Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mpango wa Amerika Kuhusiana na Burudani na Vyombo Vyetu vya Habari

(Imetafsiriwa)

Kuhalalisha Fikra Chafu kupitia Burudani na Vyombo vya Habari

Vipindi vya televisheni vya Amerika na maigizo ya tamthilia, mwanzoni vilionekana kama vitu visivyo na madhara katika kujiburudisha. Hata hivyo taasisi za kiserikali za kimagharibi zinatumia burudani ili kuleta ushawishi wa kifikra na kisiasa hasa dhidi ya Ulimwengu wa Kiislamu. Burudani huathiri akili, huhalalisha fikra potovu na mitazamo ya kigeni na kuifanya ya kawaida. Hivi karibuni kumehalalishwa fikra chafu katika jamii kama vile suala la unywaji pombe, matumizi ya madawa, uasherati, uzinzi na ushoga vimedogoshwa kwa msaada wa tasnia ya burudani na vyombo vya habari. 

Uhalalishaji wa Ushoga

Hollywood imekuwa mstari wa mbele katika kuhalalisha ushoga, huku ikizipa filamu zake mguso wa vichekesho au msisimko, kama vile “The Eternals,” “Brokeback Mountain” au “I Now Pronounce You Chuck and Larry.” kuhusu televisheni, kipindi maarufu sana cha Friends Sitcom kilirusha matangazo ya harusi ya watu wa jinsia moja, tarehe 18 Januari 1996, wiki tano tu baada ya kipindi cha Sitcom Roseanne kufanya hivyo. Kulikuwa na shutma za awali ndani ya Amerika. KJAC-TV huko Port Arthur, Texas na WLIO huko Lima. Ohio ilikataa hata kuonesha tukio hilo. Hata hivyo, baada ya muda, tukio hilo lilichangia wimbi ambalo lilisababisha mabadiliko katika sheria, vyombo vya habari na elimu. Sasa ndoa za watu wa jinsi moja zimehalalishwa na kuna juhudi za kuhalalisha kujamiiana baina ya wanandugu (maharimu).

Ukuzajiwa Hedonism

Kiakili, burudani inakuza dhana msingi ya njia ya maisha ya Magharibi, ambayo ni kihedonisia. Hedonisia ni nadharia ya kimaadili ya magharibi kwamba furaha kwa namna yoyote ndio jambo zuri na lengo sahihi la maisha ya binadamu. Iliibuka kama makabiliano ya vizuizi vya kanisa katika jamii ya Magharibi juu ya mwenendo wa mtu binafsi. Funzo la msingi kuhusu hedonisia kuwa kusiwepo na vizuizi vya kidini katika harakati binafsi za kujitafutia furaha, maadamu hutadhuru wengine. Burudani za Amerika zinazidi kubainisha aina za burudani katika ulimwengu wa Kiislamu.

Pentagon ya Amerika na Jukumu la CIA

Ni jambo la kumbukumbu kwa umma kwamba Pentagon ya Amerika imekuwa na afisi ya mawasiliano ya burudani tangu 1948 kupitia sheria ya uhuru wa habari wa Amerika, faili zinaonyesha kuwa kati ya 1911 na 2017 zaidi ya kanda 800 za filamu zilipokea msaada kutoka idara ya ulinzi ya serikali ya Amerika (DoD). Hii inajumuisha na franchise blockbuster kama vile filamu ya Transformer, Iron Man na Terminator. Kwenye runinga, zaidi ya majina 1100 yalipata ungwaji mkono na Pentagon, 900 kati yao tangu 2005 kutoka Flight 93 hadi Ice Road Truckers hadi Army Wives. CIA ilipoanzisha afisi ya mawasiliano ya burudani mnamo 1996, ilifanya kazi kwa bidii kwenye filamu ya Al Pacino The Recruit na filamu ya mauwaji ya Osama bin Laden Zero Dark Thirty.

Nyaraka kutoka idara ya ulinzi ya Amerika afisi ya ushirikiano wa burudani huko Pentagon zilifichua uhusiano wa kijeshi juu ya filamu ya John Gunn iitwayo kikosi "Suicide Squad" na “Hearttwarming” inayoonyesha vitendo vya kijasusi vya Amerika. Idara ya kijasusi ya Amerika imetumia washirika wa uhalifu kutekeleza oparesheni chafu, pamoja na kuziyumbisha serikali za Amerika Kusini.

Mafungamano ya Burudani, Vyombo vya Habari na Wabunge

Nchini Amerika, makundi sita ya kimataifa yana miliki na kudhibiti vyombo vyote vya habari, ikiwa ni pamoja na magazeti, majarida, wachapishaji, mitandao ya televisheni, idhaa za kebo, studio za Hollywood, lebo za muziki na tovuti maarufu. Wao ni Time Warner, Walt Disney, Viacom, Rupert Murdoch’s News Corp, CBS Corporation na NBC Universal. Mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari duniani ni Google, akifuatiwa na Walt Disney, Comcast, 21st Century Fox na CBS Corporation. Vyombo vya habari vina uhusiano mkubwa na wabunge wa Amerika na maseneta ambao wanawashawishi na kwa upande wao wanafahamishwa kuhusu upangiliaji wa raia. Taarifa za habari zilizochochewa na jumuia za kimataifa za Amerika zina athari kubwa katika utangazaji wa habari ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu.

Ukuzaji wa Hedonisia katika Ulimwengu wa Kiislamu

Tasnia ya burudani ya Magharibi ina ajenda ya ulimwengu mzima, inamuelekeo fulani katika Ulimwengu wa Kiislamu. Uvamizi wa kithaqafa unafanyika kwa sababu mataifa ya Magharibi yanataka kutambulisha kuwa mfumo wao wa maisha kama mbadala bora zaidi ya mfumo wa maisha wa Kiislamu. Vijana waliolelewa kwenye njia sahihi kwenye mapaja ya mama wanaalikwa kufuata njia ya maisha ya Magharibi, kupitia burudani. Ujumbe wa burudani ya Magharibi ni kufuata matamanio yetu, badala ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Ni kututia moyo kwamba maadam hatumdhuru mtu mwengine yeyote, tunaweza kufanya vitendo vya Haraam katika kujifurahisha.

Kutoridhika na Wajibu

Ni kweli kwamba mwanadamu hupenda na kutopenda vitu na hutenda kutokana na jinsi vinavyo athiri furaha yake. Kwa hiyo binadamu hupima mambo kwa mtazamo wa kufurahisha au kutofurahisha. Walakini, hii ni tofauti na jambo kuwa la halali au haramu kwake. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿

 Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [Baqara 2:216] Hivyo japokuwa mwanadamu anahukumu kuwa hapendi kupigana, anapigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu mtungaji Sheria ameibainisha kuwa ni kheri.

Kutenda Kwa Apendavyo Mwenyezi Mungu (swt)

Uislamu sio njia ya matamanio, ambapo mwanadamu hujishughulisha na kujiepusha kwa msingi wa anachopenda au asichokipenda. Uislamu hupima vitendo na kuacha mambo na matendo kwa msingi wa yale aliyoyaamua Mwenyezi Mungu (swt) na sio kwa matamanio yetu. Mwenyezi Mungu (swt) alionya,

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ﴿

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah al-Maidah 5:49].

Kupenda na kuchukia kwa msingi wa Uislamu

Kwa kuongezea, Uislamu unajenga kupenda na kutopenda kwa mujibu wa hukumu za Kiislamu. Basi mtu huja kupenda kupigana kama ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na kumridhisha Yeye (swt). Tofauti na mtu asiyekuwa na muongozo, Muumini hufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa raha, kwani mielekeo yake imeundwa na yale yote aliyoyaleta Mtume (saw). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema,

 «لا يُؤمنُ أحدُكُم حتى يكونَ هَوَاهُ تبعًا لما جِئتُ بِهِ»“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yafuate yale niliokuja nayo.”

Kwa hivyo, Waumini hawapendi kunywa pombe, kutumia madawa ya kulevya na uasherati, ingawa ni ya kupendeza. Vile vile wanapenda ndoa, Swalah na kuchuma kwa njia za halali.

Vyombo vya habari katika Khilafah

Katika Khilafah vyombo vya habari vitaeneza Ukweli wa Uislamu, utulivu na furaha unaoleta kwa watu binafsi na jamii, uadilifu unaouweka na ubora wa kijeshi wa dola. Zaidi ya hayo, vyombo vya habari vya Khilafah vitafichua uongo na ufisadi wa mifumo iliyotengenezwa na mwanadamu, pamoja na udhaifu wa vikosi vya kijeshi vya adui. Kwa hivyo, vyombo vya habari vitatoa mchango mkubwa katika kueneza Uislamu duniani kote. Ni juu ya Waislamu kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itahakikisha vyombo vya habari vinatekeleza jukumu lake la kuwatoa wanadamu kutoka katika giza la ufuska, kuwapeleka kwenye nuru ya Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Hassan Waleed – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu