- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mwizi Mwenyewe Ndiye Anayepiga Kelele ‘Mkamate Mwizi’ Zaidi ya Wengine
(Msemo wa Warusi)
Unafiki wa Wale wanaolalamika Kuhusu Unafiki
Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje (MOFA) wa Urusi, Maria Zakharova, alitoa maoni kwa majibu ya Muungano wa Ulaya (EU) juu ya hukumu ya kile kinachoitwa ‘Kesi ya pili ya Bakhchisaray ya Hizb ut-Tahrir’. Aliwaonya washirika wa Ulaya kutokana na kuwagawa magaidi katika makundi ya wazuri, wabaya na wa wastani.
“Suala hili linashughulika na washiriki katika seli ya Crimea ya shirika la Kiislamu la Hizb ut Tahrir. Wamepata vifungo tofauti kutokana na uhalifu wa kigaidi uliothibitishwa. Kinyume na madai ya Brussel, maoni yao ya kisiasa, utaifa au asili yao havina uhusiano wowote na hukumu hiyo ya mahakama. Hii sio mara ya kwanza kuyaona majaribio ya washirika wetu Wamagharibi kuwagawa magaidi kwenye makundi ya wazuri, wabaya na wa wastani. Kwa masikitiko, wakaazi wa nchi za Ulaya (EU) wenye uzoefu wa vitisho vya mashambulizi ya kigaidi ya mwanzoni kabisa wanaelewa matokeo ya kutisha ambayo majaribio kama hayo yanayo.”
Alisema pia kuwa shirika hili limefungiwa nchini Ujerumani tokea 2003. (Source:https://www.mid.ru/en/diverse/-/asset_publisher/zwI2FuDbhJx9/content/brifing-oficial-nogo-predstavitela-mid-rossii-m-v-zaharovoj-moskva-23-sentabra-2020-goda)
Kwa mara nyengine tena, tunashuhudia namna ambavyo maafisa wakuu wa shirikisho la Urusi wanakimbilia uongo wa wazi na uzushi katika jaribio la kuhakikisha matendo yao ya kihalifu yanayoitwa sheria za Urusi za kuwatiisha Waislamu.
Katibu wa Habari wa Wizara ya Kigeni ya Urusi akizungumza kuhusu hukumu ya hatia ya Mahakama ya Wilaya ya Kusini ya Kijeshi iliotolewa Septemba 16, 2020 ndani ya kile kinachoitwa “kesi ya pili ya Bakhchisarai ya Hizb ut Tahrir” kuhusiana na Waislamu 7 kutoka Crimea inajaribu kuwadanganya watu kwa kudai kuwa watu hawa 7 walikuwa wamehukumiwa kwa matendo ya kigaidi.
Dai lake kuwa “Tunapaswa kuelezea kwa masikitiko kuwa tabia ya kuvuruga ukweli kwa mtazamo wa kupotosha walimwengu imekuwa ni nembo ya kidiplomasia ya EU” katika ushirikiano unaotumika kwa Zakharova na serikali anayoiwakilisha.
Inavyoonekana, Zakharova hakujali hata kusoma hukumu hiyo ya Mahakama ya Kijeshi ya Wilaya ya Kusini. Bila shaka, ili kufahamu kiburi chote na uwongo wa matamshi ya Zakharova “kuhusiana na uhalifu wa kigaidi”, inatosha hata kugeukia nafasi ya mashtaka ya serikali.
Msingi rasmi wa madai katika “kesi ya ugaidi” sio kupanga, matayarisho au utekelezaji wa matendo ya kigaidi, lakini mkutano wa wazi (subhet) katika msikiti wa Bakhchisarai, ambao ulihudhuriwa na makumi ya watu. Pia, Waislamu waliotiwa hatiani walihukumiwa kwa kusoma vitabu vya Kiislamu na mazungumzo kuhusiana na Uislamu.
Uamuzi huu wa kisiasa sio wa kimahakama uliopitishwa na mfumo mbovu wa haki wa Urusi pia unafichua kufilisika kwake wenyewe kwa kuwa simu, hard drive, tablet, kipakatalishi na keyboard vinatambuliwa kuwa ni vifaa vya kihalifu katika hukumu ya mahakama hii!!!
Hakuna ramani, hakuna muongozo wa mipango ya mashambulizi ya kigaidi, hakuna silaha, hakuna miripuko, hakuna hata mazungumzo ya kupanga chochote kinachohusiana na vurugu kuwa ni ushahidi wa maana katika kuthibitisha mashtaka haya.
Waendesha mashtaka na majaji mara kwa mara wamethibitisha katika vikao vya mahakama kutokuwepo alama hata ndogo za harakati za kigaidi kwa upande wa washtakiwa, wakimaanisha tu uamuzi mbaya kwa Mahakama ya Upeo ya Shirikisho la Urusi mwaka 2003. Waraka wa Kimahakama ambao haukuwa ukifanya kazi katika maslahi ya jamii ya Urusi ambayo sehemu yake kubwa ni Waislamu, lakini ulitumika kwa maslahi ya serikali ya Urusi. Mwaka 2003 Mahakama ya Upeo ya Urusi ilihakikisha uamuzi muovu ambao unatambua idadi kadhaa ya mashirika ya Kiislamu kuwa ni ya kigaidi, hii ikikusudia kufikia baadhi ya malengo katika sera za ndani na kigeni.
Hizb ut Tahrir imepatiwa mistari michache tu katika uamuzi huu wa kushangaza, ambapo hakuna hata neno moja lililotajwa lenye msingi wa “ugaidi”, achilia mbali kuleta angalau ukweli mmoja wa kuihusisha Hizb katika matendo ya vurugu.
Washiriki wote waovu wa umoja huu, ima ni FSB (Wachunguzi wa Usalama wa Shirikisho), waendesha mashtaka, mahakimu au wamiliki kutoka afisi za juu walio nyuma yao wote wanafahamika vyema – kile kinachotokea si chochote bali ni uadui dhidi ya Uislamu, ambao unachochewa na wivu na hofu isiyo na msingi na baadhi ya wakati chuki za kiitikadi.
Hata hivyo, watu na mashirika ambayo hayahusiki na ugaidi na matendo ya kigaidi wakati mmoja walichukuliwa kuwa ni wahalifu na magaidi.
Hizb ut Tahrir ni chama cha siasa cha Kiislamu ambacho kinajifunga katika matendo yake kwenye kazi za kifikra na kisiasa pekee. Majaribio yoyote ya kuituhumu Hizb ut Tahrir kwa ugaidi yanavunjika kwa historia ya miaka 60 ya kazi za Hizb katika nchi zaidi ya 40 za ulimwengu.
Ama kwa tamko la Zakharova la kupigwa marufuku kwa Hizb ut Tahrir nchini Ujerumani katika jaribio la kujiunga na kile kinachojulikana kwa uovu wa “jitihada za kimataifa dhidi ya ugaidi”, hapa pia tunaona majaribio ya kupotosha ukweli.
Kufungiwa kwa Hizb ut Tahriri nchini Ujerumani mwaka 2003 hakuhusiani na mashtaka ya ugaidi. Idadi kubwa ya wanachama wa Hizb ut Tahrir bado wanaendesha shughuli zake nchini Ujerumani, na hakuna mashtaka ya uhalifu wa wanachama wa harakati hii katika nchi hii.
Kwa kweli, marufuku yote imeshuka kufikia kutowezekana kwa usajili rasmi na kutowezekana kufanyika matendo ya wazi kwa upande wa Hizb ut Tahrir nchini Ujerumani.
Kwa hivyo, kuwekwa kizuizini, kipigo, mateso kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Urusi pamoja na kuandamwa na kutiwa hatiani kwa kipindi cha tarakimu za makumi ya miaka chini ya kisingizio cha kupigana na ugaidi haiwezi kulinganishwa na uhalisia wa kuzibana harakati za Hizb ut Tahrir za wazi nchini Ujerumani.
Zaidi ya hayo, Zakharova kwa makusudi hakutaja kauli za maafisa na vyombo vya utekelezaji sheria vya nchi za Ulaya, ambavyo vimetamka kuwa haiwezekani kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir kutokana na kukosekana kwa kidokezo hata kidogo cha ugaidi au fujo.
Pamoja na majaribio ya kilaghai kupitisha fikra za matakwa yake kuwa ni uhakika, Zakharova ameonyesha kushindwa kabisa katika suala hili, pamoja na uelemeaji wake wa kisiasa.
Hapa, kutokana na muundo uliobanika, sitozama kwenye sababu za kupigwa marufuku Hizb ut Tahrir nchini Ujerumani. Nitataja tu kuwa kupigwa marufuku huku ni mfano wa wazi wa suala la “uhuru wa kusema” unaotukuzwa na Wamagharibi, ikiwemo Ujerumani, humalizika mara tu unapohusu Waislamu na wito wao kwa ajili ya mradi wa kisiasa wa Kiislamu.
Akitoa maoni juu ya maneno ya Zakharova kuhusu kutokubalika kutumia “unafiki katika mapambano dhidi ya ugaidi”, izingatiwe kuwa Urusi katika suala hili inashiriki nafasi ya mwanzo ya heshima pamoja na wanaoitwa “washirika wa Kimagharibi”.
Hivyo, mamlaka za Urusi hazifuati misingi yake yenyewe juu ya jinai na maamuzi, achilia mbali kufuata maadili mazuri au ya kibinaadamu.
Kilele cha unafiki ni onyo kuhusu matokeo ya “mchezo wa kugawanya magaidi katika wazuri na wabaya”.
Nchi nyingi kote duniani zinakabiliana na unafiki wa Urusi katika mapambano yake dhidi ya ugaidi.
Watu wengi na hasa wakaazi wa Ulaya wana uzoefu mwanzoni kabisa wa vitisho vya mashambulizi ya Urusi na wanajua matokeo ya majaribio hayo yalionayo ya kuhuzunisha.
Urusi iliwapachika Waislamu wa Syria, walioasi dhidi ya ukatili wa Assad, kuwa ni magaidi, wakati ikipeleka “watu washenzi” Ukraine Mashariki na Crimea, na kuwa wapiganaji.
Zaidi, Urusi imefuata matendo ya kihalifu ya Amerika ya kutumia Makampuni Binafsi ya Kijeshi kama Blackwater inayojulikana kama Academi kwa kuunda mfano wake ya Urusi inayoitwa PMC Wagner, ambapo uhuni wao umewafanya kuwa mamluki katika mikono ya wahalifu wa kimataifa.
Urusi, katika desturi zao bora za “ugaidi wa wakomunisti” (red terror), iliwamaliza wapinzani wa kisiasa katika miji ya Ulaya, hata kuamua kutumia sumu hadi silaha za kemikali na mionzi. Na baada ya yote haya, Zakharova anajaribu kusoma hotuba kuhusiana na kutokubalika kuunga mkono magaidi? Urusi sio tu inaunga mkono magaidi; bali yenyewe ni dola ya kigaidi.
Kwa ufupi, tunasema:
Zakharova na utawala wa kisiasa ambao anauwakilisha hutumia uongo, uzushi, unafiki na utapeli ili kuwashawishi watu kuwa wanatenda kwa njia sahihi.
Matendo ya Urusi katika hali ambayo kila mtu awe ni mshirika katika uovu wake, wakati ambapo kwa mujibu wa yanayoitwa masuala ya Hizb ut Tahrir, zaidi ya watu 300 wamepewa vifungo vikubwa, vikiwemo vya kipindi cha tarakimu za makumi ya miaka, kwa sababu tu ya kulingania Uislamu na kusema, “Mola Wangu ni Mwenyezi Mungu”.
Kwa matendo haya, Urusi inajaribu kuficha ukweli, ambao uko wazi kwa kila mtu, kuwa ni dola ya kigaidi.
Msemo huu wa Kirusi ni fasaha zaidi, mfupi na wenye kuelezea kwa usahihi juu ya kinachofanyika leo:
"Mwizi Mwenyewe Ndiye Anayepiga Kelele ‘Mkamate Mwizi’ Zaidi ya Wengine"
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fazil Amzaev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine