- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Haki Zilizochukuliwa na Madhalimu Hazirejeshwi Kupitia Unyenyekevu
(Imetafsiriwa)
Haki za Waislamu hazirejeshwi kupitia unyenyekevu, ulegezaji msimamo, diplomasia na mapatano. Haki zilizoporwa za Waislamu zitarejeshwa kwa msimamo wa ujasiri, mapambano na kujitoa muhanga. Ibn Khaldun (rh) alipohusisha unyenyekevu wa Bani Israil, alionya juu ya udhalilifu kabla ya ukandamizaji katika Muqadimah (utangulizi) wake. Aliandika,
أن المذلة والانقياد كاسران لسورة العصبية وشدتها فإن انقيادهم ومذلتهم دليل على فقدانها فما رئموا للمذلة حتى عجزوا عن المدافعة
“Hakika madhila na unyenyekevu vinavunja bidii ya kundi na nguvu zao. Hakika madhila yao na unyenyekevu wao ni dalili ya kupotea kwao. Hawakuchukia hali ya udhalilifu hadi wakashindwa kujihami.”
Katika zama zetu za mwenye nguvu mpishe na utamaduni wa VIP, ni lazima ifahamike wazi kuwa nguvu haiji kutokana na mamlaka, cheo, utajiri au itifaki, bali ni kutokana na msimamo madhubuti, bila kujali kuwa yupo mamlakani ama la. Muislamu anaweza asiwe na hata uwezo wa kutwaa mamlaka na utawala, lakini hatokuwa dhalili na mwenye kunyenyekea mbele ya watu au watawala, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt).
Abu Dharr (ra) amesema kuwa alimuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amteuwe kuwa Gavana, lakini (saw) alimgonga begani kwa mkono wake na akasema,
«يَا أَبَا ذَرٍّ إِنَّكَ ضَعِيفٌ وَإِنَّهَا أَمَانَةٌ وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ إِلَّا مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا»
“Ewe Abu Dharr, hakika wewe ni dhaifu, na hii ni amana na itakuwa ni sababu ya hizaya na majuto siku ya kiama isipokuwa kwa yule aliyeichukua kwa haki yake na kupeana haki iliyo juu yake ndani yake.” (Muslim). Katika mapokezi mengine amesema (saw) kumwambia,
«يَا أَبَا ذَرٍّ إِنِّي أَرَاكَ ضَعِيفًا وَإِنِّي أُحِبُّ لَكَ مَا أُحِبُّ لِنَفْسِي لَا تَأَمَّرَنَّ عَلَى اثْنَيْنِ وَلَا تَوَلَّيَنَّ مَالَ يَتِيمٍ»
“Ewe Abu Dharr, mimi ninakuona dhaifu na mimi ninakupendelea yale yanayoipendelea nafsi yangu. Usikubali kuongoza juu ya watu wawili na wala usisimamie mali ya yatima.” Imam An-Nawawi amesherehesha,
هذا الحديث أصل عظيم في اجتناب الولايات، لا سيما لمن كان فيه ضعف عن القيام بوظائف تلك الولاية
“Hadithi hii ni msingi mkubwa katika kuepuka uongozi, hasa hasa kwa yule aliye na udhaifu juu ya kusimamia nyadhifa za dola.”
Hata hivyo, kutoweza kwake kutawala, Abu Dharr al-Ghafari (ra) hakuwa dhalili wala mwenye kunyenyekea. Kwa hakika, (ra) alitangaza kwa ushujaa Uislamu wake mbele ya Maquresh, mabwanyenye wa Makkah na akashambuliwa kikatili na kupigwa bila huruma. Kwa ujasiri alirudi kwa watu wake, kabila la Ghifar, na hakupumzika hadi idadi kubwa ya watu wakaingia kwenye Uislamu, akiupiga pigo kubwa Ushirikina wa Kikureish.
Kwa hakika, Abu Dharr (ra) alikuwa ni mwenye shakhsiya imara aliyeangaza kama nyota inayoongoza kwa shakhsiya imara za hivi leo. Kwa hakika, Waislamu hawatakiwi kuwa madhalili au kuwa wenye kunyenyekea mbele ya madhalimu ambao wanautesa Ummah wa Kiislamu. Wao ni waporaji haramu wa mamlaka, kizazi cha Yazid, kwa kuwa hawakuteuliwa kutawala kupitia Bay’ah ya kisheria, kutawala kwa Uislamu. Wao ni wale wanaopuuza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Wao ni wale wanaozikaribisha ghadhabu za Mwenyezi Mungu (swt) kwa kujiingiza katika yale aliyoyakataza Yeye (swt). Hakuna fursa ya kukubali, kuafikiana au kuvumilia juu ya dhulma zao. Hakuna njia ya kuelekea kwenye mabadiliko isipokuwa kwa yule aliyeandaliwa vyema kupitia juhudi kubwa, mapambano na kujitoa muhanga, akifuata nyayo za kizazi kilicho bora zaidi, Masahaba (ra).
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan