Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jinsi Vyombo Vya Habari Vinavyopotosha Maoni kwa Kulazimisha Utatanishi na Ulinganishi wa Uongo

(Imetafsiriwa)

Utatanishi ni hali ya kisaikolojia ya mwanadamu ambayo hutokea pindi akili inapokubaliana na mawazo mawili yanayo kinzana kiasi cha kumfanya mtu kukosa utulivu. kutatua hisia hizi mbaya mtu hufanya uhalali batili wa kile kinacho mtatiza na kuruhusu mawazo mawili yanayo kinzana yote kuchukua nafasi kama ukinaifu.

Mifano ya hali ya utatanishi inaweza kupatikana katika mahusiano ya kinyanyasaji. Mtu anaweza kuelewa wazi kuwa kuwa mkali au mwenye lugha chafu ni tabia mbaya. Lakini ikiwa imetokea kwa mtu wanayemjua kumpenda na kumuamini, wanaweza kufikiria kuwa kutokea kwake ni kwa sababu ya kuondoka kwa mapenzi na wasiwasi mkubwa. Kwa matokeo haya, watavumilia hali ambayo ingedhaniwa kuwa haiwezi kuvumiliki. Wanaweza hata kwenda kinyume na nafsi zao wenyewe kwa kumpa rafiki ushauri kuachana na mahusiano mabaya, lakini wao bado wakiyadumisha yao kwao wenyewe.

Usawa wa uwongo ni masimulizi ambapo maswala mawili tofauti yanaonekana kuwa na kiwango sawa cha thamani na hulinganishwa kwa maneno sawa ilhali kiukweli vinastahili ushughulikiaji wa kitofauti. Kulazimishwa kinguvu kuunganisha baina ya dhana mbili mara nyingi huishia kudharau upande wa majadiliano na hutumiwa kama njia ya kudanganywa ili kupata faida isiyofaa katika majadiliano.

Mfano wa hii inaweza kuwa kama vile mwanaikolojia anavyoona vitu vitokanavyo na nyuklia kuwa hatarishi kwa mazingira na wanaweza kufanya kampeni ya kupiga marufuku vifaa vyote vitokanavyo na nyuklia kutumika, pamoja na matibabu ya mionzi katika hospitali zinazosaidia wagonjwa wa saratani. Njia hii nzito ya “kupaka kila kitu kwa brashi moja” ni mbinu yenye kasoro kiakili. Mchakato wa kufikiria unashindwa kutambua kuwa matibabu ya mionzi inaokoa maelfu ya maisha na kutibu vizuri, taasisi za matibabu zinapaswa kuruhusiwa kunufaika na rasilimali hii muhimu.

Mawazo haya yaliyotajwa hapo awali hutumiwa na vyombo vya habari kudhibiti mawazo ya umma na kusababisha ubaguzi katika utoaji wa habari. Ripoti ya kukaliwa kwa Palestina ni kisa cha kawaida.

Mtazamo kwamba mtu anaweza kuchukua kitu kinguvu ambacho sio chake unajulikana kama kitendo haramu cha wizi.

Mtazamo wa kuthibitisha ubora wa mtu kwa msingi wa nasaba yake DNA unajulikana ulimwenguni kama kitengo cha ubaguzi.

Dhana ya utoaji haki za kibinadamu tofauti kwa misingi ya kikabila, kiuchumi au kijografia inaeleweka ulimwenguni kuwa kitendo cha dhulma.

Kuua, kukamata, kuteka nyara, na utesaji watoto vinaeleweka ulimwenguni kuwa uhalifu uliochupa mipaka.

Kushindwa kuchukua hatua ndani ya mipaka ya sheria za kimataifa inaeleweka kuwa kitendo cha vita na ugaidi.

Walakini hayo yote hapo juu yanathibitishwa kilugha kwa matumizi ya lugha inayowashawishi watu kukubali kisichokubalika kwa kuvifanya kuwa halali.

Utafiti uliofanywa na MIT ulichambua makala 33,000 ya gazeti la New York Times wakati wa mageuzi ya kwanza na ya pili kuonesha jinsi gani ubaguzi wa Orientalist dhidi ya Wapalestina ulivyokuwa wazi katika habari nyingi za Amerika.

Mfano wa hivi karibuni unaweza kuonekana katika majadiliano ya namna walowezi wa kizayuni walivyoshambulia makaazi ya wapalestina ya Sheikh Jarrah na kuwaondoa kinguvu kutoka katika nyumba zao na ardhi ya mababu zao.

Maneno kama “kufukuzwa” yalitumiwa kuelezea tukio ambalo lilibadilisha dhana ya kwamba nyumba zilishatapeliwa na watu walilazimishwa kuhama makaazi. Kuchanganyikiwa kiakili sambamba na vurugu zilizokithiri za watu wasio na silaha ikaonekana kuwa ni haki. Wazo kwamba “wako kwenye ardhi ya Israel na wanaondolewa kihaki” hutatua tatizo la uvamizi kuonekana wa kidhulma sana katika vyombo vya habari.

Ukiukaji wa sheria za Umoja wa Mataifa juu ya haki ya kuabudu zimekuwa zikivunjwa kila wakati, kesi ya hivi karibuni. Machapisho yaliyo samba mitandaoni ambayo yaliyoonesha ukweli kwamba walowezi wa ‘Israel’ walielezea wazi kuwa “ikiwa hawataichukua nyumba hiyo, mtu mwengine ataichukua” yaliwafanya watu kuona zaidi yale masimulizi yaliyopotoshwa katika vyombo vya habari.

Wakati wa shambulizi la Mei 2021 dhidi ya Wapalestina wakati wakiendelea na ibada katika msikiti wa Al Aqsa, tukio hili liliripotiwa kwa njia ambayo ilidhoofisha ukweli kwamba huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita katika sheria za kimataifa. Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha habari cha uturuki TRT habari za ulimwengu iliripoti kwamba maneno kama “mapigano”, ‘Israel’ mabomu ya gaza na matamshi ya tafsida kama “mgogoro” na “milipuko” yalitumiwa. Kwa maneno ya kutofahamika, hii ilimruhusu mtu kutafsiri kuwa udhahiri huu mkubwa wa ukosefu wa usawa katika nguvu ulikuwa ni “jibu” kwa vitendo visivyojulikana vya vurugu kwa upande wa wenye kuabudu wasiona hatia.

Ripoti ya TRT inanukuu yafuatayo katika Makala yake ya tarehe 27 Mei 2021: “viwango vya uhariri vimepitishwa na vyombo vya habari kama vile Deutsche Welle ambayo inawazuia waandishi wa habari kutumia maneno kama “ukoloni au ubaguzi wa rangi” wakati wa kuripoti uhalifu wa serikali ya Israel. Kumekuwa na ripoti za waandishi wa habari kuondolewa kuiangazia Gaza kwa sababu walivitaka vyumba vya habari “kujumuisha muktadha wa kihistoria na kijamii, waandishi wa habari wenyewe ufahamu wa eneo hilo, na la muhimu zaidi, sauti za Wapalestina."

Nukuu ya hapo juu inaonesha jinsi gani lugha inavyofuatiliwa kikamilifu ili kupotosha mtazamo wa umma katika kuunga mkono Uzayuni na kuhitajika uwepo wa dawamu ya utumaji ujumbe ili kusiwe na uthamini mbadala kwa uwepo wa Wapalestina.

Utafiti mpya unaonesha jinsi uwezekano wa Wapalestina kuhusishwa na matumizi ya lugha za uchochezi ni mara 1.5 kuliko ‘Waisraeli’ na mara mbili zaidi kuangaziwa mara kwa mara katika magazeti juu ya Intifada ya Kwanza na ya Pili ya Wapalestina. (Mark Lennihan/ AP)                   

Vichwa vya habari vya upotoshaji katika habari vimewekwa ili kuleta athari za ubaguzi dhidi ya Waislamu hata kama watu watakosa kusoma maelezo yaliyo andikwa ndani ya gazeti. Hili limejadiliwa kiundani zaidi katika Makala ‘Gazeti la New York Times Lapotosha Mapambano ya Wapalestina’ na Holly M Jackson katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT). Utafiti huo wa Jackson ulionesha kitakwimu kuwa ingawa vurugu za ‘Israel’ zilizidi zile vurugu za Wapalestina. Vipengele viwili vya kilugha vilitumika kama lengo la utafiti katika mbinu za uwasilishaji wa taarifa. Kwanza ilikuwa kutambua kama vitendo vya vikundi vya ‘Israel’ na Wapalestina vilikuwa vikielezwa kwa sauti kali na hafifu. Pili ilikuwa kuainisha malengo na lafudhi ya lugha iliyotumika.

• Karibu asilimia 40 walivitaja vikundi vya Wapalestina au watu binafsi, huku karibu asilimia 93 wakivitaja vya ‘Waisraeli’

•Karibu asilimia 12 ya uasibishaji wa Wapalestina ulitumia lugha ya uchochezi, tofauti na asilimia 5.9 wa ‘Waisraeli’.

• Wakati huo huo, Wapalestina walitajwa kwa sauti hafifu kwa asilimia 15.7, ya mara walizonasibishwa huku sauti hafifu ikitumika kwa asilimia 6.4 ya mara walizotajwa ‘Waisraeli’.

Jackson alihitimisha kuwa;

“Matumizi ya sauti hafifu-inavunja moyo au kuficha wale wanaochochea vitendo viovu juu ya Wapalestina; hii ina athari ya kejeli ya kupunguza uwajibikaji wa Israeli kwa kusababisha mateso kwa Wapalestina”.

Masomo ya kitaaluma yamethibitisha kuwa utatanishi unatokana na matumizi ya lugha inayoathiri jinsi tunavyotafsiri ukweli.

Uwongo sawia wa Mayahudi wa kuhitajia mahali penye amani baada ya vita vya kwanza vya dunia kumefanya mtazamo wa kitendo cha kuiba na kupokonya ardhi ya mtu mwengine na kuanza kuleta mazungumzo ya amani na mhalifu kama chenye kukubalika. Wazayuni wenye huruma ambao wangepinga wazo hili katika mzozo wowote wa ndani au wa kimataifa. Kama ilivyokuwa wakati wa Iraq ilipovamia Kuwait, au katika Vita vya Falklands kati ya Argentina na Uingereza. Matumizi ya dini yaliyofanywa na Wazayuni na wafuasi wao kuhalalisha kitendo cha kuwafanya mamilioni ya watu kukosa makazi katika nchi zao haichukuliwi kuwa kali au ya ushabiki, lakini inalinganishwa na “kuheshimu haki ya mtu kuabudu na kuwa na elimu sahihi”. Kulazimisha watu wa Gaza kuishi kama wanyama au raia wa daraja la pili, waliozuiwa na ukuta haramu inalinganishwa kwa kirongo na haki ya kulinda taifa dhidi ya magaidi. Kutoa onyo kwa familia kabla ya mitaa yao yote kulipuliwa kwa bomu inalinganishwa na kitendo cha kuheshimu “haki za kibinadamu”.

Mwenyezi Mungu (swt) hatambui uwezekano wowote wa ukweli au haki kutoka kwa watu ambao wana ajenda isiyo ya kweli dhidi ya Uislamu na Waislamu. Na kwa ishara hiyo hiyo Mwenyezi Mungu (swt) katika Quran anatambua kwamba sisi kama Ummah hatuwezi kuviita vitu kimakosa. Tunapaswa kuwa wakweli na waadilifu katika mambo yote.

(لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ)

“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.”  [Al-Mumtahinah 60:8]

Hili linaturuhusu kutofautisha kati ya Wazayuni na Mayahudi; ambao wanaweza kukinzana baina yao.

Huu hakika ni mfano wa jinsi tathmini muhimu ya mambo inapaswa kuongozwa na ukweli na sheria thabiti kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Hatuwezi kudanganywa kuingia katika chuki kwa ajenda za kisiasa au kupigania utaifa au viongozi ambao wanawakilisha mitazamo ya Haramu.

Kuwachanganya watu na usawa wa uongo vyote ni zana za kisiasa za kuupotosha Ummah huu na kusababisha udhaifu juu ya kurejea kwa utawala wa Kiislamu kwa muundo wa Khilafah.

Ikiwa sisi kama Waislamu tunafahamu ujanja na ubabaishaji huu, tunaweza kuweka mazingatio zaidi juu ya utatuzi sahihi kwa kufanya kazi ya ulinganizi kwa njia ya Mtume (saw) kwa kuweka mfumo utakaokomboa ulimwengu kutokana na madhara makubwa ya sheria zilizotungwa na binadamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut tahrir na

Imrana Mohammad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu