Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuangazia Muundo wa Uimla Eneo la Asia ya Kati kutokana na Kesi ya Kukamatwa Wanawake wa Kyrgyz

Kukamatwa kwa wanaharakati wa kike kadhaa wa Kiislamu nchini Kyrgyzstan chini ya pazia la misimamo mikali inaonekana kuwa ni mtindo wa zamani ulioundwa na watawala Waislamu wa Kyrgyz kwa mara nyengine tena, mithili ya madikteta wenzao nchini Uzbekistan na Kazakhstan.

Hakuna tofauti na serikali na madikteta wengine wa Asia ya Kati, tangu 2010 serikali ya Kyrgyz imetoa sheria mpya ambayo inazuia shughuli zozote za kidini ndani ya nchi hiyo. Wengi wanaamini kwamba sheria hiyo imetekelezwa kwa makusudi na serikali kama jaribio la kulazimisha mtazamo wake juu ya dini fulani katika jamii, na lengo lake si jengine ila ni jamii ya Kiislamu. Sheria hii ambayo hivi karibuni ilipitishwa inayalazimisha makundi ya kidini, ima ya halali au la, kusajili mashirika yao. Sheria hiyo pia inakataza ugawanyaji wa fasihi ya kidini ya aina yoyote, iliyopigwa chapa au rekodi za sauti au video, katika sehemu za ummah, shule, na taasisi za elimu ya juu.

Yanayojiri nchini Kyrgyzstan sio hali mpya, bali bado imo ndani ya muundo wa uimla ambao serikali za Asia ya Kati zinasifika nao. Eneo la Asia ya Kati linajumuisha Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan, na Uzbekistan, na watu milioni 55 kati ya milioni 66 ni Waislamu. Tunajua kwamba Waislamu eneo la Asia ya Kati wamepitia ubaguzi mkubwa sana na mateso ya kinyama wakati wa zama za Usovieti hadi leo. Baada ya kuporomoka kwa Muungano wa Kisovieti, siasa za eneo la Asia ya Kati zilishikiliwa na nchi nyingi mpya pamoja na serikali za kidhalimu za kiimla eneo hilo, ambazo kihakika ni urithi wa mabaki ya wakoloni makatili wa chama cha Usovieti wa Kikomunisti. Madhalimu hawa ndio waliokuwa watu wenye nguvu katika Ukomunisti waliokuwa mamlakani kwa muda mrefu. Wameendelea kuinyamazisha da'wah ya Uislamu na wanaharakati wake, kwa kisingizio cha utulivu wa usalama, na malipo yake yamekuwa makubwa. Unyama ndio bei yake. Inajulikana vyema kwamba serikali za kidikteta za eneo la Asia ya Kati zingali zinatabanni vipimo vya Kikomunisti katika kukabiliana na ukuaji wa Waislamu.

Nchi za Asia ya Kati zinazo tawaliwa na madikteta zote zimo katika shirika la kieneo la SCO (Shanghai Cooperation Organization). SCO ni shirika la serikali tofauti tofauti katika eneo la Asia ambalo wanachama wake ni Jamhuri ya Watu ya China, Urusi, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, na Uzbekistan. Isipokuwa Uzbekistan, nchi nyengine zote awali zilikuwa wanachama wa Shanghai Five ambayo ilibuniwa mnamo 1996. SCO ilitangazwa mnamo Juni 15, 2001, baada ya Uzbekistan kujiunga. Shirika hili linakuuza uhusiano baina ya nchi hizi katika nyanja za mipaka ya kitaifa, uchumi, kawi, na utamaduni. Wengi wanasema kuwa shirika hili ni sugu kwa nguvu ya NATO na Amerika. SCO pia ni changamfu katika utoaji wa mipango ya kupambana na Uislamu na wanaharakati wa Kiislamu eneo la Asia ya Kati chini ya pazia la ugaidi.

Wazimu huu dhidi ya Uislamu na Waislamu kihakika mizizi yake ni hofu ya Urusi ya Khilafah. Vladimir Putin, ameelezea hili waziwazi kabisa katika makala yaliyotolewa hivi majuzi nchini Urusi. Alitangaza, "Wataunda Khilafah kuanzia Kaskazini mwa Ulaya hadi Asia ya Kati", - alijibu Putin (2017). "Ndio hatari kubwa zaidi". Putin ameendelea kusisitiza msimamo wake katika kuviongoza vita dhidi ya Uislamu chini ya bendera ya SCO na kuwashinikiza viongozi wa Waislamu eneo la Asia ya Kati ikiwemo Kyrgyzstan. Mnamo Juni 14, 2019, Baraza la SCO lilikongamana katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek, na wajumbe wa nchi wanachama wake walikutana kujadili maswala ya kieneo, hususan maswala ya kiuchumu na kiusalama. Raisi wa Urusi Vladimir Putin, aliyehudhuria na kulielekeza kongamano hilo, alisisitiza haja ya kupigana (na ugaidi na misimamo mikali) chini ya ushirika na nchi nyengine katika eneo hilo na kupigana kwa pamoja. Na  izingatiwe kwamba wakati wa kongamano hilo, Raisi wa Kyrgyz Sooronbay Jeenbekov na Raisi wa Urusi Vladimir Putin walinong'onezana faraghani nyuma ya mlango.   

Muundo wa uimla eneo la Asia ya Kati ni mkusanyiko wa mabaki ya mfumo wa Kikomunisti na maslahi ya kisekula ya leo ya Urasilimali. Unaonyeshwa waziwazi kupitia ushirikiano wa SCO, dori kuu ya Urusi, huku China ikiwa ubavuni mwake. Serikali eneo la Asia ya Kati zimetangaza vita juu ya Uislamu na Waislamu kwa miaka mingi chini ya pazia la "vita dhidi ya ugaidi", na hazijasita kuwakamata wanawake wa Kiislamu. Muundo huu unaonekana kuzishajiisha nchi za Waislamu kama Indonesia, ambayo inatabanni muundo huu huu kupitia utaratibu wa hatua za utiaji hatiani zile wanazoziita 'nembo za misimamo mikali'.

Waislamu wote eneo la Asia ya Kati na kote ulimwenguni wanapaswa kujitahidi kusimamisha tena Khilafah ya pili kama mamlaka halisi ya Ummah wa Muhammad (saw). Ili kumaliza dhiki hizi, wanahitaji kumaliza uungaji mkono wao kwa watawala madhalimu mithili ya Jeenbekov na serikali za kiimla vibaraka wa Urusi, kupitia kusimamisha tena Khilafah kama ngao yao ya kweli.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ)

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [8:36].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Fika Komara

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

مسلمات_قرغيزستان#   

#KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük     

#FreeMuslimahsKyrgyzstan

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 31 Agosti 2020 12:32

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu