Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Maisha haya ya dunia si chochote bali ni mafupi,
kwa hiyo Tumcheni Mwenyezi Mungu (swt) kikamilifu

Uendaji mbio, uchangamfu, uchukuliaji mambo kwa udharura na upangaji mipango na ufuatiliaji katika kufanya da’wah tuliouona katika maisha ya Mtume (saw) ilikuwa sio eti ana “dhibiti wa wakati”. La, ilikuwa ni athari ya kukatikiwa juu ya maisha haya ya dunia, kama ilivyo pambanuliwa katika yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliyoyaeleza. Hakika, uhai umedhihirishwa kuwa ni mfupi, hata na wale ambao wameishi muda mrefu miongoni mwa watu.
Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُو

“Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, Basi tufani liliwachukua, nao ni madhalimu.” [Al-Ankabut: 14]

Mtume (saw) alisema:
فَلَمَّا أَتَاهُ مَلَكُ الْمَوْتِ، قَالَ: يَا نُوحٌ، يَا أَكْبَرَ الأَنْبِيَاءِ، وَيَا طَوِيلَ الْعُمُرِ، وَيَا مُجَابَ الدَّعْوَةِ، كَيْفَ رَأَيْتَ الدُّنْيَا؟ قَالَ: مِثْلَ رَجُلٍ بُنِيَ لَهُ بَيْتٌ لَهُ بَابَانِ، فَدَخَلَ مِنْ وَاحِدٍ، وَخَرَجَ مِنَ الآخَرِ
“Malaika wa mauti alikuja kwa Nuhu (as) na kumuuliza: Ewe Nuhu, Mtume uliyeishi miaka mingi zaidi, uliyaonaje maisha haya ya dunia na starehe zake? Akajibu: Ni kama mtu niliyeingia katika chumba kilicho na milango miwili, na nikasimama katikati ya chumba kwa muda mfupi, kisha nikatoka kwa mlango mwengine”

Huo ndio mtizamo wa Nuhu (as) aliyeishi karne tisa na nusu, je, sisi tuyatizame vipi maisha yetu Ummah wa Muhammad (saw); ambayo Mtume (saw) alisema:

«عُمُرُ أُمَّتِي مِنْ سِتِّينَ سَنَةً إِلَى سَبْعِينَ سَنَةً»

“Maisha ya Ummah wangu ni kuanzia miaka sitini hadi sabini.” [Tirmidhi]

Je sisi sio kama ambao tunazaliwa karibu na mlango tunaotakiwa kutoka? Au sio hivyo? Je kweli tunayo maisha ya kutosha kiasi kwamba tucheleweshe kuiendea mbio Dini yetu? Ni jukumu la kila mmoja wetu kwenda mbio kuhakikisha kuwa umri wake haukupotea bure. Kila siku na kila sehemu ya siku yetu lazima ihesabike kwa kuishi maisha yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt).
Hakika maisha haya ya dunia si chochote bali ni mafupi na Siku ya Kiyama, yatakumbukwa hivyo na wale ambao hawakumcha Mwenyezi Mungu (swt). Watakuwa wameumaliza umri wao katika michezo na kuyakimbilia matamanio yao. Watakuwa katika waliokata tamaa kutokana na kuumaliza uhai wao na watadai kuwa umri wao ulikuwa ni siku moja au sehemu ya siku.

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ * قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ * قَالَ إِنْ لَبِثْتُمْ إِلاَّ قَلِيلاً لَوْ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ * أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لاَ تُرْجَعُونَ * فَتَعَالَى اللَّهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ

“Mwenyezi Mungu Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka? Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu. Mwenyezi Mungu Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua. Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A’rshi Tukufu.” [Al-Muminun: 112 -116]

Hivyo tunatakiwa kuzitumia vipi siku au sehemu ya siku zetu? Kwa kipimo kipi tunatathmini kuwa siku nzima iliyotumika kuwa na familia, au kukaa afisini hadi usiku sana kwamba ni kuutumia vyema muda; lakini masaa kadhaa kuyatumia katika kazi ya kulingania kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume kwamba ni muda uliopotea? Tunawezaje kupumzika majumbani mwetu siku yoyote au sehemu ya siku ilhali Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) haitekelezwi, damu ya Waislamu inanyunyizwa katika ardhi, ardhi za Waislamu zimevamiwa na watu duni katika binadamu na Waislamu wametawanyika katika ulimwengu kama wakimbizi, wakizama baharini wakimbia au wakilala peupe kwenye baridi na bila chakula? Je ni kweli tunao muda wa kupumzika na je, huu ni muda wa kupumzika?

Tusikubali kudanganywa na shetani kuhusu kuwepo kwetu hapa duniani. Si tu kwamba maisha haya ni mafupi bali kwa hakika ni mafupi ukilinganisha na ya Akhera yenye kudumu.

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا مَتَاعٌ

“...Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo. [Ar-Rad 13: 26]

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ

“Sema: Starehe ya dunia ni ndogo.” [An-Nisa' 4:77]

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

يَا قَوْمِ إِنَّمَا هَٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَإِنَّ الْآخِرَةَ هِيَ دَارُ الْقَرَارِ

“Enyi watu wangu! Hakika haya maisha ya dunia ni starehe ipitayo tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima.” [Ghafir: 39]
Mtume (saw) alisema:

«وَاللَّهِ مَا الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ مِثْلُ مَا يَجْعَلُ أَحَدُكُمْ إِصْبَعَهُ هَذِهِ - وَأَشَارَ يَحْيَى بِالسَّبَّابَةِ - فِي الْيَمِّ فَلْيَنْظُرْ بِمَ يَرْجِعُ»

“Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, hii dunia (si chochote ukiilinganisha) na Akhera ni kama mmoja wenu akitie kidole chake katika bahari na kisha akitoe aangalie kilichobakia kidoleni mwake.” [Muslim]

Hivyo basi, kwa nini tuiache bahari kwa kile kisichojaza hata kidole, tukienda mbio kwa masaa, masiku, mawiki na miezi? Tusipoteze muda kwa vitu ambavyo havina maana ambavyo vitatupelekea kutoshughulikia matendo ambayo tumeamrishwa juu yetu. Hakika, lazima tuchunge wakati tukiiendea mbio dunia kila dakika, saa na siku ili tuweze kupata nafasi ili kufanyiakazi yale mambo muhimu kuhusiana na Akhera yenye kudumu.
Sio tu kwamba maisha ya dunia ni mafupi bali pia yanaweza kuisha wakati wowote. Hakuna kuepuka au kukimbia kifo. Wakati wa kifo hatuujui sisi, sasa iweje kuhairisha kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha? Kuhairisha huko kumejengwa juu ya kujidanganya binafsi, matumaini ya kirongo na mtizamo finyo.

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ

“Utakapofika muda wao basi hatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia.” [Al-Aa'raf 7:34]

Mtume (saw) alisema:
«أَكْثِرُوا ذِكْرَ هَاذِمِ اللَّذَّاتِ » “Kila mara kumbuka muuaji wa furaha, akimaanisha kifo.” [Ibn Maajah]

Hatutakiwi kuchelewesha mambo ya Dini yetu kwa matumaini kuwa bado tutakuwepo mwezi ujao, wiki ijayo, kesho au hata saa ijayo. Matumaini hayo ni ya uongo. Hakika, mwanadamu hufikwa na kifo kabla matumaini hayo hayaja kamilika.
Mtume (saw) alichora mistari michache na kusema:

«هَذَا الأَمَلُ وَهَذَا أَجَلُهُ، فَبَيْنَمَا هُوَ كَذَلِكَ إِذْ جَاءَهُ الْخَطُّ الأَقْرَبُ»

“Haya ni matumaini ya mwanadamu, na haya ni mauti yake ghafla, na wakati yupo katika hali ya matumaini, ndivyo kifo kinavyomjia” [Bukhari]

Tunawezaje kuupa mgongo mwito wa ulinganizi wa Khilafah ili kujiunga na kazi ya kusimamisha utawala kwa Shari’ah iliyoshukishwa na Mwenyezi Mungu (swt)? Tunawezaje kuhairisha juhudi muhimu za kusonga mbele katika kupambana na utawala wa kikafiri? Kwa nini ucheleweshe hadi kesho lile ambalo laweza kufanyika leo? Je hii sio kasi inayotakiwa kuwa nayo baada ya kuona kwamba twaweza kufa wakati wowote? Ikiwa hatuendi kwa kasi inayostahiki, je si lazima tubadilishe mazoea yetu ili tuweze?

Hakika maisha ya dunia ni mafupi, kwa hiyo tuyafanyie kazi vilivyo. Mipango, matamanio na furaha ya dunia hii yasitushughulishe na kuchukua muda wetu, kiasi kwamba hatuna nafasi iliyobakia kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) haki kamilifu.
Mtume (saw) alisema:

«كُنْ فِي الدُّنْيَا كَأَنَّك غَرِيبٌ أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ»

“Ishi katika dunia hii kama ambaye ni mgeni au msafiri.” [Al-Bukhari]

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ

“Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha nay a Akhera ni chache.” [At-Tawba: 38]
Muislamu anaishi kama msafiri, anapita kupitia uhai, na haishi kama ambaye anaishi milele hapa. Hafikirii mara mbili kuhusu kubadilisha kazi lau inachukua muda wake ambao angelikuwa anafanya Da’wah au inayomchokesha kiasi kwamba haimpi nafasi ya kuwa katika uchangamfu kubeba Da’wah. Atapunguza mipango yake ya kuboresha biashara yake, kujiendeleza kiajira, kununua nyumba, kusomesha wanawe na kumfurahisha mkewe kwa sababu muda wake mwingi muhimu anautumia katika ulinganizi wa Uislamu.
Ukimuona utaona ishara ya ukosefu wa usingizi na mapumziko ndani ya mtu huyu. Licha ya hali hiyo, ukimuambia azidishe Da’wah, atakuwa tayari kufanya hivyo, kwa hiyari na bila kulalamika. Anafahamu fika uzito wa hotuba ya Mtume (saw) pale aliposema:

«لَا رَاحَةَ بَعْدَ الْيَوْمِ يَا خَدِيجَةُ» “Hakuna kupumzika baada ya siku hii, Ewe Khadija.”

Ni yule anayekwenda mbio kwa malengo, bila kuhairisha au kusitasita kila anapojua kuna jambo la kufanywa kwa ajili ya Dini yake. Imesimuliwa na ‘Uqba bin Al-Harith: Siku moja Mtume (saw) alipomaliza kuswali swala ya Asr aliondoka kwa haraka kuelekea nyumbani kwake na kurudi mara moja. Mimi (au mtu mwengine) tukamuuliza kuna tatizo gani na akajibu:

«كُنْتُ خَلَّفْتُ فِي الْبَيْتِ تِبْرًا مِنَ الصَّدَقَةِ، فَكَرِهْتُ أَنْ أُبَيِّتَهُ فَقَسَمْتُهُ» “Nimewacha nyumbani kipande cha dhahabu ambacho kilikuwa ni cha Sadaka na sikupenda kibakie mpaka usiku katika nyumba yangu, hivyo nimeenda kukichukua nikigawanye” [Bukhari]
Muislamu ni yule anayekimbilia bila kupoteza wakati katika kuendeleza ulinganizi wa mwito wa Mwenyezi Mungu (swt) hata kama ni hatari kwake yeye. Muslim amesimulia kuwa imeripotiwa kutoka kwa Ana b. Malik alisema: Mtume (saw) alimtuma Busaisah kama jasusi kuangalia msafara wa Abu Sufyan umefikia wapi… Washirikina wakawa wanatunyemelea na Mtume (Saw) akasema:

«قُومُوا إِلَى جَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَوَاتُ وَالأَرْضُ» “Inuka uingie Peponi ambayo upana wake ni sawa na mbingu na ardhi.”

'Umair b. al- Humam al-Ansari alisema: يَا رَسُولَ اللَّهِ جَنَّةٌ عَرْضُهَا السَّمَوَاتُ وَالأَرْضُ “Mtume wa Mwenyezi Mungu, Pepo ni sawa na urefu baina ya mbingu na ardhi?”

Mtume (saw) alisema
نَعَمْ “Naam.” 'Umair alisema: بَخٍ بَخٍ “Ubora ulioje!” Mtume (saw) akamuuliza: «مَا يَحْمِلُكَ عَلَى قَوْلِكَ بَخٍ بَخٍ» “Nini kilichokufanya utamke maneno hayo?" Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, لاَ وَاللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِلاَّ رَجَاءَةَ أَنْ أَكُونَ مِنْ أَهْلِهَا “Si lolote bali ni hamu ya kuwa miongoni mwa wakaazi wake” Mtume (saw) akamwambia: «فَإِنَّكَ مِنْ أَهْلِهَا» “Hakika wewe ni miongoni mwa wakaazi wake.” Umair akatoa tende kutoka katika begi lake na kuanza kuzila. Kisha Umair alisema: لَئِنْ أَنَا حَيِيتُ حَتَّى آكُلَ تَمَرَاتِي هَذِهِ إِنَّهَا لَحَيَاةٌ طَوِيلَةٌ “Lau nitaendelea kuishi ili nile hizi tende zote zangu, itakuwa muda mrefu." (Msimuliaji alisema): Alizitupa tende zote alizokuwa naz. Kisha akapigana na maadui mpaka akauawa.” Hakika Muislamu hacheleweshi kujitoa muhanga hata kama ni kula mlo wake wa mwisho duniani.

Hakika maisha ya dunia hii si chochote bali ni mafupi na mwisho wake haujulikani na mtu yeyote, kwa hiyo tumcheni Mwenyezi Mungu (swt) kikamilifu. Lau tunazembea, tuzinduke kutoka katika kususuwaa hadi kufanya kazi. Ikiwa twatembea tuongeze kasi yetu. Tukamilishe mipango ya leo, leo, ili kesho tuzindue mipango mingine. Tuyafanye majukumu ya Dini na ya Ummah wetu yaamue kasi na sio kwamba majukumu haya yawachwe kutokana na kasi yetu. Twendeni mbio tukiwa wachangamfu na nishati ili umri wetu katika maisha haya mafupi yahesabiwe vilivyo wakati tutakaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikiwa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na
Musab Umair – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:48

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu