Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Athari ya Kuvunjika kwa Familia Juu ya Watoto na Jamii

Bwana Hakimu Coleridge, aliyekuwa hakimu wa familia nchini Uingereza akiwa na tajriba ya zaidi ya miaka 37 kuhusiana na sheria ya familia alilinganisha kuvunjika kwa maisha ya familia kuwa ni maangamivu sawa na athari ya mvuke wa kidunia. Alielezea kuwa ni tatizo linalo athiri nyanja zote za jamii na kwamba kila siku mahakimu kama yeye wanashuhudia “sherehe zisizoisha” za mahangaiko ya wanadamu, na kwamba “uovu wote wa jamii ukifuatiliwa unatokana na kuanguka kwa umadhubuti wa familia.” Bwana Coleridge hayuko pekee katika kuelezea athari za maangamivu ya kuvunjika kwa familia. Katika ripoti ya Kitengo cha Haki kwa Jamii (CSJ), ilionya kwamba Uingereza iko ndani ya “tsunami” ya kuvunjika kwa familia na athari mbaya juu ya watoto na jamii. Kuvunjika kwa maisha ya familia sio tatizo la kipekee kwa Uingereza bali ni tatizo la kiulimwengu, likitofautiana tu katika ukubwa ndani ya nchi tofauti. Tatizo linaonekana kuendelea kukuwa haraka ndani ya nchi ambazo maadili ya uhuru ya kimagharibi ndiyo yamepewa kipaombele. Kunukuu maneno ya mwanasiasa mkuu na mwenye tajriba wa Australia, Kevin Andrews, “Tishio kubwa linaloukumba ulimwengu wa kimagharibi sio mvuke wa kidunia, janga la kifedha au Uislamu wa misimamo mikali, bali ni kuendelea kuvunjika kwa miundo muhimu ya jamii ya umma –ndoa, familia na jamii.”

Vigezo kadhaa vinaweza kutajwa kama sababu ya kwa nini familia zinavunjika. Uzinifu, matatizo ya kifedha, vurugu, pombe na madawa ya kulevya ni baadhi tu ya sababu za kwa nini tunaona familia za vunjika. Matatizo yote haya yana athari mbaya kwa kila mtu ndani ya sehemu ya familia, lakini watoto ndiyo wahanga dhaifu wanaoathiriwa na kuvunjika kwa familia. Hii inatokana hususan kwa sababu ya kuwategemea wazazi ili kuwasaidia kukuwa watu wazima. Maisha ya familia katika kesi nyingi hutakiwa kubuni jengo imara la watoto kuendelea na kukuwa maishani. Lakini sehemu ya familia inapoanguka, watoto huwachwa na ukosefu wa umadhubuti na kuwasababishia kukukosa mtizamo muhimu wa utotoni ambao ni muhimu kwa maisha.

Mahusiano na Wazazi:

Athari kubwa inayopatikana kwa watoto baada ya familia kuvunjika ni wao kukosa mahusiano na mmoja au wazazi wote.

Kwa mfano, wazazi wanapotengana, watoto mara nyingi hukulia ndani ya familia ya “mzazi mmoja” ambapo mara nyingi zimepelekea kupunguza au kupoteza mawasiliano na mmoja wa wazazi. Huko Uingereza na Marekani thumuni moja ya watoto wanalelewa bila baba yao mzazi (Afisi ya Takwimu Marekani na Afisi ya Takwimu ya Uingereza). Uingereza takribani watoto milioni moja wanakuwa bila kuwepo kwa baba katika maisha yao (CSJ). Takwimu hizi zimekuwa zakushtusha zaidi wakati ambapo utafiti wa hivi majuzi uliofanywa na Harry Benson, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika shirika hilo la Uingereza la Msingi wa Ndoa, unaonyesha kuwa “kukosekana kwa baba ndani ya nyumba imebakia kuwa chanzo nambari moja katika kutabiri matatizo ya kiakili kwa vijana ndani ya Uingereza.” Iko wazi kuwa watoto wanapokuwa bila baba ndiyo inayowapelekea kuwa dhaifu kwa ujumla.

Ikiwa haitoshi kwa watoto wengi kuwa na mawasiliano na mmoja wa wazazi yatakuwa machache au kukosekana kabisa baada ya kuvunjika, basi pia kuna ushahidi kuwa mahusiano na mzazi ambaye watoto wanakulia naye, hupungua kwa vigezo kadhaa. Kwa mujibu wa (Pryor, J. and Rodgers, B. (2001) Children in Changing Families. Oxford: Blackwell) Moja katika vigezo ni mahitaji ya mzazi mmoja, mara nyingi mama, kwa kuwa mtafutaji mkate wa familia kiasi kwamba hulazimishwa kuwakabidhi watoto wao katika mikono ya wengine kuwaangalia na mara nyingi kuwalea kutokana na majukumu ya kikazi. Huku sehemu ya familia inapokuwa ndogo kila miaka inavyoendelea watoto wanawachwa katika malezi ya watu wasiokuwa muhimu au wanawachwa kujitafutia wenyewe kama “watoto machokoraa” wanaorudi kutoka shule na kuingia nyumba iliyotupu na wanamotakiwa kujisimamia ikijumuisha kujiandalia chakula. Zaidi ya hayo msongo wa mawazo kwa baba na mama uko juu kutokana na talaka, hii ikipelekea mihemko zaidi kwa mahusiano ya mtoto na mzazi.

Athari Mbaya ya Kiuchumi:

Baada ya kuvunjika kwa familia, hali ya kiuchumi ya watoto hubadilika kimsingi.

Utafiti uliofanywa Marekani unaonyesha kuwa mama mlezi anapata hasara ya kati ya asilimia 25-60 ya mapata yake kabla talaka. Kina mama asilimia 50 walipata makubaliano ya msaada kwa watoto na asilimia 25 ya kina mama ambao kihakika walikubaliwa kupewa msaada, hawakupata malipo. (US Census Bureau. 2011. Divorce Rates Highest in the South, Lowest in the Northeast, Census Bureau Reports United States Census Bureau Web Site.) Uingereza familia za mzazi mmoja ndizo ambazo zinatarajiwa kuishi katika umasikini wa kifedha. Wazazi pweke wanatarajiwa kuishi mara 2.5 zaidi chini ya asilimia 60 ya mapato ya kati na kati. Asilimia 41 ya watoto kutoka kwa familia za wazazi pweke wanaishi chini ya asilimia 60 ya mapato ya kati na kati baada ya gharama za nyumba. (CSJ, Fractured Families) Kumnukuu mwalimu kutoka Uingereza kinachomaanisha kutoka mashinani: “Tunawaona watoto wasiokula kabla muda wa mchana. Wengi hawawezi kumiliki sare na viatu. Na wengi wanawalea wadogo zao peke yao.” Watoto wanaoishi katika umasikini ni takribani mara mbili zaidi wanaotarajiwa kuishi katika nyumba mbaya. Hili lina athari kubwa juu ya miili na akili zao pamoja na kufaulu kwao kielimu.

Athari za Kijamii, Kihisia, Kiuwezo wa Kitabia na Afya ya Kiakili Juu ya Mtoto:

Kama jamii tunahitaji kufahamu kwamba katika mahusiano mengi tofauti tofauti ambayo watu huwanayo kwa muda wa maisha yao, mahusiano kati ya mzazi na mtoto ni moja miongoni mwa ambayo ni muhimu. Namna wazazi wanavyotendeana na wanavyowatendea watoto wao, itakuwa ni kiashiria kikubwa cha namna watakavyokuwa ukubwani na dori watayoweza kucheza katika jamii. Huku mahusiano kati ya mzazi na mtoto yanapozidi kudorora kutokana na hali ya familia, tunaona kwamba watoto kutoka katika familia zilizovunjika wanapoteza kwa ujumla hisia ya kustahiki kuwa sehemu fulani. Hisia hii inamaanisha kujihisi kukubalika na kuthaminiwa kama mwanachama au sehemu ya kitu. Ni fikra muhimu tunayohitaji kuihisi ili tuweze kuyaendea masuala yanayotuzunguka na kupambana na mazito maishani mwetu.

Wajuzi wamependekeza kuwa fikra hii muhimu inakosekana ndani ya vijana wengi kutoka katika majumba yaliyovunjika na ndiyo kigezo kikubwa kinachopelekea vijana kuingia katika magenge. Inaweza kuwa sababu ya kwa nini tunaona ongezeko la uhalifu wa magenge. Vijana wengi wanaona kuwa uanachama katika magenge ni kama mbadala wa familia na yanayowapatia hisia hiyo ya kustahiki kuwepo sehemu fulani. Katika mahojiano na wanachama wa magenge kutoka Marekani, yaliyofanywa na Joe Killian, muandishi wa News and Record, wanachama wengi walisema kwamba, “Kuwa ni sehemu ya genge inamaanisha kuwa hauko peke yako katika dunia, ambayo ni sawa na vile watu wengi wanavyoelezea kuwa ni sehemu ya familia iliyoshikamana au kundi la marafiki.”

Zaidi ya hayo, uamuzi ufuatao ulipeperushwa katika ripoti na Muungano wa Kitaifa wa Uingereza wa Muungano wa Wakuu wa Shule wa Walimu wa Kike uliosisitiza dori ya kuvunjika kwa familia kuwa ndiyo imepelekea kukua kwa tamaduni za magenge ndani ya Uingereza. Ilisema kwamba kuvunjika kwa familia na kukosekana kwa baba kama msimamizi inawezekana kulaumiwa kuwa chanzo cha wanafunzi kujiunga na magenge, “Watoto wa umri wa miaka tisa wanahusishwa na uhalifu wa kupangiliwa ili wapate kuhifadhiwa na kupata “hisia ya kustahiki kuwa sehemu” kwa sababu ya kukosekana viigizo kutoka nyumbani.”

Hali ya ustawi jumla ya watoto pia inaathiriwa kutokana na familia zao kuvunjika. Ilipatikana kuwa ustawi jumla wa watoto kutoka katika nyumba zilizovunjika uko chini ikilinganishwa na watoto wanaotoka katika familia za wazazi wawili. Tathmini kubwa juu ya watoto wa wazazi walio talakiana ya (Amato 1991 and 2001: Children of divorce in the 1990s: an update of the Amato and Keith (1991) meta-analysis. Journal of Family Psychology,15, 355-70) iligundua kuwa watoto kutoka katika familia za talaka walikuwa na kiwango cha chini kutokana na athari ikijumuisha kufaulu kielimu, kitabia, marekebisho ya kisaikolojia (kiakili), dhana ya kibinafsi, uwezo wa kijamii na afya ya muda mrefu. Katika utafiti mwengine, ushahidi uligundua kuwa watoto kutoka kwa wazazi waliotengana wanauwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya kitabia na wanaweza kufanya vibaya shule na kuacha shule wakiwa na viwango vya chini vya kuhitimu. (Pryor, J. and Rodgers, B. (2001) Children in Changing Families. Oxford: Blackwell). Utafiti mwengine ni kuwa watoto ambao wazazi walio talakiana wanaweza kuwa na viwango vya chini juu ya dhana ya binafsi na mahusiano ya kijamii (Amato 2001) na kwamba wasiwasi na msongo wa mawazo huzidi baada ya tukio la talaka (Strohschein 2005Parental divorce and child mental health trajectories. Journal of Marriage and Family 67: 1286.)

Mzigo wa familia kuvunjika juu ya ujumla wa maendeleo ya hisia kwa watoto pia iliwekwa wazi na utafiti uliofanywa Sweden ambapo takribani watoto milioni moja ulionyesha kuwa watoto wanaokuwa wakiwa na wazazi pweke wanauwezo wa kupata mapungufu ya kiakili makubwa, kujaribu au kujitoa uhai au kudumu na kunywa pombe. Takwimu za kushtusha kutoka Marekani juu ya athari ya kukosekana baba nyumbani na maendeleo ya watoto zimeonyesha namna gani tatizo lilivyokubwa. Kwa mfano Marekani asilimia 63 ya vijana wanaojitoa uhai wanatoka katika nyumba zisizokuwa na baba (US Department of Health) na watoto wa kutoka nyumba za wazazi pweke ni mara mbili zaidi kuwa wanauwezo wa kujitoa uhai (Irwin Sandler, PhD, professor of psychology and director of the Prevention Research Center, Arizona State University, Tempe). Zaidi ya hayo, utafiti wa watoto 1,977 wa umri wa miaka 3 na zaidi wanaoishi na baba nyumbani au msimamizi kama baba iligundua kuwa watoto wanaoishi na wazazi wadamu waliooana walikuwa na kiwango cha chini cha matatizo ya kitabia katika kujieleza na kujiamulia kuliko watoto wanaoishi na mzazi mmoja asiyekuwa wa damu. (Hofferth, S. L. (2006). Residential father family type and child well-being: investment versus selection. Demography, 43, 53-78.). Pia kuna matumizi makubwa ya madawa ya kulevya kwa watoto wasioishi na baba na mama yao. (Hoffmann, John P. “The Community Context of Family Structure and Adolescent Drug Use.” Journal of Marriage and Family 64 (May 2002): 314-330.)

Zaidi ya hayo, utathmini wa takribani familia 11,000 uliyofanyika ndani ya Uingereza uligundua kuwa kuvunjika kwa familia ndiyo chanzo hatari cha kipekee kwa afya ya kiakili kwa watoto wanapo baleghe na kuwepo kwa wazazi waliotengana ni athari kubwa ya kipekee juu ya afya ya kiakili kwa wasichana hususan matatizo ya kihisia. Na kwa pamoja ni kigezo kikubwa katika afya ya kiakili ya vijana ikiwa na mahusiano ya matatizo ya kitabia (The Times)

Imesemekana kuwa kuzidi kwa maradhi ya kiakili ni kutokana na kukosekana kwa furaha ndani ya jamii. Huku idadi ya msongo wa mawazo na wasiwasi miongoni mwa vijana, na idadi ya watoto na vijana wanaozuru ndani ya kitengo cha Ajali na Dharura (A&E) wakiwa na matatizo ya kiakili ikizidi ndani ya miaka 10 na huku idadi ya wanaosajiliwa hospitalini katika vijana walio na matatizo ya kula ikizidi. (The Independent) Serikali kamwe haziwezi kupinga kuzidi kwa idadi ya vijana ambao wameathirika kihisia na kiakili kutokana na kuvunjika kwa familia na kinachoashiriwa ni kuhusu maadili na mwenendo wa maisha ya jamii ambazo serikali hizi zinatawala juu yake.

Katika jamii zote za kimagharibi, familia pana zimepotea kabisa, na kwamba utamaduni wa wazazi wawili umezidi kupungua kutokana na idadi kubwa ya talaka, kuoana tena, kuchukuana, uzazi wa upweke na mahusiano ya jinsia moja yote yamezidi. Matokeo ya mabadiliko haya juu ya jamii kiujumla hususan maisha ya watoto yamekuwa yakushtusha. Ilhali serikali zajitia hamnazo katika kutoa suluhisho. Hili si la kushangaza kwa kuwa ndiyo maadili huru ya kisekula na nidhamu wanazopigia debe na kutekeleza juu ya dola zao na ambazo zimesababisha michafuko katika jamii. Lakusikitisha, inatarajiwa kuwa maangamivu yanayotokana na kuvunjika kwa familia yataendelea na hata kuzidi katika miaka ijayo, ikimakinisha mahangaiko kwa wengi hususan wachanga.

Imeandikiwa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:16

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu