- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Sarah Everard Amefelishwa na Mfumo
(Imetafsiriwa)
Inaweza kuwa kwa yeyote kati yetu wanawake - lakini alikuwa ni Sarah Everard, msichana mdogo kutoka London ambaye aliuawa kinyama na polisi mkatili PC Wayne Couzens.
Jioni ya Machi 3, 2021, Couzens alitumia kadi ya msako ya Polisi wake wa Metropolitan na pingu kumteka nyara Bi Everard chini ya kisingizio cha kumkamata, wakati alipokuwa akitembea kuelekea nyumbani kwake akitokea kwa rafiki yake huko Clapham, London kusini.
Huku Sarah akiwa ameingizwa katika gari lake aliendesha kwa maili 50 kabla ya kumbaka na kumnyonga hadi kufa. Siku kadhaa baadaye Couzens akauchoma mwili wake katika harakati za kujaribu kuficha ushahidi.
Huku maelezo ya uchunguzi wa Polisi yakiibuka wakati wa kesi wiki hii, kilio cha umma kilielekea kwa jeshi la polisi wa Metropolitan kwa orodha ya kufeli kulikofanywa wakati wa uchunguzi wa mauwaji hayo.
Kushindwa kunako akisi taasisi:
Kesi hiyo ilifichua kwamba Couzens afisa wa ulinzi wa kidiplomasia aliyekuwa nje ya majukumu yake, anaye hudumu katika ubalozi wa Amerika alikuwa amehusishwa siku mbili tu kabla ya mauwaji ya Sarah katika tuhuma mbili za matukio ya udhalilishaji, na pia tukio la hapo awali la udhalilishaji la mnamo 2015.
Kwamba matukio haya 'yalisahaulika' kwa urahisi na wapelelezi, ni ushahidi mpana wenyewe dhidi ya jeshi la polisi la Kent na Metropolitan, ambao walishindwa kuelewa kwamba tabia hiyo potovu inahitaji tahadhari kubwa na kwamba mnyanyasaji huyo wa kijinsia angekuwa tayari amekamatwa na kuhukumiwa.
Kuongeza katika uzembe huu wa wazi, kesi hiyo pia ilifichua kwamba Couzens, alikuwa kwenye kikundi cha WhatsApp na maafisa wengine watano wa polisi ambao kwa sasa wanachunguzwa na Afisi Huru ya Maadili ya Polisi (IOPC) kwa utovu wa nidhamu. Mahakama ilisikia kwamba kwa pamoja walitumiana ujumbe wa “kibaguzi” ikiwa ni pamoja na “maudhui ya udhalilishaji wanawake”. Angalau watatu kati yao wanakabiliwa na uchunguzi wa makosa ya jinai chini ya kifungu cha 127 cha Sheria ya Mawasiliano, ambayo inahusu vitu ambavyo “vinaudhi sana au za tabia mbaya, za aibu au zenye kutisha”.
Kana kwamba inahitaji uthibitisho zaidi wa tabia mbaya za Couzens, na wenzake walikiri mahakamani kwamba alipewa jina la utani kama “mbakaji”.
Kwa kuzingatia mapungufu yasiopingika ya taasisi, wakuu wa polisi na serikali imetia mkazo sana katika kurejesha imani ya umma kwa jeshi la polisi. Hii sambamba na kusisitiza kwa kuchukua tahadhari za kiusalama ambazo ni pamoja na kutotembea peke yako baada ya giza kuingia au kutumia vipokea sauti vya sikioni (headphone), kukaa katika maeneo yenye taa nyingi, kutuma ujumbe kwa marafiki wako mahali ulipo, kuvaa nguo nyeusi na kubeba funguo mikononi mwako kama silaha.
Walakini, kutokana na kwamba mauaji kadhaa hivi karibuni yalitokea ambapo wanawake, pamoja na dada Bibaa Henry na Nicole Smallman waliuawa kikatili kwa pamoja katia eneo la umma lenye mwanga, na Sabina Nessa akiwa amevaa nguo zenye rangi nyeusi, ushauri huu wa usalama sio tu kuwa una makosa, hauingii akilini kabisa. Inaachia mzigo wa usalama kwa wahanga peke yao, bila hata kuchunguza sababu za uhalifu wa kikatili, uhalifu wa kijinsia au kuhoji kwa nini ukatili kama huo unazidi kuenea katika jamii inayoitwa endelevu na iliyostaarabika.
Inaeleweka maumivu ya jumla wanayohisi wanawake na kupotoshwa kwa uchunguzi kumechochea kizazi kingine cha wanawake wenye nia ya kupinga mitazamo iliyopo dhidi ya unyanyasaji wa wanawake na usalama. Kwa hivyo katikati ya mikesha na maandamano, ‘Rejesha Usiku’, harakati za miaka ya 70 zilizochochewa na muuaji Peter Sutcliff, kauli za ukomavu, zimewashwa upya tangu Kifo cha Sarah. Kwa hivyo, kauli iliyoshika kasi kwa sasa katika umma ni juu ya udhalilishaji wa wanawake ndani ya jeshi la Polisi, ubaguzi wa wanawake, taasubi sumu za kingono na kufukuzwa vibaya kwa wapotoshaji. Kama vile Kamishna wa North Yorkshire Philip Allott ambaye alizua ghadhabu aliposema Bi Everard “kamwe asingejisalisha” kukamatwa na muuaji wake!
Hata hivyo, kile kinachokosekana kwenye majadiliano haya muhimu sana ni mtazamo kamili juu ya maingiliano ambayo wanaume na wanawake watashiriki katika jamii na jinsi utawala halisi unavyoonekana. Hii ni muhimu kwa sababu taasubi jumla juu ya wanawake kati ya jamii pana ni dhahiri utaathiri maafisa wa polisi, ikizingatiwa kuwa wao pia ni sehemu ya jamii hiyo.
Taasubi:
Inatambuliwa sana kuwa taasubi sumu kwa wanawake zimeenea katika jamii zote za kiliberali, na hizi hulelewa sana kupitia thaqafa ya Pop na tasnia ya burudani, ambayo sasa inajumuisha mitandao ya kijamii na mipango ambayo njia zote za uhuru wa kibinafsi zinaonyeshwa.
Vivyo hivyo uliberali ndio lengo la mkakati wa kila nidhamu ya kidemokrasia, na kadri malengo ya maadili na adabu yanavyoendelea kubadilika, zaidi ya hapo kabla watu kuepuka kuwajibika kwa tabia zao. Kwa njia hii mara fikra hatari, zimekuwa kanuni za kijamii ambazo kwa kawaida huenea katika sehemu zote za jamii ikiwa ni pamoja na taasisi za kiraia na hata serikali. Kwa njia hii, kwa wengi sana, punde maisha yatakuwa mafupi zaidi kushinda bahati nasibu kati ya mwathirika wa tabia mbaya na aliyeepuka.
Uislamu kama mfumo mbadala:
Uislamu ni nidhamu mbadala ya ile jamii ya leo ya kisekula kwani unashughulikia wanaume na wanawake kwa utaratibu. Sheria za Mwenyezi Mungu ambazo Waislamu wanazifuata kuhusiana na maingiliano baina ya wanaume na wanawake katika maisha jumla na maisha binafsi zimepangwa na Mwenyezi Mungu (swt) mwenyewe.
Sheria zinazohusiana na taratibu za mavazi, kutenganishwa kwa jinsia tofauti katika mazingira mbali mbali pamoja na kibali cha kufanya maingliano kwa uhuru wakati inapolazimu. Pamoja na tabia zilizopendekezwa ambazo zinafaa zaidi kwa heshima ya umbile letu la kibinadamu tulilopewa na Mungu. Hizi ni baadhi tu ya viwango vya kiuungu ambavyo vinatupa maarifa juu ya hadhi ya heshima na thamani ya mwanamke. Maadili ya Kiislamu yanaonyesha thamani ya kila mwanamke, mzee au mchanga, bila kujali hali yake ya kijamii, utajiri, mwili au uwezo wake.
Kwa hivyo, uhalifu wowote dhidi ya mwanamke katika jamii ambayo anachukuliwa kuwa wa thamani sana bila shaka utazingatiwa kwa umakinifu zaidi – na uzito wa uhalifu huo utaakisiwa na hatua zitakazochukuliwa na mamlaka dhidi ya wahusika.
Hii inaonyeshwa na mfano wa mpendwa wetu Mtume Muhammad (saw) wakati alipozingira ngome ya Banu Qaynuqa kwa siku kumi na tano, baada ya dhulma ya Mwanamke wa Kiislamu ambaye Muislamu aliyetokea kumsaidia aliuawa. Vivyo hivyo mnamo 88 Hijria wakati Muhammed bin Qasim alipotumwa na Hajjaj bin Yusuf kumuokoa mwanamke wa Kiislamu iliyotekwa nyara na maharamia huko Sindh, thamani ya mwanamke na jukumu la serikali vilianzishwa kikamilifu kama kiwango cha dhahabu cha sheria adilifu.
Ni kwa kurudi kwa Khilafah (Ukhalifah) kwa njia ya Utume katika nchi za Waislamu ndipo wanawake watathaminiwa na kuwa salama, na kuweza kutarajia haki kutoka kwa wale walio na mamlaka juu yao. Uislamu ndio mfumo pekee ulio na nidhamu fafanuzi ya kijamii inayoweza kutunza uhusiano kati ya wanaume na wanawake. Kuwatoa wanadamu kutoka kwenye giza la tamaa za kibinafsi na tabia ya sumu, kuwaingiza kwenye nuru ya usalama na uadilifu kwa wote.
Allah (swt) asema katika Qur-an,
(وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَـئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ)
“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” [Surah At-Tawbah: 71].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Maleeha Fahimuuddin