Jumanne, 17 Muharram 1446 | 2024/07/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ushuhuda wa Shahzad Sheikh Kuhusu Naveed Butt
#MjueNaveedButt
#MwacheniHuruNaveedButt

Nilikutana na Naveed Butt kwa mara ya kwanza kwenye darsa aliyokuwa akihutubia katika Bustani ya Aziz Bhatti jijini Karachi, kabla ya kuwa mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Mtu mrefu, mpana, mwenye ngozi nzuri na ndevu zilizotunzwa vizuri, alikuwa mwenye umbo la mtu mtanashati, lakini alikuwa amevaa vazi la haya na akili razini. Baada ya mkutano huo wa kwanza, nilikutana naye mara mbili zaidi, ingawa kwa kifupi tu, bila kupata nafasi ya kuzungumza naye mengi. Lakini, nilivutiwa sana na njia yake nzuri ya kuongea na kuhutubu. Wakati fulani baada ya kuwa mwanachama wa Hizb ut Tahrir, niliwadhifishwa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Pakistan, na kuwa naibu msemaji wa Naveed. Baada ya kuwa naibu wake, nilikuwa na fursa nzuri ya kutumia wakati pamoja naye, kujifunza mengi kutoka kwake.

Jambo la kwanza kumhusu ambalo lilinishangaza ni kwamba ni watu wachache sana katika Hizb walimwita Naveed Butt. Watu wengi walimwita "Maamoo" (mjomba). Nilipomuuliza mtu mmoja ni kwa nini ilikuwa hivyo, niliambiwa kwamba mmoja wa watoto wa dada zake yuko katika Hizb pia, kwa hivyo kwa kuwa anamwita Maamoo, kila mtu sasa anamwita Maamoo. Nilipenda pia kumwita Maamoo, ingawa uhusiano wangu naye ulikuwa kwa njia ambayo alikuwa kama kaka yangu mkubwa.

Nakumbuka matukio machache kuhusiana na Maamoo ambayo kamwe siwezi kuyasahau.

Maamoo alikuwa akitembelea Karachi mara moja au mbili kwa mwaka, wakati ambao niliandamana naye kwenye mikutano na wanahabari. Wakati mmoja, alipokuwa ziarani, tulikutana na mhariri mkazi wa jarida la kila siku la Kiurdu. Mhariri mkazi huyu alivutiwa sana na Maamoo na akatupeleka kuonana na rafiki yake wakili. Wakili huyo hakuwa tayari kukubali kwamba Quran na Sunnah zinatupa sheria za kina za utawala, uchumi na mahakama, akisema kwamba kamwe hajawahi kuona hivyo ndani ya Quran. Kwa hivyo, Maamoo alimuuliza tu, je, Katiba ya Pakistan inatupa sheria zozote za kina? Wakili huyo akaanza kumtazama Maamoo usoni kwa mshangao. Halafu, Maamoo akafafanua kuwa vitabu hivi vingi vya sheria katika afisi yake vimetolewa kutoka kwa Katiba hii hii ya Pakistan, ikitoa maelezo ya mfumo huu, unaotekelezwa nchini Pakistan. Baada ya hili Maamoo aliwasilisha majina kadhaa ya vitabu maarufu vya sheria ya Kiislamu (fiqh), akimuuliza wakili kama amewahu kuvisoma. Wakili huyo alikiri kwamba hakuwa amevisoma. Kwa hivyo Maamoo aliuliza, ni vipi unaweza kusema kwamba Quran na Sunnah haitoi mfumo wowote wa maisha, ikiwa havijasoma vitabu hivi? Na nilishangazwa na jinsi Maamoo alivyojua vitabu vingi vya sheria ya Kiislamu (fiqh).

Vivyo hivyo, wakati wa ziara nyingine, tulishikwa na kiu katika mchana wenye joto kali, kwa hivyo tulisimama kwenye duka la vinywaji baridi, ambapo niliagiza Apple Sidra. Napenda Apple Sidra sana, tangu utoto mwangu, lakini kawaida haipatikani kwa urahisi. Maamoo alikubali kwamba ninunue kinywaji, lakini kisha akaniomba nilete kinywaji kingine. Nikamuuliza Maamoo, kwa nini hunywi, kuna kitu kibaya? Alisema kuwa nina shaka, kuhusu ikiwa inaruhusiwa kunywa Apple Sidra. Nilisema hakuna chochote kibaya nayo, lakini ikiwa huridhiki basi mimi pia sitakunywa. Kwa mara nyingine tena alithibitisha amri yake juu ya sheria za Kiislamu (fiqh), kwa kusema kwamba unaweza kunywa kama umeridhika, lakini mimi siwezi, kwani nina shaka. Kawaida viongozi huwalazimishia wengine matakwa yao, lakini Maamoo hakulazimisha uelewa wake kwangu katu, akiniacha nitende kulingana na uelewa wangu mwenyewe.

Kuna tukio jengine ambalo kamwe siwezi kulisahau, wakati ninaandika juu yake, machozi yananilenga lenga machoni mwangu. Maamoo alikuwa akitujali sana, kiasi kwamba hata kama hatungemshirikisha shida zetu za kiuchumi na wasiwasi mwingine juu ya maisha naye, angejua kuyahusu, kwa namna fulani. Wakati  mmoja alinipa rupia elfu hamsini, kwa hivyo nikamuuliza Maamoo, kwanini unanipa hizi? Alisema kuwa nimepokea pesa kutoka kwa urithi na najua unakabiliwa na shida, kwa hivyo ndio sababu ninakupa pesa hizi. Nilisema Maamoo wewe pia huko sawa, kwa hivyo sasa kwa kuwa umepokea pesa kutoka kwa urithi, lazima uzitumie kwa familia yako, kwa kuwa huna jukumu kwangu. Lakini, alinilazimisha nikubali pesa hizo. Siku hiyo hakika nilihisi kuwa nina kaka mkubwa. Baada ya tukio hilo, alinipa elfu thelathini, wakati mwingine.

Siku nilipopokea habari za kutekwa nyara kwa Maamoo, nilikuwa njiani kutoka mjini kwangu kukutana naye na niliagizwa nirudi. Siku hiyo, hadi mwezi mmoja, baada ya kutekwa nyara kwake zilikuwa siku ngumu sana maishani mwangu. Lakini, kisha nikatulia, kwa msaada wa Mashababu, nilianza kufidia kutokuwepo kwake, ili siku atakaporudi, asihuzunike kwamba naibu wake hakuweza kuonyesha jinsi alivyomfundisha vizuri. Hii ni ingawa, wakati ninajitathmini, nadhani sijaonyesha hata asilimia kumi yake. Katika miaka hii minane ya kutekwa nyara kwake, nimemwona mara nyingi katika ndoto zangu na kila wakati namuona akiwa katika hali nzuri. Ninajaribu kuhakikisha kuwa hakuna Swala inayoswaliwa bila ya kuomba Dua Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya kurudi kwa haraka na salama kwa Naveed. Katika maisha yangu, ikiwa nina hamu kubwa nyingine yoyote mbali na kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ni kwamba ninataka kumkumbatia Maamoo kwa mara nyingine tena.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shahzad Sheikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu