao kwa kuhofia "kupoteza mapato yote ya kidemokrasia ya wanawake" kupaza sauti zao dhidi ya kitengo hiki cha ghasia!

Wapenda wanaharakati, wanasiasa na mawaziri wa kike katika ulimwengu wa Kiislamu, mnaodai kusimama kwa ajili ya haki za wanawake wa Kiislamu! Wanawake wachaMungu wa Kiislamu wa Kyrgyzstan sio wanasiasa wenye ushawishi, wala sio wanaharakati maarufu; wala sio wanawake wenye mapato ya kileo kama mlivyo nyinyi, bali uwepo wao tu pekee unaleta tishio kwa serikali hii katili ya kileo. Hawahitaji kunyosha kidole ili kuvutia makini ya sheria, bali sheria daima hufuata mkondo wake ili kuwafikia kwa ukali wake wote… Vipi basi bado ulimwengu haujajua kuhusu ghasia hizi dhidi ya wanawake wasio na madhara yoyote?!

Je, wakati haujawadia wa kuzitilia shaka nafsi zenu, nyadhifa zenu, na vyeo mlivyopewa katika nchi zenu za kidemokrasia mnazozipenda? Ikiwa walinzi wa mfumo huu, unaochukia Uislamu na Waislamu, wanawapigia makofi basi ni lazima mkubali kuwa mnasimama msimamo wa makosa! Ikiwa mnapokea sifa kutoka kwa mabunge ya kisekula ya kidemokrasia na vyombo vya habari, huku dada zenu wa Kiislamu wakinyimwa uhuru wao katika nchi za kidemokrasia kote duniani; na ikiwa vyombo vya habari vya kisekula vinazipa nguvu sauti zenu na maoni yenu kwa kupendelea mazungumzo ya Kimagharibi, huku vikichafua sura ya Uislamu, wanawake wake, vima na historia yake; na ikiwa Ulaya na Magharibi zinawapa usaidizi wa kifedha kwa ajili ya kutabikisha makubaliano na miradi ya kimataifa, huku dada zenu wakinyimwa nafasi ya kwenda katika shule za umma na sehemu za umma wakiwa wamevalia mavazi yao ya Kiislamu ni lazima basi mzitilie shaka fikra mnazozipigia debe! 

Wanawake hawa, wachaMungu, waheshimiwa wa Kiislamu, ambao hawainamii kitu chochote isipokuwa maamrisho ya Mola wao (swt), ambao hawasemi neno lolote dhidi ya radhi za Muumba wao, wasiokuwa na taarifa au tabia yoyote ovu, chafu, isiyo ya sawa, wamenyakuliwa kutoka kwa waume zao, watoto wao na wazazi wao huku nyinyi mkifurahia heshima ya makafiri, kihakika hii ni ishara kwamba NYINYI ndio mnaodhalilishwa! Badilisheni sasa!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

مسلمات_قرغيزستان#   

#KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük     

#FreeMuslimahsKyrgyzstan

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 30 Agosti 2020 15:26

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu