Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Janga la Kiuchumi la Kiulimwengu: Miaka 10 Baadaye

Msimu wa kiangazi wa mwaka wa 2017 ni maadhimisho ya muongo mmoja wa janga la kiuchumi la kiulimwengu. Kampuni ya Lehman Brothers nchini Marekani iliporomoka, masoko ya fedha ya Kiamerika almaarufu kama Wall Street yalianguka na uchumi wa kiulimwengu ukatumbukia katika janga. Trilioni za dola kama mapato zilipotea (dola trilioni 22 za Kiamerika, kwa muda wa miaka mitano), mamilioni ya wafanyikazi waliachwa bila kazi na maelfu ya ahadi zikatolewa na wanasiasa na watunga sera – kila mmoja kuanzia Obama na Gordon Brown mpaka David Cameron na Christine Lagarde – kwamba mambo yatabadilika. Lakini, karibu muongo mmoja baadaye, kinacho shangaza zaidi ni kuwa mabadiliko ni machache. Muongo mmoja huku kukiwa bado kuna kadhia nyingi zilizo sababisha janga hili ambazo hazija tatuliwa, huku wahalifu wake wakipewa uangalizi mzuri na serikali za Kimagharibi kwa kupewa usaidizi wa kifedha (ili kuzuiwa kuporomoka kwa makampuni yao yaliyo feli) na uchapishaji wa pesa.

Uchumi wa nchi kubwa za kiulimwengu unaendelea kujikokota kufikia kudumisha uzalishaji wake, licha ya miaka kadhaa ya kuuamsha kupitia sera za kifedha na matumizi. Uchumi wa nchi nyingi changa pia unakumbwa na changamoto za kimuundo za muda mrefu, zikiwemo deni linalo ongezeka, raia wakongwe, na uhaba au ubovu wa miundo msingi.

Kiasi kikubwa cha pesa duni zilizo tengezwa ziko katika benki kuu ya Amerika ya Federal Reserve, benki kuu ya Uingereza ya Bank of England na benki kuu ya Ulaya ya European Central Bank (ECB) ambazo zimesukumwa na wawekezaji wa kifedha katika masoko yalio na uzalishaji mkubwa ya Afrika Kusini, Brazil na India, miongoni mwa masoko mengine. Wanauchumi katika Bank for International Settlements, ambayo ni benki kuu ya benki kuu, wanaamini kuwa dola trilioni 9.8 za Kiamerika zimetolewa kutoka benki za kigeni kama mikopo na dhamana katika nusu ya kwanza ya muongo huu baada ya Lehman Brothers kuporomoka. Kiasi cha dola trilioni 7 za Kiamerika ya pesa hizo zimelekezwa kwa masoko yanayo ibuka.  

Tangu janga hili la kifedha mnamo 2007, msururu wa hatua za dharura zilichukuliwa sio tu kuokoa uchumi wa nchi za kimagharibi bali kuukoa mfumo mzima wa mabenki. Kulikuwa na tishio la kweli la kusambaa kwa uporomokaji wa mabenki kwa sura ya kudorora kwa uchumi ikitabiriwa kuwa kama 1930. Mabenki yaliinuliwa kwa zaidi ya trilioni 21 za Kiamerika ikifuatiwa na msururu wa sera zisizo za 'kawaida' kutoka benki kuu. Yote haya yaliundwa kuiokoa nidhamu, mabenki na kusababisha uzalishaji katika uchumi wa nchi za kimagharibi. Licha ya hatua hizi zilizo husisha pia uchapishaji wa pesa na upunguzaji wa kiwango cha riba kufikia karibu na sufuri, kupona kwa uchumi katika nchi za Magharibi kunakwenda kwa kasi ndogo yenye uchungu mwingi.

Katika mkutano wa kiuchumi wa kiulimwengu wa kila mwaka jijini Davos, Switzerland kuanzia Januari 20 mpaka 23, 2016 viongozi wa kiulimwengu waliamua kuchochea kwa haraka vita vya kifedha ili kuwarahisishia wao kulazimisha uwekaji wa viwango vibaya vya riba. Suluhisho lao kwa 'tatizo' hili mnamo 2016 lilikuwa ni kuusukuma ulimwengu kugeuka kuwa jamii isiyo tumia pesa moja kwa moja katika miamala yake. Mnamo 2016 benki kuu zilianzisha mpangilio huu kupitia kuondoa noti za viwango vikubwa, ambayo inapelekea miamala mikubwa ya kifedha kutoweza kufanyika. Aliyekuwa Seneta wa Amerika Ron Paul alidokeza: "Jamii isiyo tumia pesa moja kwa moja ni ndoto ya IRS: ni kujua na kudhibiti fedha za kila Muamerika."     

Miongoni mwa matukio muhimu zaidi katika historia ya kiuchumi ya hivi karibuni ni kufichuka kwa stakabadhi milioni 11.5 zinazo onyesha shughuli za kila siku za kampuni ya sheria ya Mossack Fonseca mnamo 2016 ambayo iliyashauri makampuni makubwa ya kiulimwengu, madikteta, wafalme pamoja na viongozi waliochaguliwa kidemokrasia juu ya jinsi ya kuficha pesa zao na kukwepa ushuru.

Tukio hili kwa mara nyengine tena ladhihirisha, kupitia utajiri huu mkubwa wa ushahidi, kuwa huku wengi ulimwenguni wakilazimishwa kwa nguvu kulipa ushuru mkubwa, matajiri na watawala hulipa kiasi kidogo tu kupitia akaunti zao za ng'ambo. Matokeo makubwa ya ufichuzi huu yatakuja pale ufichuzi huu utakapo fichua mabenki na nidhamu ya fedha. Sio siri kuwa utajiri mkubwa umefichwa katika hazina za ng'ambo takwimu zikikadiria kuwa rasilimali zilizofichwa ni asilimia 8 ya utajiri wote wa kifedha wa kiulimwengu ambapo mbeleni hatukuwahi kupata maelezo haya. Na kadhia hii ya utajiri wa ng'ambo ni ishara tu ya saratani kubwa. Pengo kati ya matajiri na masikini umeendelea kukua kwa miongo, na pesa hizi nyingi zilizoko ng'ambo ni ishara ya mtindo huu.

Serikali za kimagharibi zilijiokoa kutokana na mporomoko wa kiuchumi kupitia kuzisaidia kifedha benki zilizo sababisha janga hili. Ufadhili huu ulifanywa kupitia kukata bajeti za serikali na kupunguza ufadhili kwa wasio jiweza katika jamii chini ya kisingizio cha 'sote tumo ndani ya janga hili kwa pamoja'. Waliziba nyufa tu na kuendelea kulingania mfumo wao ulimwengu mzima. Wanaendelea kuwasilisha mfumo wao kama suala nyeti katika kutatua ufukara na deni la kiulimwengu, licha ya kuwa mfumo wao huo huo ndio uliosababisha janga hili la kiuchumi la kiulimwengu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:29

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu