Jumatano, 14 Jumada al-thani 1442 | 2021/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipaumbele vya Amerika

Uchaguzi wa uraisi wa Amerika umeonyesha mgawanyiko mkubwa nchini Amerika na kile ambacho raisi wa Amerika Donald Trump kwa muda mrefu akicheza nacho. Rais mpya wa Amerika hivi sasa anakabiliana na changamoto za msingi katika kuiongoza Amerika kupitia changamoto mbali mbali za kistratejia. Ushindi wa kura wa Democrat kwa namna nyingi haubadilishi ukweli kuwa Amerika inakabiliana na idadi kubwa ya changamoto na yeyote ambaye angeweza kushinda uchaguzi angekuwa na jukumu la kukabiliana na masuala haya ya kimsingi. Ya muhimu zaidi katika haya ni:

Hivi sasa China rasmi ni nchi yenye nguvu kubwa katika eneo ikiwa kileleni kiasi cha kuipa changamoto nafasi ya Amerika katika eneo la Kusini Mashariki ya Asia. Utawala wa Trump ulichukua hatua kali dhidi ya China na ulianzisha vita vya kiuchumi. Licha ya hatua za kujirejea za ongezeko la kodi na kuionyesha China kuwa inamiliki sarafu kwa manufaa yake (kisha baadaye kuiondoa), hakuna kilichotatuliwa kuhusiana na masuala ya msingi. Yeyote ambaye angeweza kushinda uchaguzi wa raisi angeweza kukabiliana na kipaumbele hichi cha kimkakati. Changamoto kwa Amerika ni matendo yake dhidi ya China ambayo hayafikii malengo yake iliyokusudia na katika kipindi hichi China inatanua nafasi yake. Amerika karibuni itafikia hatua ya kujaribu kila kitu kuzuia ukuaji wa China, kwa kifupi ikiwa ni vita halisi.

Amerika kwa muda mrefu imeweka macho yake kwa Afghanistan, kabla hata ya matokeo ya 9/11. Ukaribu wake kwa Asia ya Kati na Urusi, pamoja na China imeufanya kuwa jambo la kulikusudia kuwa ni msingi wa kutangulizwa katika eneo kushughulikia changamoto zinazoibuka kwa nguvu za Amerika. Raisi trump amevirithi vita vya Afghanistan ambavyo watangulizi wake wameshindwa kuvitatua. Wakati Trump akizungumza kuhusu kuvimaliza vita, amegeuka juu ya hili. Trump ametangazia sana juu ya juhudi zake binafsi katika kukubaliana juu ya mkataba na Taliban. Lakini uhalisia ni kuwa, Amerika inakabiliwa na matatizo makubwa katika kufikia dhumuni lake, ambalo Trump hajasaidia kwa uingiliaji kati wake wa kutafuta umaarufu. Hali halisi ni kuwa Amerika inaendelea hatua kwa hatua kuipoteza Afghanistan kwa Mujahidina wa Kiafghan na wanafahamu kuwa ni suala la muda tu kabla hawajatolewa kikamilifu na hivyo kuhitajia kukamilisha mapatano ya amani wakati bado wakiwa na baadhi ya umiliki.

Amerika hivi sasa inakabiliana na tatizo ambalo himaya zote hukabiliana nalo, la kuwa katika maeneo yote, na wakati huo huo kudhibiti kile inacho kikoloni. Kama zilivyokuwa himaya za kabla yake, Amerika inatumia jeshi lake, katika kiwango cha juu cha utayari kote ulimwenguni kushikilia nafasi yake. Haya yote yanahitaji fedha, fedha ambazo haziwezi tena kutumika kwenye elimu, miundo mbinu au afya. Kodi za ndani hazitoshelezi kugharamia haya na hivyo kuelekea kwenye madeni, ambayo yametengeneza kiputo cha madeni ya dolari trilioni 22! Vita vya Afghan vimekusudiwa kuondoa taka taka, askari wa karne ya 7, lakini hivi sasa ni vita vya kuendelea visivyo onyesha kuwa na mwisho. Uhalali wake pekee hivi sasa ni kubakisha uaminifu kuliko kuwa na mwisho wowote wa kistratejia. Maafisa wa Amerika hivi sasa wanakiri kuwa nchi yao imejitanua sana ikiwa inashughulikia masuala mengi sana ya ndani na majukumu ya kimataifa. Amerika inaishi zaidi ya uwezo wake; inakabiliana na changamoto za kieneo kote duniani ambako imejitanua. Yeyote ambaye angeweza kushinda uchaguzi wa Uraisi, atakabiliwa na kushughulikia tatizo hili.

Sera za utawala wa Trump zimeumiza muungano na urafiki ambao Amerika iliujenga kwa umakini kwa kipindi cha miongo kadhaa na ilikuwa ni katika rasilimali kubwa kwa zaidi ya miaka 70 iliyopita. Sera ya Trump ya ‘Amerika kwanza’, inayo rejewa rejewa imewacha ombwe ambalo China imeliziba kwa haraka. Kwa mataifa ya dunia, Amerika sio tena yenye nguvu kama ilivyokuwa kabla ya vita vya Iraq na Afghanistan na kwa kujitoa Amerika kwenye taasisi za kimataifa, China imekuwa mshirika mwenye kuaminika zaidi, ikiwa na uwezo mkubwa katika matumizi. Wakati Trump huenda akaamini kuwa anaiangamiza Amerika ili kuihifadhi, Amerika inahitaji mshikamano, usikivu na utiifu wa mataifa mengine ili ifikie ajenda yake ya kiulimwengu.

Huku raisi mpya wa Amerika wakati wote akiwa huvutia hisia za dunia, kiuhalisia raisi anauwezo mdogo sana kufanya mabadiliko ya msingi kwa sera muhimu za Amerika. Raisi wa Amerika anagawanya mamlaka pamoja na bunge la Seneti na wingi wa vyombo kutoka sekta za kifedha, maeneo ya ulinzi na kampuni za kimataifa. Maraisi wote wameweka mtazamo wao maalum kufikia malengo ya kistratejia, lakini malengo haya ya kistratejia si aghlabu kubadilishwa. Amerika inakabiliana na mgogoro kama dola kuu kwa kuwa imekuwa na mafanikio katika sera chache sana za kigeni tokea 2003. Kwa upande wa masuala ya ndani, tokea mgogoro wa kiuchumi wa kiulimwengu mwaka 2008, changamoto za ndani za Amerika zimeongezeka na zimekuwa zenye usumbufu zaidi. Wakati huo huo, tawala zinazofuatana zimeonyesha uwezo mdogo zaidi kuzitatua.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 25 Novemba 2020 20:28

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu