Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Pindi Akili Inapokuwa Mtunzi wa Sheria, Taharuki Hutawala

Miaka mitano iliyopita, Profesa Miroslav Djordjevic, mtaalamu wa upasuaji na urekebishaji viungo vya uzazi anayeongoza duniani, alipokea mgonjwa katika kliniki yake ya Belgrade. Alikuwa ni mgonjwa aliyejibadilisha jinsia yake aliyefanyiwa upasuaji katika kliniki nyengine kuondoa uume wake – na tangu wakati huo amebadili mawazo yake. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Djordjevic kuagizwa kufanya ile inayo itwa" upinduaji" wa upasuaji. Katika miezi sita mengine, watu wengine sita walikutana naye, vile vile wakitaka pia kupinduliwa kwa upasuaji wao.  (National Post).     

Kama Waislamu tunaamini kuwa akili ya mwanadamu ina kikomo katika utambuzi juu ya maisha. Pia tunafahamu kwamba akili ya mwanadamu huathiriwa na mazingira iliyomo ndani yake na hivyo basi haina dawamu katika kufanya maamuzi. Ni kutokana na sababu hizi ambapo Waislamu hawaichukui akili ya mwanadamu katika kufikia uhakika thabiti wa ni nini sahihi na nini kosa au ni nini kheri na nini shari kwani yote haya daima hubalika na huwa na uwezo wa kupatikana dosari ya ni kitu gani kitakachomletea mtu binafsi na jamii kheri na furaha.

Fikra hii moja kwa moja hutokamana na Aqeedah yetu (ya kimaisha) inayo tufunza kwamba twahitaji kuwa na imani ya kukatikiwa kwa Allah (swt) na yale aliyotuteremshia kupitia Qur'an na Mtume wake Muhammad (saw) na kwamba kupitia yeye pekee ndio hujifunza kile kinachotakiwa kukadiriwa na kuonekana kuwa sahihi au kosa. Pia tunajifunza kuwa furaha imefungamanishwa moja kwa moja na kufuata muongozo kuhusiana na lile ambalo ni sahihi na kosa kwani hili ndilo litakalo pelekea utafutaji radhi za Allah na kupelekea Waislamu kupata furaha.    

Kwa kufungamanisha ufahamu huu na yale tuliyopata katika makala ya juu, inadhihirisha wazi kuwa kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wanaohisi majuto baada ya kufanyiwa upasuaji na urekebishaji wa nyeti zao, matokeo ya hili ni jambo ambalo kihakika lapaswa kuwa mshangao kwa Waislamu. Ama kwa mtazamo wa Kiislamu aina hizi za upasuaji ni haramu/makosa na kamwe hazipelekei kwenye mafaniko wala furaha katika maisha haya wala ya akhera, kutokana na yafuatayo:

Imethibitishwa katika al-Sahih kuwa 'Abdallah ibn 'Abbas (ra) amesema: 

«لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم المتشبهين من الرجال بالنساء، والمتشبهات من النساء بالرجال»‏ Mtume wa Allah (saw) amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake na wanawake wenye kujifananisha na wanaume. (al-Bukhari).

Habari za watu kujutia kubadilisha jinsia zao kihakika zimekuja kama mshtuko kwa Profesa Djordjevic aliyehojiwa katika makala hayo na kama mtaalamu wa upasuaji na urekebishaji wa viungo vya uzazi aliposema: "linaweza kuwa janga la kikweli kusikia hadithi hizi". "Wale wanaotaka kupindua upasuaji huu, wameongea naye juu ya viwango vikubwa vya msongo wa mawazo kufuatia kipindi chao cha mpito baada ya upasuaji huo na katika kesi nyengine hata kufikiria kujiua." Daktari huyu ana hofu kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha maombi ya kutaka upinduaji wa upasuaji na pia ukosefu wa utafiti wa kielimu juu ya suala hili. Ameonyesha wasiwasi wake juu ya utaratibu unaofuatwa wakati wa kutoa maamuzi juu ya upasuaji huu.

Haya ndio haswa tunayo tarajia kwa mtu anaye liangalia suala hili kwa msingi wa aqeedah tofauti ya kimaisha isiyokuwa Aqeedah ya Kiislamu. Mfumo huru wa kimaisha wa kiilmani, aqeeda iliyojengwa juu ya msingi wa maridhiano na kutenganisha dini na maisha. Aqeeda inayoamua nini ni sahihi na nini ni kosa, kwa kutegemeza kipimo cha maslahi, inayopelekea kupatikana kwa kitendo, ambayo hutegemea furaha juu ya starehe za mwili anazopata mtu. Sasa basi ikiwa maslahi na furaha iliyopatikana kutokana na upasuaji wa aina hii yako chini ya uangalizi, fikra yote kuhusu utaratibu huu inahitaji pia kutathminiwa upya. Hili bila shaka ni jambo ambalo vuguvugu la kutetea ubadilishaji jinsia halingependa kulisikia kwani tunaposoma zaidi katika makala hayo yanaashiria kuwa ndilo sababu kubwa inayozuia vyuo vikuu kutofanya utafiti juu ya kadhia hii. Hii ni kwa sababu utafiti huu unavunjilia mbali porojo yao kuwa upasuaji huu ni jambo la lazima ili watu hawa waweze kupata furaha. 

Ni muhimu kwa Waislamu leo, hususan wale wanaoishi nchi za magharibi kulielewa suala hili vyema kwani huenda wakakabiliwa na shinikizo kubwa la kukubali fahamu kama kadhia za ubadilishaji jinsia, ukhanithi, mahusiano ya kijinsia nje ya ndoa na kadhalika kama tabia zinazo kubalika ndani ya jamii.

Kivitendo hii humaanisha kwamba fikra hizi zitatekelezwa na kupigiwa debe ndani ya jamii kama haki ya mtu binafsi kutafuta na kutimiza starehe na furaha zao. Wataziwasilisha kwa kuruhusu haki hizi, kama ishara ya mtu au jamii ya kisasa, iliyoendelea, iliyo staarabika, na iliyo na uadilifu, na kwenda kinyume na haya kuoneka kama dhulma na ushamba kwa mtu binafsi au jamii.  

Pindi sisi kama Waislamu, tutakapo fahamu maumbile yenye kikomo ya akili ya mwanadamu, na hatari za kuiruhusu kuamuru lipi ni sahihi na lipi ni kosa, na kwamba Allah pekee ndiye mwenye ujuzi kamili wa lipi ni zuri kwa watu binafsi pamoja na jamii – ndipo tutakapo weza kukataa shinikizo hizi za kukubali fahamu ambazo zinagongana na Uislamu wazi wazi.

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ

“Na hukumu baina yao kwa yale yote aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na ikiwa wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu."  [Al-Maaida: 49]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:26

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu