- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kuchukua Mafunzo Kutoka kwa Shakhsiya za Watumwa Wawili Watukufu: Bilal (ra) na Wahshi (ra)
Licha ya muda mrefu kupita, baadhi ya hisia na hatma zinafanana, kwa mfano, hatma na hisia za watumwa hawa kutoka zama za Mtume Muhammad (saw) zinafanana na hatma za baadhi ya watu ambao tabia zao zinalingana na utumwa katika uhakika wa leo. Watumwa wa zamani walitekwa nyara na viongozi wa kiqureishi wenye msemo katika jamii ilhali watumwa wa leo wanatekwa nyara na matarajio, matamanio na udhaifu wao wenyewe nk. Utukufu wa watumwa hawa wawili katika zama za Mtume (saw): Bilal ibn Rabah (ra) na Wahshi ibn Harb (ra) ni ule ambao pia twaweza kuupata katika shakhsiya za Waislamu tofauti tofauti leo.
Watumwa wote wawili wana uhalisia sawa. Wote walitekwa nyara kuwa watumwa, lakini Bilal (ra) alikuwa na mtazamo tofauti kuhusu maisha. Lengo lake daima alikuwa amelielekeza katika kumridhisha Allah (swt) pekee, hata awe katika hali ngumu kiasi gani. Alivumilia mateso mengi kwa ajili ya Allah na kujitolea muhanga sana kwa ajili ya dini yake. Lakini Wahshi hakufurahia hali aliokuwa nayo, alitaka kufanya kila njia kujiweka huru kama wengine. Leo, watu wengi wako zaidi ya Wahshi. Hawaridhishwi na maisha yao na wako tayari kufanya chochote kwa ajili ya mabadiliko pasi na kuzingatia radhi za Allah (swt).
Bilal (ra) hakuwa na ujuzi wa maalum isipokuwa aliweza kutamka Iqama vizuri, leo kila Muislamu anamtambua kwa kujitolea muhanga kwake. Ukweli huu kuwa Bilal (ra) hakurudi nyuma katika Imani yake ya kiislamu na kwamba alipata mateso mengi ulikuwa na athari kubwa kwa Maqureishi zama zile. Tabia hii ilikuwa ni ushindi mkubwa kwa uislamu. Leo, maadui wa uislamu hutumia mbinu za mateso za kisiri na za kuhadaa ambapo japo umma unaona maelfu ya waislamu wakifariki, hili aghalabu halina athari sawa kwao kama tamko 'Ahadun Ahad' kutoka kwa Bilal (ra) mjini Makkah,
Sababu ya hili ni kuwa watu wengi wameshindwa kuutazama huu ulimwengu kama makao ya muda tu ambapo wamo katika vita na shetani. Ikiwa twataka kuwa kama Bilal (ra) hatuna budi kujifunza kufanya kila kitu maishani mwetu kwa ajili ya kumridhisha Allah (swt). Huu ni mtazamo wa maisha uliojaa ikhlas usiokuwa na riyah. Maisha ya watu waliojishughulisha na kumridhisha Allah (swt) pekee hayana chuki, uhasidi, kiburi wala huzuni. Lakini suluki mbaya huwatoa watu katika maana halisi ya maisha na kuwafungulia njia ya moto wa jahanam. Ikiwa mtu anafanya kazi kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah, 'mama wa faradhi zote', ni muhimu pia mtu huyu daima azingatie radhi za Allah (swt) na awe na ikhlas katika mambo yote ya maisha yake. Hii ndio tofauti kubwa baina ya watu hawa wawili. Waislamu leo lazima wachague yupi katika ya watumwa hawa wangependa kumuiga. Zama zimebadilika lakini ujumbe ni ule ule.
﴿وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى * وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّى * وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَى * إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّى * فَأَمَّا مَن أَعْطَى وَاتَّقَى * وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَى * فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَى * وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَى * وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَى * فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَى * وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّى * إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَى * وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَى * فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّى * لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى * الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّى * وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى * الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّى * وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَى * إِلَّا ابْتِغَاء وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَى * وَلَسَوْفَ يَرْضَى﴾
((Naapa kwa usiku unapo funika* Na mchana unapodhihiri*Na kwa Aliye umba dume na jike*Hakika juhudi zenu bila shaka ni mbali mbali*Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu*Na akaliswadiki lililo jema*Tutamsahilishia yawe mepesi*Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake*Na akanusha lililo jema*Tutamsahilishia yawe mazito*Na mali yake yatamfaa nini atakapo kuwa anadidimia? Hakika ni juu yetu kumuonyesha uwongofu*Na hakika ni yetu sisi akhera na dunia*Basi nakuonyeni na moto unaowaka*Hatauingia ila muovu kabisa*Aliye kadhibisha na kupa mgongo*Na mcha Mungu ataepushwa nao*Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa*Na wala si kwa kuwa yuko yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa*Ila ni kutaka radhi za Mola wake mlezi aliye juu kabisa*Naye atakuja ridhika)) [Surah Al-Layl]
Allah (swt) anataraji kutoka kwa Waislamu suluki fulani; mtu anaye wasaidia wenzake, mtu aliye na uchaji Mungu, na mtu anaye taraji malipo ya mbeleni kutoka kwa Allah (swt) na kamwe hafadhilishi dunia. Allah (swt) atamfanyia njia nyepesi mtu kama huyo ambaye amelenga radhi za Allah (swt). Ili kuwa kama Bilal (ra), yamaanisha kuyafanya haya kuwa ndio tabia yake. Tabia ni muhimu na ni jambo zuri, lakini Muislamu ajishughulishe katika kuwa na tabia njema zinazo mkurubisha kwa Allah (swt). Hivyo basi, ni bora kwa muumini kuwa mtumwa wa Allah (swt) na kupata ukombozi wa milele peponi, kuliko kuwa mtumwa wa dunia hii hadaifu na matamanio yake na kupata kifungo cha milele motoni.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahri na
Amanah Abed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir