Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Maandamano Nchini Iran

Tangu kutokea kwa mapinduzi ya Iran mwaka wa 1979, viongozi wa kidini wa kishi'a wametumia hadhi yao inayo karibiana na ya kiwahyi miongoni mwa raia wa Iran kuwadhibiti na kuwalemaza kuamini kuwa serikali ya Iran imebeba bendera ya Uislamu dhidi ya njama za Kizayuni na Amerika katika kuchukua uongozi wa Mashariki ya Kati.

Uhakika wa mambo ni tofauti kabisa na taswira inayo onyeshwa na serikali hii, kama vile ilivyo kwa serikali ya Saudi katika bara Arabu, serikali ya kidini ya Iran imerahisisha kupatikana kwa maslahi ya kimikakati ya Amerika tangu kubuniwa kwake.

Uvamizi wa Amerika na kuikalia kwake Afghanistan isingeliwezekana lau si kwa usaidizi wa Iran, ambapo Iran ilifunga mpaka wake wa magharibi kuzuia kuingia kwa misaada yoyote kuwafikia wale waliopinga uvamizi wa Amerika.

Zaidi ya hayo, uvamizi wa Amerika nchini Iraq na vitisho dhidi ya Waislamu wa Iraq isingewezekana lau si kwa usaidizi wa serikali hiyo ya kidini hususan katika kuanzisha vita vya kimadhehebu vya makundi yalioegemea upande wa viongozi hao wa kidini kukabiliana na uasi dhidi ya utawala wa Amerika.

Fauka ya yote ni uingiliaji kati wa serikali ya Iran katika kumsaidia dhalimu katili wa Syria ndio iliofichua urongo wa miito ya mapinduzi ya serikali hiyo ya kidini na madai yake ya upinzani dhidi ya umbile la Kizayuni. Iweje serikali inayo foka kuhusu hamu yake ya kutaka kuiangamiza dola ya Kizayuni inaisaidia serikali ya al-Assad, ambayo imedumisha usalama katika mipaka yake kaskazini na umbile la Kizayuni na kulifanya umbile hilo kuwa na usalama kwa zaidi ya miaka 50?

Uingiliaji kati wa serikali hii ya kidini nchini Syria unaangazia ushirikiano wake wa kimikakati na Amerika na usaidizi na ushirikiano wa viongozi hao wa kidini katika kujitanua kwa Amerika eneo la Mashariki ya Kati. Uokozi wa serikali ya al-Assad, ni kipaumbele cha Amerika, kiasi ya kuharakisha kwake katika kuiokoa serikali hiyo inayo poromoka kwa kasi jijini Damascus haikuwa tu kwa kulisahilishia kundi la Hezbollah (wakala wa Iran nchini Lebanon) katika biashara haramu ya mihadarati, 1.kama mlanguzi wa mihadarati kutoka Colombia Marekani ilisafirisha dola 1.7 bilioni pesa taslimu nchini Iran kwa ajili ya kuandikisha wanamgambo wa kishia wa Kihazara na wa Kipakistani kujaza pengo la jeshi la al-Assad linalozidi kupungua. Malipo haya ya pesa taslimu yalifuatiwa na rasilimali huru zenye thamani ya takriban dola 33.6 bilioni ili kuiruhusu Iran kufadhili uingiliaji kati nchini Syria ulio dhaminiwa na Amerika.  

Miito na kelele tasa zitokanazo na ghadhabu feki kamwe haziwezi kuficha sura ovu ya serikali hii ya kidini ya Iran, mauaji ya zaidi ya Waislamu 500,000 nchini Syria, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen na kichinjo cha kila siku katika vita vyake vya kimadhehebu nchini Iraq ni baadhi tu ya natija ya sera za serikali hii ya kidini na uingiliaji kati wake ili kuhifadhi maslahi ya Amerika eneo la Mashariki ya Kati.

Kama ilivyo kwa wateja wengine eneo la Mashariki ya Kati kuendelea kubakia hai kwa utawala wake ni jambo muhimu mno na mazingatio mengine yote yasiyokuwa hili yanachukua nafasi ya pili. Licha ya uchumi wa Iran kuchukua nafasi ya tatu kwa ukubwa eneo la Mashariki ya Kati kwa thamani ya takriban dola 340 bilioni  ufujaji na usimamizi mbaya wa viongozi hawa wa kidini na wapambe wao, na kuendelea kukua kwa gharama za viongozi hawa wa kidini katika kuingilia kati kwao kinyama ili kuhifadhi maslahi ya Kiamerika, imefukarisha raia wa Iran. Licha ya malipo makubwa kutoka kwa Amerika kumekuwepo na upungufu wa asilimia 30 katika viwango vya maisha kwa familia wastani ya Kiirani kwa muda wa zaidi ya miaka 10 sasa, huku nafasi za ajira zaidi ya 26,000 zikipotea katika muda wa wiki moja pekee iliyopita.

Ingawa serikali hii ya kidini itajaribu kuyaonyesha maandamano yanayo endelea kwa sasa kama njama za Kiamerika/Kizayuni/Kiwahabi, idadi ya waandamanaji hawa inakanusha uvumi huu, badala ya waandamanaji hawa kutoka katika jamii zilizo huru, idadi kubwa ya waandamanaji hawa inatoka katika tabaka la wafanyikazi waliofukarishwa na sera za kimadhehebu na kikabila za viongozi hawa wa kidini. 

Huku serikali ya kidini ya Iran na serikali ya Ibn Saud zote zikihitilafiana juu ya utabikishaji sera huru ili kujishindia mapenzi ya Amerika kwao, Waislamu hawana budi kutambua kuwa licha ya utiifu uchukizao wa mataifa haya kwa Amerika, misimamo yao inazidi kuwa mibaya kila uchao kwa kuwa biladi yoyote ya Kiislamu yaweza kufukarishwa na kuporomoshwa na vikwazo na sera za kibiashara za kimagharibi. Bali upinzani dhidi ya ukoloni wa kimagharibi unaweza kupatikana pekee kupitia umma wa kiulimwengu uliounganishwa chini ya Khalifah anaye fanya kazi kwa ajili ya maslahi ya Uislamu na Waislamu.  

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muzzamil Hussain

  1. http://www.newsweek.com/hezbollah-cocaine-smuggle-united-states-obama-751928
  2. https://www.cbsnews.com/news/u-s-paid-1-3-billion-to-iran-two-days-after-cash-delivery/
Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:25

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu