Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uavyaji Mimba Nchini Amerika

(Imetafsiriwa)

Haki za uavyaji mimba nchini Amerika zinajadiliwa tena zikikita kambi maeneo ya Texas ambayo imeweka sheria ambayo itawazuia wanawake kutoa mimba baada ya kufika wiki 6. Mbali na kikomo cha muda, kipengele kingine chenye utata cha sheria hii ni ruhusa kwa raia binafsi, kinyume na watumishi wa serikali, kuleta kesi dhidi ya wale wanaofanya uavyaji mimba. Watu hawa wamesema, na hii kimsingi “huunda mfumo wa haki kinyume cha sheria ambao ndani yake mtu yeyote anaweza kuleta kesi dhidi ya waavyaji mimba wanaotuhumiwa kwa kukiuka marufuku hiyo.” [Chanzo: Washington Post].

Mahakama kuu ya Amerika haikuzuia sheria hii. Hii imepelekea kwenye mjadala juu ya haki za utoaji mimba kote Amerika, na kama sheria ya Texas inamaanisha kuwa “kuna wengi wanaofanya kazi mahakamani walio tayari kuifuta Roe V Wade.” [Chanzo: BBC]

Roe V Wade ni uamuzi wa Mahakama kuu ya Amerika tangu 1973, ambayo ilipiga chini sheria ya Texas iliofanya uavyaji mimba kuwa kosa la jinai na ilitambua haki za wanawake za kuisitisha mimba. (Chanzo: Dallas News). Mahakama iliamua kwamba Katiba ya Amerika inalinda uhuru wa mwanamke wa kuchagua kutoa mimba na, matokeo yake, iliwaruhusu wanawake “kuwa na haki za kikatiba zisizofungwa kwa kitendo hicho wakati wa miezi yao mitatu ya kwanza (wiki 12) ya uja uzito.” (Chanzo: BBC). Mahakama mara hii imejitenga na haki hiyo, ikiimarisha sheria za utambuzi wa ndoa na wazazi na kuruhusu udhibiti mkubwa wa waavyaji mimba, lakini kwa kiasi kikubwa sheria hiyo imeugwa mkono. (Chanzo: BBC).

Katika kukabiliana na upingwaji wa Mahakama Kuu katika kuizuia sheria ya Texas, Nyumba ya Wanademokrasia (Democrats) imeweka mbele mswada ambao umeweka mahala pake haki za kutoa mimba na kupangilia kuilinda Roe V. Wade. Mswada huu “ungeweza kuwapa wagonjwa haki ya kutoa mimba bila ya vipimo au taratibu za kitabibu zisizo za lazima – kwa ujumla inaeleweka ni pamoja na sonografia kali (ultrasound), ushauri au vipindi vya lazima vya kusubiri.”  Mswada huo pia “ungezuia majimbo katika kulazimisha uhudhuriaji wa kliniki ya mtu kabla ya kutolewa mimba, mara nyingi hujulikana kama hitajio la “safari-mbili”. Mswada huo pia ungezuia majimbo katika kukataza utoaji mimba wowote kabla ya uhai wa kijusi na kuzuia katazo la utoaji mimba baada ya uhai wa kijusi ikiwa, ni kutokana na imani-nzuri ya maamuzi ya mwisho ya watoa huduma za afya, kuendelea kwa ujauzito kunaweza kuhatarisha maisha au afya ya mgonjwa mjamzito.” (Chanzo: CNBC)

Hesabu ya mwisho katika baraza hilo ilikuwa 218 kwa 211: Kiuhalisia hakuna Mwanajamhuri (Republican) yeyote aliyeipigia kura, na ilipita kwa kuungwa mkono na Wademokrasia (Democrat) wa Nyumba moja tu. (Chanzo: MSNBC). Lakini wakati inapitishwa kwa nyumba hiyo hilo halimaanishi kuwa ndio itakuwa sheria. Kama inavyotarajiwa kwamba Mswada huo “utakabiliwa na upinzani mno kutoka seneti ya Wanajamhuri (Republicans) na hautarajiwi kusonga mbele kupitia baraza hilo.” (Chanzo: CNBC)

Kama sheria hii itakuja kufanya kazi, ingeifanya Amerika “moja ya nchi chache duniani – pembezoni mwa China na Korea Kaskazini – katika kuruhusu chaguo la uavyaji mimba mpaka kujifungua,” na matokeo yake, ingeondoa ulinzi wote wa maisha ya ambaye hajazaliwa. (Chanzo: Dallas News)

Idadi ya uavyaji mimba nchini Amerika iko juu kupita maelezo. Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa 2013, zilikuwepo nchi 9 tu ambazo zina kiwango cha juu cha uavyaji mimba kilichoripotiwa kuliko Amerika: Bulgaria, Cuba, Estonia, Georgia, Kazakhstan, Romania, Urusi, Uswidi, na Ukraine.

Kila mwaka, karibu nusu ya mimba zote miongoni mwa wanawake wa Amerika ni zisizokusudiwa. Karibu nusu ya mimba hizi zisizopangwa, milioni 1.3 kila mwaka, huishia kwa kutoa mimba. (Shirikisho la Kitaifa la Uavyaji Mimba)

-Wanawake wengi wanaopata mimba (83%) hawajaolewa; 67% hawajawahi kuolewa, 16% wametengana, wametalikiana, au wajane. (Shirikisho la Kitaifa la Uavyaji Mimba)

-Wanawake wanaoishi na wenza ambao hawajaolewa nao wanachangia 25% ya utoaji mimba (Abort).

 

-Wanawake walioolewa wana uwezekano mdogo sana kuliko wanawake ambao hawajaolewa katika kutatua mimba zisizotarajiwa kwa kutoa mimba. Mwaka 2018, 4% ya mimba kati ya wanawake walioolewa ziliishia kwa kutoa mimba. (Abort).

Kutokana na takwimu, takriban 88% ya utoaji mimba hupatikana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito. Na zaidi ya nusu ya utoaji mimba wote hupatikana ndani ya wiki nane za kwanza. (Shirikisho la Kitaifa la Uavyaji Mimba)

Mstari wa sasa wa hoja ni kwamba sheria ya Texas inaondoa haki ya kikatiba ya mwanamke kutoa mimba, ambayo ni yenye madhara hasa kwa wanawake katika kesi kama vile za ubakaji. Lakini ushahidi wa takwimu unaonyesha idadi ya mimba zinazotokana na ubakaji ni ndogo. Kama ilivyo kwa idadi ya utoaji mimba unaotokana na matatizo ya kiafya. Kwa ujumla, wanawake wanaoteseka kutokana na ujauzito kupitia mashambulizi na masuala ya matibabu ni 7.5% tu. Utoaji mimba mwengine ni matokeo ya fikra za Kimagharibi za ubinafsi na uhuru, au kushindwa kwa Wamagharibi katika kutoa usalama wa kifedha, na msaada wa kihisia na wa kifamilia kwa watu.

Mwaka 2004, taasisi ya Guttmacher bila kujitambulisha iliwahoji wanawake 1,209 baada ya kuavya mimba kutoka kliniki tisa tofauti za uavyaji mimba kote nchini. Kati ya wanawake waliohojiwa, 975 walitoa sababu ya msingi ya kutoa mimba. Jedwali hili linaorodhesha kila mojawapo ya sababu na asilimia ya wahojiwa walioichagua.

                                          Asilimia   Sababu                                                                                      
 ˂0.5%  Mwathirika wa Ubakaji
 3%  Matatizo ya afya ya Kijusi
 4%  Matatizo ya afya ya Kimwili
 4%  Inaweza kutatiza elimu au kazi
 7%  Hajakomaa vya kutosha kulea mtoto
 8%  Hataki kuwa mama mlezi bila baba
 19% Amemaliza kupata watoto 
23% Hawezi kumudu mtoto
25% Hayuko tayari kupata mtoto
6% Nyenginezo

Haki za Binadamu zenye Kasoro: Mama dhidi ya Mtoto

Hoja iliyotolewa na wanaounga mkono uavyaji mimba ni kwamba haki ya uavyaji mimba ni haki ya msingi ya binadamu.

“Hii inahusu uhuru. Inahusu uhuru wa wanawake kuwa na chaguo kuhusu ukubwa na nyakati za kuwa na familia zao, hii haiwahusu watu katika mahakama [kuu] au wanachama wa Congress,” Spika wa Bunge alisema. (CNBC)

Hoja yao ni kwamba “sheria ya haki za binadamu inaelezea wazi kwamba maamuzi juu ya mwili wako ni yako peke yako – hii ndio inayojulikana kama kujitawala kimwili. Kulazimisha mtu kubeba ujauzito usiohitajika, au kuwalazimisha kutafuta utoaji mimba usio salama, ni ukiukaji wa haki zao za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki za faragha na kujitawala kimwili.” (Amnesty International)

Upande mwengine wa hoja hii ni kwamba kulinda haki hii kwa ajili ya akina mama huondoa haki kutoka kwa mtoto ambaye hajazaliwa. Mtoto ambaye hajazaliwa hawezi kujilinda mwenyewe, na kwa hivyo inahitaji serikali kuingilia kati na kupitisha sheria ili kuhakikisha haki hizi za binadamu pia zinatumika kwa kijusi.

Lakini ikiwa lengo ni kumlinda mtoto, basi sheria pekee haitahakikisha hilo kama ushahidi unavyoonyesha kwamba kupiga marufuku uavyaji mimba hakupunguzi hilo. Ndani ya Amerika kabla ya Roe V. Wade, inakadiriwa wanawake milioni 1.2 wa Amerika walitoa mimba kinyume cha sheria kila mwaka. (NBC News) “Takwimu za kihistoria na za kisasa zinaonyesha kwamba sehemu ambayo utoaji mimba ni kinyume cha sheria au imezuiliwa vikali, wanawake hutumia njia zisizo salama kukomesha ujauzito usiohitajika… Leo, takriban wanawake milioni 21 kote ulimwenguni wanapata utoaji mimba usio salama, wa kinyume na sheria kila mwaka.”

Kati ya 2006 na 2015, kiwango cha utoaji mimba cha Amerika kilipungua kwa 26%. Sababu kubwa za kushuka sio sheria kali za utoaji mimba – ni upatikanaji uzazi wa mpango bora. (Vox)

“Pindi dawa za kuzuia mimba zikiwa hazipatikani, wanawake hutumia uavyaji mimba, hata kama haujaidhinishwa kisheria na hata kama unawaweka katika hatari kubwa ya kimwili,” Diana Greene Foster, profesa msaidizi katika Chuo kikuu cha California San Francisco anayesomea uavyaji mimba, aliiambia Kliff 2016. “Pindi dawa za kuzuia mimba zinapopatikana zaidi, matumizi ya uavyaji mimba hupungua.”

Lakini wakati kiwango cha uavyaji mimba kinapungua, utaratibu unabaki kuwa wa kawaida. Hii ni kwa sababu jamii ya Kisekula inahamasisha mahusiano kati ya watu ambao hawajaoana na mimba mara nyingi ni matokeo yasiyotarajiwa. Wakati uzazi wa mpango unaweza kupelekea uzuiaji, mtindo wa maisha unaohimizwa mara nyingi hupelekea uzazi wa mpango kutotumika au kushindwa na utoaji mimba umekuwa mbadala unaokubalika; bila kujali athari kwa watu binafsi au jamii kwa ujumla.

Kwa hivyo, kwa nini serikali inalifanya jambo hili kuwa mjadala?

Cha ajabu, CNBC iliripoti kwamba Sheria ya Ulinzi wa Afya ya Wanawake “inaweza kuwapa Wanademokrasia (Democrats) nishati katikati mwa muhula wa 2022 na hoja yenye nguvu kwa wapiga kura wanaotazama uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama kuu kama haki zinazomomonyoa wengi walioamini kuwa ni sheria iliotulia.”

Je, hii ni kuhusu haki za mtu binafsi na uhuru, au ni kuhusu kuhakikisha vyama vinapata kura wanazozihitaji katika muhula wa katikati?

Hoja hii inathibitishwa zaidi na ukweli kwamba mgawanyiko juu ya haki ya kutoa mimba una upendeleo mkubwa, kwa kukaribia nusu -asilimia 53- ya watu waliosema wao ni Wanajamhuri (Republican) wangependa kuiona Roe V Wade ikipinduliwa, huku asilimia 81 ya Wademokrasia (Democrats) na asilimia 73 ya Waliohuru (independents) wanaitaka iwepo. (NBCnews)

Hali hii ni dosari ya sheria iliyotungwa na mwanadamu

Uwiano kati ya haki za mtu binafsi na uingiliaji wa Serikali ni ule ambao daima huzigawanya jamii za kisekula, na ni kiashiria cha wazi kwetu kwamba kuipa nguvu kuu sheria iliyotungwa na mwanadamu sio suluhisho la matatizo ya binadamu.

Sheria iliyotungwa na mwanadamu ina kasoro; Sayansi inaendelea, mawazo yanabadilika, maoni ya watu hubadilika kulingana na manufaa na dhurufu. Kwa hiyo, majadiliano kuhusu mawazo ya utoaji mimba yote yana dosari- isipokuwa tukirejelea kwenye Uislamu na sheria ambayo Muumba wetu ametupa.

Katika Utawala wa Kiislamu, kusingekuwa na mjadala na hakuna mgongano kati ya haki za kijusi na za mama. Haki hutolewa na Uislamu, na haziwezi kuondolewa kutokana na mabadiliko ya mazoea ya kitamaduni au manufaa ya watu.

Sheria ya Kiislamu imepanga haki za kijusi; mara tu roho ya mtoto inapopuliziwa ndani yake katika siku ya 40, utoaji mimba ni haramu, isipokuwa kama kuna dharura ya kutishia maisha ya mama (ambayo inathibitishwa na daktari mtendaji wa Kiislamu). Baada ya kipindi hiki cha muda, kijusi hupewa haki chini ya Sheria ya Kiislamu na ana pesa ya damu (diya) inayohusishwa na maisha yake ndani ya sheria za mahakama za Kiislamu.

Hoja zingine zote, zilizotengenezwa katika mfumo wa sasa wa kisekula, ni matokeo ya dosari katika imani na jamii yao. Badala ya kuzingatia hili kama suala la mtu binafsi, ieleweke kwamba matendo ya mtu binafsi huathiri jamii na suala la uavyaji mimba linapaswa kuchambuliwa kama suala la jamii. Mfumo wa Uislamu umepanga mahusiano kati ya mwanamume na mwanamke na ubebaji mimba hutokea ndani ya taasisi ya ndoa, kumhakikishia mtoto ana kitengo imara cha kumlinda na kumlea.

Imehadithiwa na An-Nu’man bin Bashir: Mtume (saw) amesema,

«مَثَلُ الْقَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّهِ وَالْوَاقِعِ فِيهَا كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلَاهَا وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا فَكَانَ الَّذِينَ فِي أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنْ الْمَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ فَقَالُوا لَوْ أَنَّا خَرَقْنَا فِي نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا وَإِنْ أَخَذُوا عَلَى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا وَنَجَوْا جَمِيعًا»

“Mfamo wa mtu anayeshikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu na mtu mwenye kuikiuka ni kama mfano wa watu waliopanda safina. Baadhi yao wakawa wako sehemu ya juu na baadhi yao wakawa wako sehemu ya chini; wale walio sehemu ya chini wakitaka maji hupanda kwa walio juu yao, (kwa kuchoshwa) wakasema, lau kama tutatoboa sehemu yetu (tutapata maji kiurahisi) na hatutawasumbua tena walioko juu yetu. (Walioko juu) wakiwaacha (walioko chini) wafanye wanayotaka kufanya, wataangamia wao na wote kwa jumla, lakini wakiwazuia kwa mikono yao (wasitoboe) wataokoka wao na wote kwa jumla." (Sahihi Bukhari)

 Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu