- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Risala Tatu kwa Maafisa wa Jeshi Tukufu la Pakistan
(Imetafsiriwa)
Muundo wa nguvu za kiulimwengu hivi leo uko katika hali ya mabadiliko, kukiwa na mfungamano wa nguvu na miungano inayochukua sura kote duniani na ambapo Wamagharibi wanaondoshwa kutoka nafasi yao ya uongozi duniani. Wakati huo huo Ummah wa Kiislamu ukichemka kwa mwamko wa hamasa ya Kiislamu na kuongezeka ghafla kwa vijana wanaohitajia mabadiliko – muda sasa wa maamuzi ya kivitendo ya kusimamisha mfumo mpya wa kiulimwengu kwa muundo wa dola ya Khilafah ya Kiislamu hivi sasa.
Ni jukumu lenu kuona kwamba kutawala kwa Uislamu kunadhihiri, kuona kwamba Khilafah Rashidah ya pili inasimamishwa, ambapo Hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) katika mambo yote zinatekelezwa na kukamilishwa kote katika jamii. Kwa kuliwezesha hili, Hizb ut Tahrir imetengeneza mwongozo kwa ajili ya dola hiyo na imechambua kwa undani namna mfumo huo utakavyofanya kazi katika idara zake tafauti; kiuchumi, kisheria, kijamii, utawala nk. na kukubalika na Waislamu wengi wenye uwezo, wakweli na wasomi kulibeba jukumu hili, katika Pakistan na duniani kote.
Kwa kuzingatia hili, sisi katika Hizb ut Tahrir tunatoa wito kwenu, maafisa katika jeshi la Pakistan, kuitikia wito na kupiga hatua mbele ya kutekeleza jukumu lenu la Kiislamu, kama walivyokuwa viongozi wa makabila ya Aws na Khazraj katika Madina walivyolinganiwa na kuitikia wito kwa kupiga hatua mbele kumnusuru Mtume (saw) katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu na kwa kufanya hivyo wakawa ni Maanswar.
Kivitendo ni juu yenu sasa kutoa utiifu wenu na msaada wa nguvu (Nusra) kwa Hizb ut Tahrir, ili Khilafah iweze kusimamishwa kivitendo katika Ummah, ikiwa Pakistan ndio nukta yake kianzio, bila kuchelewa. Kwa kutekeleza hayo, Uislamu lazima uendelee pale uliposimamia, kama gurudumu la kusagia kukabiliana na ukafiri na mfumo dhalimu uliopo duniani, ambapo haki inapambana na batili, na kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, itashinda na kuwa juu.
(جَاء الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا)
“Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke.” [Al-Isra 17:81]
Kwa upekee kabisa, sisi katika Hizb ut Tahrir tunakuleteeni risala tatu ili mtilie maanani na kufaidika katika maisha haya na yajayo:
Kwanza – Kuwa maafa, vilio, dhulma ambayo inaendelea bila kupingwa dhidi ya wanyonge, wasioweza kujilinda, waliozongwa na ufukara na mfano wake katika Ummah huu viko juu ya mabega yenu.
Mnawajibika kwa maumivu yao. Mnahisabiwa kwa machungu yao. Suala hili liko mlangoni kwenu, katika miguu yenu. Ni tatizo lenu na mtahisabiwa moja kwa moja kwa hilo. Kwa sababu mnayo njia halisi ya kusitisha masumbuko yao, na muda wa kuwa hamjawa tayari kuliendea hilo, lawama za majaaliwa yao yako kwenu kwa kuwa mmechagua kutotenda juu ya kutenda.
(وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا)
“Na mna nini msipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa, wanaume na wanawake na watoto ambao husema: Mola mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anayetoka kwako." [An-Nisa 4:75]
Mwenyezi Mungu (swt) ameweka wazi kuwa Yeye ndie mwenye kuwashinda watenda uovu, lakini tafauti na mataifa yaliopita ambapo Mwenyezi Mungu (swt) aliwateremshia adhabu moja kwa moja, hivi sasa ni wajibu juu ya waumini kuchukua hatua dhidi ya watenda maovu.
(قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ)
“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya waumini.” [At-Tawbah 9:14]
Pili – Ni kuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) iko wazi juu yenu pindi hamkuitikia wito.
(أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ)
“Je! Wakati haujafika bado kwa walioamini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyoteremka? Wala wasiwe kama waliopewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu.” [Al-Hadid 57:16]
Kama hamjatilia maanani maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), basi tambueni kuwa Mwenyezi Mungu (swt) atakufuteni na kuweka watu wengine badala yenu ambao sio tu wataamini bali wataitikia wito Wake; haya ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu (swt).
(إِلاَّ تَنفِرُواْ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلاَ تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)
“Kama hamuendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawbah 9:39]
Msiwe na shaka kwa kipindi kifupi Mwenyezi Mungu (swt) anaweza kuirusha milima mikubwa ikakusageni, au akatia aina ya kitu kidogo sana ndani ya mapafu yenu na kuondosha pumzi zenu. Hayo ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu (swt).
Ni hakika kwamba mpo katika kipeo cha njia panda mkiwa na maamuzi mazito sana ambayo lazima muyafanye. Bila shaka ni maamuzi yenye athari kubwa ya kuamua njia ya maisha yenu katika dunia hii. Lakini kubwa zaidi, yataamua njia mnaoichukua katika maisha yajayo, ambayo ni ya kudumu milele. Hivyo maamuzi yenu lazima yafanyike kwa maslahi mazuri ya maisha ya baadaye, na sio kwa maisha haya mafupi ya kupita. Lazima muangalie mbali zaidi ya vidokezo vingi vya maisha haya; hamu ya kupata mali, kugombania maslahi ya biashara, kuongeza utajiri wenu, kukuza familia – yote hayo si chochote bali ni starehe za kushughulisha tu.
(يَا قَوْمِ إِنَّمَا هَذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَإِنَّ الْآخِرَةَ هِيَ دَارُ الْقَرَارِ)
“Enyi watu wangu! Hakika haya maisha ya duniani ni starehe ipitayo tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima.” [Ghafir 40:39]
Ni lazima muakisi imani zenu kwa kuupa uwazi uoni wenu. Uamuzi wenu lazima uwe kwamba, nyinyi mukiwa Waislamu mnawajibika kwa Mwenyezi Mungu (swt), msichague kumtii yeyote isipokuwa Muumba wenu, muwatupe kando wakubwa wenu wanaokuamrisheni kutomtii Mwenyezi Mungu (swt) kwa kukufungieni kwenye gurudumu kutetea mfumo wa kiulimwengu wa kikafiri, ambao hauongezi chochote isipokuwa kuuvuruga Ummah wa dunia hii, Waislamu na wasio Waislamu.
(وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا)
“Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio waliotupoteza njia.” [Al-Ahzab 33: 67]
Tatu – Mwisho, ukiwa ni mfano wa kuvutia, tunakufikishieni kwenu kutoka kwa Swahaba Mkubwa Ayub Al Ansari (ra) – Swahabah aliyebarikiwa na kuheshimiwa kwa kuwa ndiye ambaye Mtume Muhammad (saw) aliishi naye Madina baada ya Hijra.
Alifariki akiwa mwenye umri mkubwa kwenye masafa ya mbali nje ya milango ya Konstantinopoli (Istanbul) ambako alizikwa, uliokuwa mji mkuu wa Himaya ya Roma Mashariki, moja ya dola kuu za dunia wakati huo ambayo Khilafah ya mwanzoni iliwashinda. Hata katika umri huo mkubwa hakupumzika wala hakuridhika kubaki Madina, bali alijumuika na Waislamu katika kampeni ya kijeshi ya masafa ya mbali ili kuikomboa ardhi mpya na kutanua milki ya Uislamu. Alipokaribia kukata roho, aliwaagiza askari kumsogeza mbele zaidi iwezekanavyo na kumzika katika milango ya Konstantinopoli na kwa hilo kuwapa salam majeshi ya Waislamu. Ni kwa maamkizi haya kutoka kwa Ayub Al Ansari (ra), mmoja ya maswahaba wa karibu na kipenzi cha Mtume Muhammad (saw) ndio nasi tunayafikisha kwenu, majeshi ya leo yenye kuogopwa; “Assalamu ‘Alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu”.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohamed Asif